Lowassa tunakutaka wewe, mbona uko kimya?

Lowassa tunakutaka wewe, mbona uko kimya?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Amekutaja na kukusema kimafumbo, Prof. Lipumba wa CUF, umekaa kimya. Hukutoka kujibu. Akakusema kimafumbo rafikiyo Rais Kikwete pale Viwanja vya Jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni zetu, ukanyamaza. Alikuita kuwa una makandokando.Amekutaja Dr. Slaa aliyekuwa CHADEMA na kukutupia makombora ya hasara lakini umekaa kimya.

Wanakusema na kukutajataja wanatimu wa kampeni za CCM kila uchao na kila wapitapo,uko kimya. Husemi kitu. Amekutuhumu na kukuripua Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ukakaa kimya.Badala yake wanajibu akina Lissu, Mbowe, Askofu Gwajima na kadhalika. Madongo yote unalengwa wewe Edward Ngoyai Lowassa.

Yapo yanayokupata na yanayokukosa. Lengo letu watoa madongo na washabikia madongo hayo ni wewe. Tunakutaka wewe ujibu hadharani ili tujibizane nawe na uache kampeni zako kwa muda. Mbona uko kimya? Unatupuuza,unatudharau au unatuvutia mafuta? Sema!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mzee Tupatupa umesahau Mbatia alisema Lowasa sio size yenu? mkitaka majibu nendeni kwa Mbatia.Ila kwa sasa tunawaachia Gwajima anawatosha. Zaidi ya hapo mtapoteana kwenye kampeni, ukizingatia kila bomu mnaloandaa linawalipukia wenyewe.
 
Kama like LA kusema lowasa kaomba kura kanisani kumbe ni pole pole katengeneza
 
  • Thanks
Reactions: C.K
hahahaaa mimba za kutotarajia nomaaaaa lowasa mwaka huu atapeleka wengi labour
 
Lowassa anahangaikia makulaji kwanza ama anaogopa atakapojibu nini kitamkuta ..anaogopa kuusikia mwangwi wa atakachokijibu make anajua itamchafua zaidi ya hapa
 
Lowasa anawapeleka puta mpaka chooni mnafuata leo katoa nini duuu Lowasa noma
 
hajaona hoja ya msingi ya kujibu bado,yule si muimba taarabu.
 
Hii style ya Lowasa nimeipenda hata humu JF ile mijingajinga kama kina ritz na shetani khathaan usipoyajibu yanaumia roho kweli, mimi ndio nimeyamsliza kwa kuyasweka kwenye ignore list kabisa.

Huwezi kumprovoke Lowasa mnapoteza muda wenu tu.
 
Ila kama kuna watu hapa JF ambao ni wasanii wa kutupwa basi ni wewe Mzee Tupatupa, a.k.a VUTA-NIKUVUTE, posts zako mtu akizisoma haraka anaweza kudhani wewe ni CCM lakini kiukweli wewe ni UKAWA damudamu
 
Kwanza utambue Lowasa sio tu mwanasiasa bali ni mwanasiasa nguli na mchezo wa siasa anaujua vizuri..
Sasa hayo maneno, tuhuma na mishale yote anayorushiwa ataijibu pale jangwani siku ya kufunga kampeni tar 24 October..

Wakati huo muda wa wale wanaomtuhumu kurudi jukwaani kujibu utakua umekwisha na kampeni zimefungwa..

Maana yake wananchi tutaenda kupiga kura tar 25 tukiwa na ukweli wote wa tuhuma anazorushiwa hasa hasa Richmond kutoka kwa mhusika mkuu..!

Tukutane #jangwani tar 24 October kupata majibu kamili ya tuhuma zote..!
 
Mzee tupatupa lowasa ni great thinker hawezi kujibu hoja zisizo na mashiko.mwaka huu mtaisoma namba malofa ngastukaa kura kwa edo mtoto wa ngoyayi
 
Nilichogundua ni kwamba pro ccm wanafuatilia kampeni za lowassa kuliko za mgombea wao. Na hata mzee wa hapa kazi tu naye anafuatilia kampeni za lowassa kuliko hata wana ukawa. Hata NEC hawako nyuma. Kweli uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria.
 
Hii style ya Lowasa nimeipenda hata humu JF ile mijingajinga kama kina ritz na shetani khathaan usipoyajibu yanaumia roho kweli, mimi ndio nimeyamsliza kwa kuyasweka kwenye ignore list kabisa.

Huwezi kumprovoke Lowasa mnapoteza muda wenu tu.
Mkuu kuna mtu anaitwa Chin huyu kwa siku anaweza andika hata mabandiko elfu moja hakuna hata moja linalokaribiana na Ukweli na hakati tamaa , sasa hivi bandiko lolote aliloandika Chin watu hatusomi kabisa kwa kujua alichoandika ni uwongo. waige uandishi wa Tupatupa anaandika uwongo uliochanganywa na ukweli.
 
Last edited by a moderator:
LOWASA SIO SIZE YENU MBONA MMEKUWA WAGUMU KUELEWA.

LOWASA SIO SIZE YENU HIVYO HANA MUDA HUO .

pilusonyo.
#Nimehamia ukawa kwa mapenzi yangu mwenyewe.
 
lowasa hata akikaa jukwaani akajitangaza yeye mwenyewe kuwa ni mwizi fisadi na mbadhirifu bado wananchi tutamchagua hata mseme nini...ndo tunamtaka
 
Back
Top Bottom