Lukuvi: Hatuna takwimu za vifo kwa `Babu` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi: Hatuna takwimu za vifo kwa `Babu`

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Mwasapile


  Serikali imesema haina takwimu sahihi za vifo vya wagonjwa waliopoteza maisha kutokana na kukatisha dawa za kurefusha maisha baada ya kunywa kikombe cha Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Mwasapile, na haijui alipo kwa sasa.
  Mchungaji huyo kuanzia mwishoni mwa mwaka juzi na mwanzoni mwa mwaka jana alikuwa akitoa dawa ya miti shamba ambayo alidai inaponya magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, jana alisema serikali haina taarifa za mchungaji huyo wala haijui takwimu sahihi za vifo vya wagonjwa walioacha dawa ya kurefusha maisha ARVs baada ya kupata kikombe.
  Lukuvi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua warsha ya viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu mbinu za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.
  “Ni kweli serikali ilikuwa inajua taarifa za mchungaji huyo, lakini kwa sasa haijui yupo wapi na anafanya nini labda waulizwe viongozi wake wa dini,” alisema.
  Lukuvi alisema watu walioacha dawa ya kurefusha maisha baada ya kunywa kikombe walifanya makosa makubwa na kukiri kuwa wengi wao wameshapoteza maisha.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naomba msome hizo sentence mbili toka kwa Lukuvu na hasa kwenye red.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, jana alisema serikali haina taarifa za mchungaji huyo wala
  haijui takwimu sahihi za vifo vya wagonjwa walioacha dawa ya kurefusha maisha ARVs baada ya kupata kikombe.

  Lukuvi alisema watu walioacha dawa ya kurefusha maisha baada ya kunywa kikombe walifanya makosa makubwa na kukiri kuwa
  wengi wao wameshapoteza maisha.
   
 3. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lukuvi yupo sahihi, kwanza ile ilikuwa "mission" na imeshakamilika, sasa matakwimu ya nini, after all serikali haina utaratibu wa kuwa na takwimu...
   
Loading...