Lugha za kibaguzi, Uvaaji wa Sare za Vyama kwenye shughuli za kitaifa, Vipigwe Marufuku

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,856
CCM kuomba radhi,pamoja na watu mbalimbali kuendelea kukemea kitendo kilichotokea Zanzibar leo hii kwenye sherehe za Mapinduzi,nafikiri haya yote hayatoshi na wala hayatasaidi kitu na kwahivyo tunapaswa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na matukio ya aina hii katika siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu,wakati umefika tuwe na sheria,tena sheria kali, itakayozuia watu kuvaa sare za vyama vya siasa katika shughuli au matukio ya kitaifa.

Vile vile tunapaswa kuwa na sheria itakayokataza au itakayopiga marufuku kauli,vitendo na aina yoyote ya matukio ya kibaguzi au yenye mwelekeo wowote ule wa kibaguzi. Ubaguzi huu uwe wa rangi,dini au kabila.

Hili ni wazo tu ila naamini kuna wataalamu wa sheria wanaoweza kulifanyika kazi wazo hili na kuliboresha zaidi.

Wabunge mnao uwezo pia wa kupeleka hoja binafsi Bungeni kuhusu swala hili na si kuisubiri serikali tu ambayo nayo inaweza isilifanyie kazi wazo hili au ikachukua muda mrefu kulitekeleza.

Tujifunze kutokana na makosa na tuchukue tahadhari pia.
 
Last edited:
Ni kweli sherehe za kitaifa watu wanavaa nguo za chama ! Wageni waokwenda kwenyevshughuli hizo wanatuona wa ajabuvsana na wanatuona hatuna elimu .hawa watu watavaa sare hata bungeni
 
CCM kuomba radhi,pamoja na watu mbalimbali kuendelea kukemea kitendo kilichotokea Zanzibar leo hii kwenye sherehe za Mapinduzi,nafikiri haya yote hayatoshi na wala hayatasaidi kitu na kwahivyo tunapaswa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na matukio ya aina hii katika siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu,wakati umefika tuwe na sheria,tena sheria kali, itakayozuia watu kuvaa sare za vyama vya siasa katika shughuli au matukio ya kitaifa.

Vile vile tunapaswa kuwa na sheria itakayokataza au itakyopiga marufuku kauli,vitendo na aina yoyote ya matukio ya kibaguzi au yenye mwelekeo wowote wa kibaguzi. Ubaguzi huu uwe wa rangi,dini au wa kikabila.

Hili ni wazo tu ila naamini kuna wataalamu wa sheria wanaoweza kulifanyika kazi wazo hili na kuliboresha zaidi.

Wabunge mnao uwezo pia wa kupeleka hoja binafsi Bungeni kuhusu swala hili na si kuisubiri serikali tu ambayo nayo inaweza isilifanyie kazi wazo hili au ikachukua muda mrefu kulitekeleza.

Tujifunze kutokana na makosa na tuchukue tahadhari pia.
Umeongea ukweli mtupu. Bahati mbaya CCM inabidi itume ujumbe kwa CUF,Siasa za Zanzibar ni nzito kidogo.
 
sahihi..,,..inabidi tufike maala tubadilike kifikra..,,,,...kila mwananchi akisema avae sare yake c patakuwa hapatoshi .,,,...ila ccm sijua huwa wanawaza nini..,.i hate this chama
 
mimi ubaguzi siachi waindi wachina wazungu na warabu nitawabagua tu haijarishi kazaliwa wapi sababu wote ccm
 
chagadema mmepata hoja ya kuanzisha thread hata aibu hamna...

hapa kazi tu.
 
Angalia hata katika ziara za kiserikali,iwe ni kwa Mkuu wa Nchi au Mawaziri utawaona CCM wapo na sare zao kana kwamba ni shughuli za kichama!
Tanzania tunaonekana wajinga kwa kila kitu.
 
CCM kuomba radhi,pamoja na watu mbalimbali kuendelea kukemea kitendo kilichotokea Zanzibar leo hii kwenye sherehe za Mapinduzi,nafikiri haya yote hayatoshi na wala hayatasaidi kitu na kwahivyo tunapaswa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na matukio ya aina hii katika siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu,wakati umefika tuwe na sheria,tena sheria kali, itakayozuia watu kuvaa sare za vyama vya siasa katika shughuli au matukio ya kitaifa.

Vile vile tunapaswa kuwa na sheria itakayokataza au itakayopiga marufuku kauli,vitendo na aina yoyote ya matukio ya kibaguzi au yenye mwelekeo wowote ule wa kibaguzi. Ubaguzi huu uwe wa rangi,dini au kabila.

Hili ni wazo tu ila naamini kuna wataalamu wa sheria wanaoweza kulifanyika kazi wazo hili na kuliboresha zaidi.

Wabunge mnao uwezo pia wa kupeleka hoja binafsi Bungeni kuhusu swala hili na si kuisubiri serikali tu ambayo nayo inaweza isilifanyie kazi wazo hili au ikachukua muda mrefu kulitekeleza.

Tujifunze kutokana na makosa na tuchukue tahadhari pia.
point. naunga mkono na mguu hii hoja. tusigawanywe kwa sababu za kipuuzi tu.
 
Ninakubaliana na hoja lakini ningpenda kuiboresha zaidi ya hapo. Wakati umefika wa kuondokana na utamaduni wa bendera na sare za vyama vya siasa. Ili linawezekana- mataifa yaliyokomaa kidemokrasia kama US waliishaachana na sare za vyama. Katika shughuli zo zote za kisiasa - iwe ni kampeni za urais au ubunge majukwaa na washabiki huvaa mavazi yaliyochanganya rangi za bendera ya taifa, na ni bendera ya taifa mabayo hupamba kila tukio la kisiasa. Kwa hivyo tupendekeze sheria itakayopiga marufuku sare na bendera za vyama.
 
Asante kwa mawazo mazuri sana haya.Binafsi nakuunga mkono kwa asilimia mia mbili.
 
CCM huwa wanatoa hela sana,hasa kipindi wanapokuwa wanatafta uongozi,kwahiyo wananchi waliowengi wanasare za ccm hata kama sio mshabiki au mwanachama kwalengo la kupata hela, chumvi,sabuni n.k Viongozi huvaa hizo sare ilikuwaaminisha wananchi hasa wasiokuwa na uelewa mzuri wa maswala kuamini kuwa kila kitu kilichondani ya hii nchi kipo chini ya CCM.
 
Niliandika humu na nina rudia tena, tunaposema mambo ya kitaifa au nchi (mfano sherehe za uhuru, mapinduzi, muungano nk) wana ccm hudhani kwamba nchi/taifa ndio ccm na ccm ndio nchi/taifa; hadi mawazo hayo ya kipumbavu yatakapotoka vichwani mwao ndipo wazo lako hilo litakapotekelezwa, vinginevyo sio rahisi.
 
Kwa chama ambacho watukanaji watu ndio wapewa vyeo unategemea nini sasa fisiem kimekuwa chama cha kinafiki sana Leo adifa anatafuta cheo kutaka familia ya mwasisi na rais mstaafu afukuzwe fisiem kuvaa sare hizo sare zimegaiwa bure kwa hiyo viongozi wakuu wanajua kila kitu na kwa akili zao wanafurahia
 
Back
Top Bottom