M23 Again!

M23 Again!

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
496
Reaction score
768
Bukumbirwa, Rusamambu, Kilambo et Ngengere (Walikale, Ikobo) chini ya AFC/M23 tena. Ni baada ya mapigano makali baina ya M23 na jeshi la serikali ya DRC na washilika wake huko Kivu Kasikazini.
 
Malizaneni muwape nchi wanyarwanda hiyo wawatawale maana hamna akili.bure kabisa wacongo nyinyi
 
Bukumbirwa, Rusamambu, Kilambo et Ngengere (Walikale, Ikobo) chini ya AFC/M23 tena. Ni baada ya mapigano makali baina ya M23 na jeshi la serikali ya DRC na washilika wake huko Kivu Kasikazini.
Kama wana nia njema acha tu washinde
 
Duh kama wamekaa hapo Walikale uelekeo usije ukawa Kisangani.
Hahahahaha, kama ulikuwepo. Baada ya hapo, mji unaoeleweka ni huo huo. Na si kwamba wakimaliza, washikaji ngoma wanaielewa, hakika mpaka sasa badhi walishatangulia.
 
Mpaka Trump atoe neno! Hahaha
Siyo rahisi kihivo. Ujue mchina na Mrusi na wenyewe wapo. Anachokitaka Trump, Xi na Putin na wenyewe hicho hicho wanakitaka. Na nchi nyingine kina Qatar ujue hawajabaki. Mu Israel unadhani siraha zake anatengenezea vitu kutoka wapi?
Kumbuka, rais mstaafu baada ya kuvuliwa mamlaka na ulizi wa kishelia, sasa hivi ni kama raia wengine, tena anaetafutwa sasa. Na yeye huko kwenye ngazi za uongozi, ana watu wake, na hawapo tayari kumsaliti. kwa kifupi, ni vurugu mechi
 
Mkuu vip hizi habari za kusema kuwa for now wale wote waliokuwa karibu na kabila hasa viongozi wanatekwa, kuondolewa kinga kama wanazo hasa swahil and kirwanda speakers wanafungwa, na kuuawa na next stop itakuwa kwa Moise Katumbi, hii imekaaje?
 
Japo umechanganya, ila kuna kaukweli ndani yake.

Kumbuka, siku zote rais Felix, amekuwa akiwatuhumu wanajeshi wakuu, waliofanya kazi na Kabila, usaliti unaopelekea maelfu ya wanajeshi kupoteza, maisha, na wao kukimbia vita. Mpaka sasa, inasemekana majenerali 24 wapo rumande.

Siku zote ukiachana na DRC tu! nchi yoyote ukibainika we ni msaliti, au kuna chembe za usaliti, mchezo wa kukuchunguza, huo haupo.

Mawaziri wengi wamekuwa wala rushwa,jambo ambalo limewaudhi raia,baada ya madudu yao kuanikwa. Hayo yanaanikwa kutoka kule juu kabisa. Kwa maana kuna watu wapo kwa ajili ya kuivuruga serikali.

M23, ina kila aina ya siri ya ndani ya serikali. Wanaoongea Kinyarwanda na kiswahili, si kweli. Mfano hai ni General Masunzu. Ni mnyamulenge pure, ila yupo upande wa serikali. Na mpaka sasa, wanyamlenge walishagawanyika makundi mawili. Iwe walipo nchini kwao, kambini Burundi na Rwanda, au waishie nchi za ulaya na marekani.
 
Back
Top Bottom