Lundenga na Mzee Yusuf wagombea uongozi yanga

MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,166
166
Nikiwa nimeipata habari hii kutoka katika gazeti moja la kila siku "Mwananchi" Leo siku ya mwisho ya kuchukua fomu za kuwania uongozi katika klabu ya soka ya YANGA, watu maarufu nchini katika fani mbalimbali wamejitokeza kuwania nafasi hizo.

Huku katika vilabu vingine watu maarufu katika soka wakikimbizana hadi mahakamani, yanga wameibuka na yao kwa Gwiji la mziki wa mwambao kugombea nafasi ya ujumbe, wakati kiongozi wa mambo ya Ulimbwende nchini "Lundenga" akiwa ametangaza siku za karibuni kugombea nafasi ya juu tu- makamu Mwenyekiti"

Sasa wana JF huku yanga si tutaanza kuwachagua wachezaji kwa kufuata Urembo kweli!,
au tutakuwa tunashangilia kitaarabu taarabu! na Yusufu mwenyewe anasema anataka kutoa mchango wake. Ivi ataacha kuingizia kidogo verse jinsi ilivyomuingia damuni?!!

Hebu nambieni japo kuna uhuru wa kugombea nafasi, na mambo mengine, kuna weredi kweli? wajumbe na viongozi wengine hawapo? au kuboronga kumezidi hivyo kila mtu anataka alete mabadiliko? au uongozi umekuwa kitu rahisi kwa kila mtu? au ni maslahi yanatufanya tugombee hata kama hatuna mawazo ya kuchangia katika sekta hiyo.
 
Si kuna chujio la kufanaya kazi yake, Sidhani kama wanasifa yoyote ya uongozi kwenye michezo zaidi ya kwenye burudani tu.Akipata ujumbe huyo Mzee yusuph lazima yanga wataramba tu.aaraamba tena ham ham!!!
Ila ni haki yao ya kikatiba kugombea kama ni wanachama halali wa YANGA
 
Back
Top Bottom