Lunch Matata na MTU wangu wa Nguvuu.

Lunch Matata na MTU wangu wa Nguvuu.

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230

Si chaupele bali ni kipele kinahitaji kuminywa maana kimeiva, ila si chunusi ni kipele tuu.

Iko hivi..... nimefika kwenye mgahawa flani kupata mlo wa mchana, nilikuwa na miadi na mtu flani hivi ila dakika 3 baada ya muda wa miadi kufika alinipigia kuniambia amepata dharura na hatoweza kufika hapo. Kwakuwa nilikuwa nna njaa nikaagiza chakula kisha niendelee na michakato mingine.

Wakati nasubiria chakula changu akaingia huyu MTU yaani nikaanza kutokwa majasho mikononi kwenye viganja, kwenye nyayo, kwenye paji la uso na hata makwapani na mgongoni kile kijasho chembambaa daaah fedheha hii...... hehehehehehee usiombe kushikwa na kihoro.

Nikajikuta macho hayabanduki kumuangalia tangu anaingia maana nilikaa kwenye kona mwisho wa mgahawa. Yule MTU akakaa meza za katikati mwa mgahawa huku akitoa kilongalonga chake na kuanza kuongea. Nilijikuta masikio yangu hayasikii kitu kingine zaidi ya sauti yake bila kupata matamshi anayotamka na nikawa nameza funda la mate kushushia shughuli yote hiyo ya kumkazia macho kwa umakini.

Kumbe muda wote huo namtizama nilikjwa natabasamu bila mie kujijua. .. alipomaliza kuongea na simu akahisi kuna macho yanamtizama sana, akanitizama kisha akawa kama anasema.... you smile at me... do I know you..... mie tabasamu liko palepale hahahahhaha daaah....

MTU wa watu akanyanyuka na kuja kanisalimia, habari yako bibie naweza kaa hapa au kuna mtu unamtarajia? Hehe ngekewa hiii, nikashtuka aah eeh kama sekunde mbili hivi ndo akili zikanirudia kidogo nimuamkie. ... aahahahahahahahaa leo nimeaibika sio siri maana MTU yule aliona wazi alivonichanganya na jinsi nilivohorojeka kwake.

Basi nikamjibu hapana karibu ukae, niliekuwa na miadi nae amepata dharura, akanijibu ooh what a coincidence nami nilikuwa na miadi na mtu ila nafika hapa nampigia nae kaniambia amepata dharura. Tukajikuta wote tunacheka. .........

Naye akaagizia chakula tukala na maongezi yalikuwa habari haja mchanganyiko maana hatukuwa tunafahamiana kabla. Tulijikuta tumekaa pale mgahawani toka saa saba mchana hadi saa 9 bila kujua kama muda umeenda. Basi saa ya kuagana akanipa business card nikasema moyoni wallah hii nikikaa nayo ni msala kwangu, akanishukuru kwa kukaa nae na kupata mlo pamoja huku akiahidi iko siku ingine tutatoka wote tena this time kucheza mziki. Hahahahahah

Huo wimbo hapo juu nimeambatanisha na hii habari sababu huyo MTU anafanana sana na huyo kaka anayeimba huo wimbo wa Chaupele.

Nimewashirikisha kilichotokea leo mchana na msema ukweli mpenzi wa Mungu. .... we just shake hands nothing more ila.... naisubiri kwa hamu siku tutayoenda kucheza mziki aahahahahahahhaaa aliniambia tutashindana kucheza bumping looh.

Poleni kwa maelezo marefu, ambao mtatoka kapa muulize notsi kwa wenzenu. Wacha nijikoki nielekee maeneo nyanda za juu.

Badala ya kutaja jina lake huyu MTU nimemuandika kama MTU maana nikitaja jina lake tuu mtamjua.
Hivi kumbe unaweza kuwa unatabasamu halafu hata hujijui kuwa umetabasamu eeeh.... basi imenitokea leo. Alamsiki.

