GE2025 Luhende: Nitahakikisha wanafunzi hawakai chini Bukene

GE2025 Luhende: Nitahakikisha wanafunzi hawakai chini Bukene

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukene kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM )John Luhende, ameendelea na kampeni za kunadi sera kwenye jimbo hilo, akisema endapo atachaguliwa atatatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, ikiwemo uhaba wa madawati mashuleni kwa kutumia rasilimali misitu inayopatikana katika Mkoa wa Tabora

Luhende ameyabainisha hayo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Itobo iliyopo Jimbo la Bukene, Wilayani Nzega Mkoani Tabora, akisema kuwa kutokana na uwepo wa Misitu Tabora atatumia fursa hiyo kuvuna magogo kwa mujibu wa sheria na kutengeneza madawati kwaajili ya wanafunzi.

Soma pia: John Luhende ashinda kura za maoni ubunge wa Jimbo la Bukene



"Na sisi hatuwezi kuwa tunahangaika madawati lakini jimbo letu la Bukene lina mapori ndani yake, nikiwa kiongozi naenda kuhakikisha hakuna Mwanafunzi anakaa chini ndani ya jimbo hili la Bukene" Luhende alisema .

Aidha, katika sekta ya nishati ya umeme, amesema kuwa licha ya serikali kusambaza umeme kwenye maeneo mengi Jimboni humo, kuna baadhi ya maeneo bado hajafikiwa na huduma hiyo hivyo atahakikisha anafikisha umeme ili wananchi waweze kunufaika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi .
 
Ila bongo hapana kwa kweli. Miaka 60+ ya uhuru bado ahadi za kampeni ni madawati ya wanafunzi
 
Bukene town ni miji ambayo uko tokea enzi za wakoloni wa kijerumani
 
Yaani CHADEMA imeshika dola miaka 60 wanafunzi bado wanakaa chini??

CHADEMA ndio imeuza hadi mbuga zetu za wanyama kwa waarabu wakaweke vitalu vya uwindaji , imeuza mapori tengefu tena kwa bei ya kutupa.

Twende tukapige kura kwenye huu uchaguzi wenye ushindani kupata kutokea tangu tupate uhuru tukaiondoe CHADEMA madarakani.
20251023_033515.jpg
 
Back
Top Bottom