Lukuvi,liezer et al papara zenu zinaleta maafa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi,liezer et al papara zenu zinaleta maafa.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by kipindupindu, Mar 23, 2011.

 1. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa na jinsi watu wenye nyadhifa zao mbalimbali serikalini na taasisi za dini walivyochukulia suala la babu wa loliondo.kuna waliokurupuka mfano waziri lukuvii hasa baada ya kupinga tamko la waziri wa afya la kusitisha tiba hii feki!mwingine ni askofu Tomas laiza ambaye amewaaminisha waumini wake kuwa yeye mwenyewe amepona kitu ambacho hata yeye anajua si kweli.
  mzee ndesamburo amenisikitisha mno kwa kunasa katika mtego huu wa panya mpaka akatoa helikopta kupeleka watu loliondo.
  Viongozi wastaafu kama kina mahita na sumaye mmetia aibu taifa.
  Naamini Lukuvi na laiza kwa sasa watakuwa katika majuto makubwa kutokana na vifo vinavyoendelea kutokea huko loliondo (ushuhuda upo) vifo hivi vingezuilika mapema kama hawa watu wawili wangekaa kimya na kuacha ushawishi wa kinafiki.
  Leo hii wagonjwa wanatoka hospitali wanaenda kusongamana na hatimaye kufa kwenye foleni,wengine wanarudi na kuacha ARV na insulin hatimaye wanapoteza maisha!!
  Kwa taarifa yenu kuna watu tunakusanya data za vifo vinavyohusiana na habari hii ya babu na mambo yakikamilika tutamwaga hapa jamvini.

  Mungu uwalaani wote wanaohusika na utapeli huu wa babu,usiwauwe bali wateseke mbele ya macho ya watanzania.AMINA
   
Loading...