Lowassa: Tumewashika CCM Pabaya

Lowassa: Tumewashika CCM Pabaya

Ocampo four

JF Senior Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
5,789
Reaction score
2,159
Mgombea urais wa Ukawa kupitia CHADEMA Ndg. Edward Lowassa kasema kwa sasa Chama Cha Mapinduzi kiko hoi.... Lowassa kasema Ukawa wamewashika pabaya sana CCM na ifikapo tarehe 25 hawachomoki hata kwa dawa...

Lowassa kawaomba vijana, wakina mama, wazee na makundi mbalimbali siku ya kupiga kura (25.10.2015) kuwahi asubui sana katika vituo vya kupiga kura na kumchagua Lowassa, wabunge wa Ukawa na madiwani wa Ukawa...

Katika hatua nyingine mchambuzi wa siasa Professor Mbele kasema safari hii Ukawa watashinda kwa asilimia nyingi. Mbele kasema haoni miujiza ambayo CCM wanaweza kufanya kwa hizi siku 41 zilizobaki na kubadilisha mawazo ya wananchi wakati asilimia 89% ya wapiga kura washafanya uamuzi na mojority watamchagua mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa....

Mytake:... Wazee wa Lumbumba tukutaneni 25.10.2015.

==============================

*Sumaye asema hakuna wa kukifufua chama hicho

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa, amesema wamekikamata pabaya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa Watanzania sasa wanataka mabadiliko.

Amesema pia kwamba, kitendo cha mamilioni ya Watanzania kutaka mabadiliko, pia kinaungwa mkono na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyewahi kusema Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.

Kutokana na hali hiyo, amewataka wanaokosoa Ukawa, wawe na hoja za msingi badala ya kutukana.

Lowassa aliyasema hayo mjini Kimboi, Jimbo la Iramba Magharibi, mkoani Singida, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiomboi Bomani.

"Nimekuja hapa kwa heshima kubwa ili niwaombe kura kwa sababu uchaguzi ni mchezo wa hesabu, bila kura za kutosha hatuingii Ikulu ng'o.

"Nawaambia tusiwapowashinda mwaka huu, hatutawashinda tena, lazima waondoke kwa sababu Watanzania wanataka mabadiliko, tunazo baraka za Mungu na Mwalimu Nyerere.

"Wameanza kutuiga lakini wajue tunayoyafanya tumetoka nayo mbali, tumewakamata pabaya kwa sababu wananchi wanataka mabadiliko na sisi tuko tayari kwa mabadiliko, mabadiliko haya ni ‘unstoppable (hayazuiliki),"alisema Lowassa.

Akizungumzia ajira kwa vijana, Lowassa alisema atakapoingia madarakani, Serikali yake itaanzisha Benki kwa ajili ya vijana wanaoendesha boda boda pamoja na benki ya wachimbaji wadogo wadogo.

Kwa mujibu wa Lowassa, sekta nyingine zitakuwa zikipatiwa ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili kulingana na wakati husika.

"Nasema tutaondoa umasikini nchini kwa sababu nitaunda Serikali inayofanya kazi kwa kasi na asiyekuwa na uwezo wa kukabiliana na kasi yetu, atupishe.

Awali akihutubia mkutano mwingine katika Kijiji cha Ilogelo Jimbo la Singida Kaskazini, mgombea urais huyo alisema kama Watanzania hawatapiga kura za kuiondoa CCM madarakani, watakuwa wamejiangamiza.

Alisema kwamba, ingawa CCM wamekuwa wakitoa ahadi nyingi kwa wananchi, wamekuwa hawatekelezi ahadi hizo, jambo linalowafanya Watanzania wasiwe tena na sababu ya kukiamini chama hicho.

"CCM hawataki mabadiliko ingawa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Watanzania wasipopata mabadiliko ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM.

"Najua wananchi wanataka mabadiliko ndiyo maana niliwahi kusema siwezi kuzuia mafuriko kwa mikono lakini wakanidharau.

"Matokeo yake sasa yanaonekana kwa sababu tulipokwenda Iringa, mafuriko yalikuwa ni haya haya, tulipokwenda Ruvuma, mafuriko ni haya haya, tulipokwenda Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma, mafuriko yalikuwa ni haya haya.

"Sisi hapa tumejitokeza kuongoza mabadiliko ili yaje, lakini jambo la msingi kwenu ni kupiga kura ili mabadiliko hayo yaje.

