Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,045
Leo niko napitapita kwenye vijiwe mbalimbali hapa BK mjini. Nimejulishwa kuwa katika Mkutano wa Mbunge uliofanyika hivi karibuni, wananchi wamempa ishara ya taa nyekundu Kagasheki.
Simulizi liko hivi:
Hivi karibuni Lwakatare, Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala-CDM na kijana mmoja toka Singida ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu-CDM walikuja Kagera kwa programme ya kichama ya kuwanoa madiwani wa CDM. Baada ya Programme, Chama-Mkoa kikawaandalia mkutano wa hadhara.
Wakati wa kuhutubia, Kijana toka Singida akamwaga sumu kwa kuwaambia watu waliohudhuria mkutanoni kuwa; msitegemee lolote jipya toka kwa Kagasheki eti kwa kuwa amekuwa Waziri Kamili. Akawaambia labda niwape swali akija mmuulize hivi Twiga wetu wanarudi lini? Akashindilia zaidi kwa kuwaambia, ukiwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Usalama wa Taifa, Polisi, na Magereza vyote vinakuwa chini ya Wizara yako. Na hakuna mtu anaweza kuja na ndege akachukua wanyama wakubwa na akaondoka bila kubugudhiwa kama Usalama wa Taifa hawahusiki. Kwa hiyo Kagasheki asiwazuge, akija mmulize Twiga wetu wanarudishwa lini?
Siku chache Kagasheki akatua BK na akafanya mkutano wa hadhara. Wakati mkutano ukiendelea, Vijana wakaanza kiutani kumnyooshea vidole viwili.
Taratibu miguno ikaanza kusikika huku ikisindikizwa na maneno Tunataka Twiga wetu Ghafla Kagasheki akahamaki na kukosa uvumilivu, akaanza kurusha maneno hovyo. Ikawa ndo kama kawapa watu ruhusa kupiga chorus kwa sauti za Tunataka Twiga wetu na Twiga wetu wanarudi lini Mzee wa watu akaendelea kurusha meneno hovyo Najua hao ni CHADEMA mara hao CDM watachukua majimbo mengine huko kote lakini nawahakikishia hili hawatalipata Kutokana na mvulugano huu, kwa wale wanaomfahamu Kagasheki akiisha panic hawezi kulejea haraka katika control. Ikabidi mkutano uishe
Baada ya kurejea Jijini, haraka sana Kagasheki akatangaza hatua zinazochukuliwa kuwarejesha Wanyama wetu walioibiwa
Haya ndo nimewakusanyia kwa leo toka vijiwe nilivyotembelea hapa BK Mjini.