kudra hamidu
Senior Member
- Jul 1, 2012
- 152
- 107
MWENYEKITI wa Chama cha wenye Kisukari Tanzania, Profesa Andrew Swai ametamani sukari iendelee kuadimika na bei yake kuwa juu ili matumizi yake yapungue kwa jamii kutoka na madhara ya bidhaa hiyo kwa mwili wa binadamu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa semina kwa waandishi wa habari iliyolenga kuelimisha juu ya magonjwa yasiyoambukizwa, Profesa Swai ambaye ni daktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alisema matumizi ya sukari ni moja ya kichocheo cha magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu.
“Kwa upande wa sekta ya afya, tunaona ni vizuri sukari kuadimika, na ndio maana nchi kama Uingereza inapandisha bei ya sukari kuanzia mwakani ili kudhibiti matumizi makubwa ya sukari. Hivyo kuongeza bei ni njia mojawapo ya kuzuia watu wasitumie,” alisema.
Hata hivyo, alisema anatambua kuadimika kwa sukari nchini hakutokani na sababu za kiafya, lakini ni vyema serikali kuiga hatua kama ya Uingereza na nchi zilizoendelea za kupandisha bei vitu vinavyochangia magonjwa yasiyoambukiza kama sukari, tumbaku na vileo.
“Ningependa liwepo ongezeko la bei kwa bidhaa kama sigara na vinywaji vilivyoongezewa sukari, ili kupunguza matumizi yake kwa jamii,” alisema. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na moyo na shinikizo la damu, figo, saratani, kifua sugu, kisukari, magonjwa ya akili na mengine ya kurithi kama vile selimundu.
Chanzo: Habari leo