"Msipopiga kura tukashinda, mtakuwa mmejiangamiza na msipopiga kura za uaminifu, mtaibiwa, CCM ikishinda mambo yatakuwa ni yale yale.

"Nawaambieni bila kura za kutosha tumeliwa na ili tushinde, mwambie hata rafiki yako aliyeko popote, iwe na Dare es Salaam au kwingineko nchini, kwamba Lowassa anataka kura yako.

"Kama mtanionyesha imani ya kutosha kwa kunipa kura za kutosha, nawaahidi utumishi uliotukuka kwa sababu imani huzaa imani" alisema Lowassa na kushangiliwa.

Pamoja na hayo, Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu, aliwataka pia Watanzania wasidanganywe na maneno ya baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

Alisema kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu, yatatolewa maneno mengi yakiwamo yasiyokuwa na maana na kwamaba jambo la msingi ni wananchi kuwa na msimamo wa kuiondoa madarakani CCM.

Akizungumzia mazao ya alizeti, nyanya na vitunguu yanayolimwa mkoani Singida, alisema atakapoingia madarakani, atajenga viwanda vya kusindika mazao hayo badala ya utaratibu wa sasa ambapo mazao hayo yananunuliwa na Wakenya.

LISSU

Naye Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema Lowassa ndiye kiongozi anayeifaa Tanzania kwa kuwa ana uwezo mkubwa kisiasa kuliko mwanasiasa yeyote nchini.

Pamoja na hayo, Lissu alitumia muda mwingi kuwaeleza wananchi jinsi Lowassa asivyohusika na kashfa ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond.

Katika maelezo hayo aliyoyatoa katika mikutano ya Singida Kaskazini na Iramba Magharibi, Lissu alitumia kitabu cha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyosomwa bungeni mwaka 2008 na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe.

MSINDAI

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Singida ambaye pia ni mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini kupitia Chadema, Mgana Msindai, aliendelea kusema CCM haina tena sifa za kuongoza Tanzania kwa kuwa imepoteza mwelekeo.

Pamoja na hayo, alimshutumu aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM), kwamba ameshindwa kuwasaidia ajira vijana wa jimbo hilo licha ya kuliongoza kwa miaka 15.

MGEJA

Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, alisema kitendo cha baadhi ya vigogo wa CCM kuhamia Ukawa ni dalili ya chama hicho kupoteza mwelekeo.

Alisema ni aibu kwa Watanzania kuendelea kukiunga mkono CCM wakati shida zimekuwa zikizidi kila mwaka ingawa nchi ina rasilimali za kutosha.

Sumaye: Hakuna wa kuifufua CCM

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, alisema kwa sasa hakuna njia au mtu atakayeweza kuifufua CCM.

Sumaye alisema wamezunguka maeneo mengi ya nchi kila walipokuwa wakienda wamebaini Watanzania hivi sasa wanahitaji mabadiliko na hawana mpango wa kuongozwa tena na CCM.

Aidha Sumaye alipingana na wale wanaosema amejiunga Ukawa kwa uchu wa madaraka, na kusema kuwa uchu wake wa kujiunga Ukawa ni kutaka kuing'oa CCM.

"Sikuja Ukawa kutafuta cheo kwa sababu nimeshakuwa waziri mkuu na hata hapa Ukawa hakuna nafasi ninayotaka kwa sababu nafasi ya urais yupo Lowassa na nafasi ya waziri mkuu siwezi kupata kwa sababu sijagombea ubunge ila ninachofanya ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani," alisema.

Sumaye alisema kwa kuingia kwake Ukawa, amejikuta akipata vitisho kutoka serikalini ikimtishia kumny'anyang'anya mashamba yake, kitu anachokiona ni sawa na kumpiga chura teke.

"suala la kunitisha kuninyang'anya mashamba yangu ni kunikomaza zaidi kwa kuwa naamini suala hilo ni sawa na kumpiga chura teka." alisema.
Chanzo: Mtanzania
 
Mgombea urais wa Ukawa kupitia CHADEMA Ndg. Edward Lowassa kasema kwa sasa Chama Cha Mapinduzi kiko hoi.... Lowassa kasema Ukawa wamewashika pabaya sana CCM na ifikapo tarehe 25 hawachomoki hata kwa dawa...