Kasie Matata.
 
Kama si msuba basi moshi wa msuba umechangia sehemu ya hii sredi...
 
Bado unadanga tu mwaka unaisha sasa

nadhani mpaka january utakuwa unatokwa na maji kama una fistula

shauri yako wee toa tu hiyo miutamu mwisho utajikuta imebakia kokwa.
 
Kama si msuba basi moshi wa msuba umechangia sehemu ya hii sredi...

Hahahahaaa halafu nakudai msuba wangu ujue.... ngoja nimalize kulipuliza nikuibukie hukohuko.... heheheee ukiletewa kipakti cha matunda mezani ujue Kasie huyo..... muuza matunda bado yupo pale lango la kanisa.
 
hongera sana kwa kupata mtu wa kukununulia msosi mchana huu.mimi leo sijala

Umenukuu vibay Miss...... sikununuliwa chakula niliagiza chakula changu na yule MTU nae aliagiza chake na kila mmoja alilipa bili yake.

Polee ungepika walau uji ukanywa kuliko kukaa njaa au hata kula tunda la msimu. Vidonda tumbo ni hatari sana.
 
Bado unadanga tu mwaka unaisha sasa

nadhani mpaka january utakuwa unatokwa na maji kama una fistula

shauri yako wee toa tu hiyo miutamu mwisho utajikuta imebakia kokwa.

Maneno ya mkosaji hayamnyimi mpataji cheuo teh teh teh.

Kasie Matata.
 
Kuna sredi nikipitaga nikatoa my honest opinion basi wadada wanamaindigiii basi napita kimya kimya.😀😀

Na wewe unawaogopa wadada wa JF.... poleee mwaya. Mie hata sifikiriagi mara 2 nani ataudhika nani atafurahi nabandika tuu pwaaaah. Atayekunwa haya anatabasamu huku anasinzia, atayekerekwa wengine wanapita kimya, wengine wanakejeli, wengine wanatukana, wengine wanakuja na ID spea na kung'aka (hawa ndo hawajiamini kabisaa) halafu mie nawajuaga sanaa ila nawapotezea tuu.

Kasie Matata.
 
Kuna viti JF?

Hahahahaaa naonaga siku hizi watu wanawaigi kujibu sredi awe wa kwanza baada ya mtoa mada. Nafasi hiyo aliishikilia Joseverest kwa muda tuu...

It's more of a joke...

Usijikaushe na msuba wangu.... hehehee
 
Yeap, what's up. ....

You good?
Yeah, I'm good.

Just missed this kind of stuff!
Cause only Kasie can make it feel better. Sema upunguze kuhunt!
[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Na wewe unawaogopa wadada wa JF.... poleee mwaya. Mie hata sifikiriagi mara 2 nani ataudhika nani atafurahi nabandika tuu pwaaaah. Atayekunwa haya anatabasamu huku anasinzia, atayekerekwa wengine wanapita kimya, wengine wanakejeli, wengine wanatukana, wengine wanakuja na ID spea na kung'aka (hawa ndo hawajiamini kabisaa) halafu mie nawajuaga sanaa ila nawapotezea tuu.

Kasie Matata.
Basi sawa, but at the end of the day, what really is your point?
 
Yeah, I'm good.

Just missed this kind of stuff!
Cause only Kasie can make it feel better. Sema upunguze kuhunt!
[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]

Great that you are good.
Enjoy the missed stuff... plenty of them from Kasie.

Heey... how could I reduce hunting. ..?
 
Basi sawa, but at the end of the day, what really is your point?

Hahahahaaa see, I knew it some will miss the points .... here you are. It's up there...

I said I just shared here what happens today.... nothing more than sharing....

May be you know not Kasie .... she has been like that since then and that's the way she is all - ways.

Kasie Matata aka Kasinde.
 
Back
Top Bottom