Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,312
- 152,112
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lugumi Enterprises, Said Lugumi jana alijitokeza kwa mara ya kwanza na kusema mtu yeyote anayetaka ufafanuzi wa mkataba wa kampuni yake kufunga mashine za utambuzi wa alama za vidole ataupata katika Jeshi la Polisi.
Akizungumza kwa simu jana saa 7.22, Lugumi alisema kwa vile vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari za upande mmoja kuhusu sakata la mkataba huo, hawezi kuuzungumzia habari alizodai zimemchafua yeye binafsi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga na Jeshi la Polisi.
“Kwa taarifa yako habari zako zimekuwa zikiichafua Serikali, zimemchafua waziri na Jeshi la Polisi; kama ulidhani unanichafua mimi basi umeichafua Serikali yako na Jeshi la Polisi,” alisema. Alipoombwa atoe ufafanuzi baada ya fursa hiyo kupatikana alijibu: “Nenda Jeshi la Polisi.”
Aidha, mkurugenzi huyo alisema anakusudia kufungua mashtaka kwa kile alichodai kutaka kujua nani alikuwa akitoa habari zilizokuwa zikiandikwa.
“Brother, nitakufungulia mashtaka. Haiwezekani siku zote wewe uwe unaniandika bila kunihoji halafu leo unataka uzungumze na mimi. Nitakushtaki ili unieleze ulikuwa unapata wapi habari zangu. Mkiniambia mlikuwa mnapata wapi habari zangu basi,” alisema Lugumi.
Alipoulizwa mashtaka hayo yatakuhusu kosa gani Lugumi alijibu; “Nataka mnieleze mlikuwa mnapata wapi habari zangu. Kama ni Kamati ya Bunge au wapi mtanieleza.”
Kamati ya Bunge ya PAC ndiyo iliyoibua sakata la kampuni hiyo kushindwa kufunga mashine za utambuzi wa alama za vidole (AFIS) kwenye vituo vya polisi ilipokutana katika vikao vya Aprili mwaka huu. Kamati hiyo, ikinukuu ripoti ya CAG ya mwaka 2014/2015 ikisema kampuni hiyo iliyoingia mkataba na Polisi mwaka 2011 kufunga mashine hizo haikuwa imekamilisha kazi hiyo. Pamoja na kutokamilisha ufungaji mashine hizo, PAC ilisema kampuni ilishalipwa Sh34 bilioni sawa na zaidi ya asilimia 90 ya jumla ya malipo ya Sh37 bilioni za mkataba, jambo ambalo wabunge wanaona ni viashiria vya ufisadi katika Jeshi la Polisi.
Juhudi za vyombo vya habari zilimwibua Lugumi ambaye alitoa taarifa kwamba angekutana na vyombo vya habari Aprili 20, lakini hakuonekana badala yake alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba ni uzushi.
“…Mambo yaliyo mengi yaliyotajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa Taifa. Ni katika muktadha huo huo, tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwamo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika. Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, mkurugenzi wetu yupo nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida,” ilisema taarifa hiyo.
Mwananchi lilimpigia simu jana saa 5.36 ili lifanye mahojiano naye lakini ilipokewa na katibu muhtasi ambaye alisema mzee ana kikao na aliahidi kuwasilisha ujumbe huo. Saa 7.22 Lugumi alipiga simu mwenyewe na kutoa maelezo hayo.
Chanzo: Mwananchi