Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Waziri ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi amezitaka halmashauri kutimiza majukumu yake kwa kuwasilisha kwake orodha ya mashamba pori ambayo hayajaendelezwa ili hatua za kufuta vibali vya umiliki wake zifanyike na siyo kubaki kulalamika kuwa kuna mashamba makubwa ambayo hajaendelezwa na hivyo kuwanyia haki wakulima na wafugaji kufanya shughuli zao.
Lukuvi ameyasema hayo alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii alipokutana na uongozi wa mradi wa urasilimishaji ardhi
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Atashasta Nditiye amesema uwepo wa mradi huo utasaidia kuondoa migogoro ya ardhi hivyo ni vyema utekelezaji wake ukafanyika kwa umakini.
Naye Mratibu wa Mradi huo Bw Godfrey Machabe amesema mradi huo umeanza japo unakutana na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi lakini wanafanya kila liwezekanalo kuhakisha kuwa wanafikia lengo lilokusudiwa.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipata nafasi ya kuhoji mambo mbalimbali kuhusu mradi na kupatiwa majibu na viongozi.