Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,733
- 239,339
Huu ndio ukweli ambao hata Lumumba inaujua.
Haifahamiki kwanini mpaka leo CCM imeshindwa kupata mtu sahihi wa kufit kwenye wizara hii, kila aliyefuata baada ya Mrema alipwaya vibaya sana kiasi cha kushindwa kabisa kuondoa changamoto zinazolikabili jeshi la polisi.
Wako walioshindwa kabisa hata kukemea maovu, ikiwemo ujambazi pamoja na ile biashara kubwa kwa sasa nchini ya madawa ya kulevya, hadi kufikia waziri wa uchukuzi kuingilia kati na kujitutumua japo haifahamiki zilikoishia juhudi zake.
Wengine waling'olewa na bunge baada ya kunyamazia ama kushiriki kwenye operesheni tokomeza, operesheni ambayo dunia iliitafsiri kama UHALIFU MKUBWA DHIDI YA BINADAMU .
Ukiacha usaliti wake kwa wananchi bado Lyatonga Mrema hajapata mbadala wake wizara ya mambo ya ndani, sikumbuki kama aliwahi kufanya biashara yoyote na jeshi la polisi.
Pongezi kwake.