Lugalo sasa ni Hospitali ya Rufaa!

Labda upeo wangu unaweza kuwa mdogo,lakini nikiwa nimezaliwa na kuwa kwenye maeneo ya kijeshi ninavyojua ni kwamba hizo hospital zimejengwa kwenye kambi za jeshi ili kuhudumia wanajeshi na familia zao kwasababu zipo ndani ya vikosi vya jeshi ambapo kuna siri kubwa kwa raia wa kawaida haruhusiwi kuingia anavyotaka,Sasa kuiweka hiyo hospitali ya lugalo kuwa ya Rufaa inamaanisha nini kuwa Raia wote dwataruhusiwa kwenda hapo je siri na unyeti wa jeshi upo wapi?au hiyo Rufaa ni kwa jeshi tu?tunaangamiza ulinzi na usalama wa nchi hiyo ni taasii nyeti sana ila siasa zitatumaliza,hiyo sio njia ya kutatua tatizo!!!

Nakubaliana na wewe isipokuwa kitu kimoja tu; Hospitali za jeshi zinahudumia wanajeshi, familia zaio, viongozi wa serikali na Raia wanazunguka jeshi maeneo hayo. Binafsi nimetibiwa sana hospitali ya Lugalo nikitokea Kawe!
 
Hayo ni mawazo yako au kuna mahali unayasoma?...hii ni nchi huru na tawala zake ni za kidemokrasia na si kijeshi.

sawa mkuu - collaterally maana yangu ni serikali ianze kuwekeza kwa makusudi na kwa nguvu zote katika hospitali za jeshi (JWTZ na Polisi) na wanaotaka migomo bado watakuwa na nafasi ya kupata kazi hospitali binafsi na zile za nje ya nchi ambako kunalipa na wana nafasi kubwa ya ku compete na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
hahahahhaha viongozi wa bongo........ hapo ndo uwezo wao wa kufikiri ulipoishia?

breaking news;

lugalo yawa hospitali ya rufaa.

Sasa kupokea wagonjwa toka sehemu zote hapa nchini.

Mungu ibariki lugalo
mungu ibariki tanzania..
 
Khaaaaaaaa Lugalo Ile wanayotibu clinical officers iwe rufaa? tell me its a joke! Unajua nchi hii kuna utani sana, kimsingi Hospitali ambazo kidogo unaweza kusema ni za rufaa ni Muhimbili, KCMC na BUGANDO tu
 
Safi sana, maanake MNH inashuka kiwango na madaktari wake wameshaingia katika politike na kuacha science mkiwaachia peke yao wataendelea kuua watu mapema. Wao wakipasua mtu kichwa badala ya goti ni bahati mbaya! Wajeda hawanaga makuzi ni kuwajengea uwezo tu.
 
Those are traditionals rufaa, mambo yanakwenda mbele sasa we need more on-board

Khaaaaaaaa Lugalo Ile wanayotibu clinical officers iwe rufaa? tell me its a joke! Unajua nchi hii kuna utani sana, kimsingi Hospitali ambazo kidogo unaweza kusema ni za rufaa ni Muhimbili, KCMC na BUGANDO tu
 
ndani ya ccm hilo mbona linawezekana. wakuu mmesahau dhaifu aliposema kuwa hospitali zote za mikoa zitakuwa za rufaa, sasa mnashangaa hili. serikali ya ccm ni sikivu.:yawn:
 
mbona kawaida tuu,huko muhimbili kwenyewe hakuna Tscan lakini ni hospital ya rufaa.
 
Hoja yako ingekua serikali kwa ushirikiano na JWTZ wawekeze zaidi ktk hospitali za Jeshi kwa vifaa na wataalamu ili watawala watibiwe hapa nchini badala ya kutumia pesa nyingi kuwapeleka nje ningekuelewa. Lakini eti kama mkakati wa kupambana na wafanyakazi wa sekta ya afya ambao wanadai mazingira bora ya kufanyia kazi,vifaa na maslahi stahiki inaonyesha umasiking wa akili ulionao kichwani kwako!
sawa mkuu - collaterally maana yangu ni serikali ianze kuwekeza kwa makusudi na kwa nguvu zote katika hospitali za jeshi (JWTZ na Polisi) na wanaotaka migomo bado watakuwa na nafasi ya kupata kazi hospitali binafsi na zile za nje ya nchi ambako kunalipa na wana nafasi kubwa ya ku compete na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Hii itairahisishia serikali kazi ya "kuwashughulikia" wale wanaowapinga wanapokuja kuomba huduma, na sio mpaka wapelekwe Msitu Mabwepande. On a serious note: situmesikia mgomo umeisha? Na je wale madaktari 3000 wanaotoka nje hawajafika bado?
hivi hao madaktari wanao toka nje ndo wale wa Iran duh mbona kazi ipo
 
mbona kawaida tuu,huko muhimbili kwenyewe hakuna Tscan lakini ni hospital ya rufaa.
 
Hoja yako ingekua serikali kwa ushirikiano na JWTZ wawekeze zaidi ktk hospitali za Jeshi kwa vifaa na wataalamu ili watawala watibiwe hapa nchini badala ya kutumia pesa nyingi kuwapeleka nje ningekuelewa. Lakini eti kama mkakati wa kupambana na wafanyakazi wa sekta ya afya ambao wanadai mazingira bora ya kufanyia kazi,vifaa na maslahi stahiki inaonyesha umasiking wa akili ulionao kichwani kwako!

safari hii hakuna anewaunga tena mkono wauwaji hawa isipokuwa vichaa
 
Matumizi ya sasa ya hospitali Lugalo ni sawa tu na watu kutumia ile basi nadhifu la Scandinavia aina ya 'Andre Paradiso' kupakia mchanga kutwa kucha kule Mbweni.

Ukimya wa majeshi yetu na familia zao kubanana na wa-uraiani kwenye kutafuta tiba ilioelemewa zaidi ya mara 200 kidogo ... !!!!
 
Back
Top Bottom