Lowassa kawaomba vijana, wakina mama, wazee na makundi mbalimbali siku ya kupiga kura (25.10.2015) kuwahi asubui sana katika vituo vya kupiga kura na kumchagua Lowassa, wabunge wa Ukawa na madiwani wa Ukawa...

Katika hatua nyingine mchambuzi wa siasa Professor Mbele kasema safari hii Ukawa watashinda kwa asilimia nyingi. Mbele kasema haoni miujiza ambayo CCM wanaweza kufanya kwa hizi siku 41 zilizobaki na kubadilisha mawazo ya wananchi wakati asilimia 89% ya wapiga kura washafanya uamuzi na mojority watamchagua mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa....

Mytake:... Wazee wa Lumbumba tukutaneni 25.10.2015......

Hata Mzee wa kaya JK kakiri jana akiwa anamnadi mgombea urais wa Zanzibar kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni kama mchezo wa mpira wa miguu hivyo timu yake yaani CCM magamba watumie mtindo wa kukaba mtu kwa mtu, kwa maneno yake mwenyewe alisema " Man to Man" Maneno haya yanatudhihirishia kitu kimoja tu kwamba CCM inashindwa.
 
mwache mzee ajifariji Ila ifikapo Siku ya Siku asije kuanguka kwa presha

Hakuna dalili wala kishiria chochote kinachoonyesha kuwa CCM itashinda..... Kwa hizi siku 41 wajiandae kisaikolojia kutoka madarakani
 
Mmeshikana pabaya ukawa wenyewe,hakuna wakuwashika pabaya watu wenye akili hata siku moja,mwizi mwizi tu hata awe handsome,mbona hamkemei ufisadi?adui namba nne baada ya ujinga,maradhi,na umasikini.
 
Mimi nafurahi sana kusikia hayo maneno mazuri,ila kuna habari policcm wameingiza magari mapya defender za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha ccm inarudi kundini na kibaya zaidi kuna habari pia maafisa wa jw watavaa uniform za police kuhakikisha kazi yao inaenda vizuri,kikubwa ni kuombea taifa amani ili hawa ccm waikabidhi nchi ikiwa salama,jamani hizi ni mbio za kupokezana vijiti,ccm wamekimbia kwa miaka 50,na wamefanya mengi mazuri na mengi mabaya,sasa wakabithi tena kijiti kwa ukawa na wao wakimbie tuone watatufikisha wapi,then mchezo ukiwashinda tunarudisha kijiti kwa ccm ndo hivyo tu,maana wote tunachohitaji ni maisha bora na pesa tuione,sio wachache wahodhi kila kitu bila kuulizwa,hilo ndo hatutaki kabisa tena kulisikia
 
Mgombea urais wa Ukawa kupitia CHADEMA Ndg. Edward Lowassa kasema kwa sasa Chama Cha Mapinduzi kiko hoi.... Lowassa kasema Ukawa wamewashika pabaya sana CCM na ifikapo tarehe 25 hawachomoki hata kwa dawa...

Lowassa kawaomba vijana, wakina mama, wazee na makundi mbalimbali siku ya kupiga kura (25.10.2015) kuwahi asubui sana katika vituo vya kupiga kura na kumchagua Lowassa, wabunge wa Ukawa na madiwani wa Ukawa...

Katika hatua nyingine mchambuzi wa siasa Professor Mbele kasema safari hii Ukawa watashinda kwa asilimia nyingi. Mbele kasema haoni miujiza ambayo CCM wanaweza kufanya kwa hizi siku 41 zilizobaki na kubadilisha mawazo ya wananchi wakati asilimia 89% ya wapiga kura washafanya uamuzi na mojority watamchagua mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa....

Mytake:... Wazee wa Lumbumba tukutaneni 25.10.2015......

Aliye hoi zaidi ni CCM au yeye mwenyewe ambaye hata kupanda jukwaani anapandishwa kwa kushikwa masaburi, hata kipaaza sauti anashukiwa. Kwahiyo kitatokea bahati mbaya akawa Rais akipenda kwenye mikutano ya kimataifa Kama UN ataomba ahutubie akiwa amekaa
 
Mimi nafurahi sana kusikia hayo maneno mazuri,ila kuna habari policcm wameingiza magari mapya defender za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha ccm inarudi kundini na kibaya zaidi kuna habari pia maafisa wa jw watavaa uniform za police kuhakikisha kazi yao inaenda vizuri,kikubwa ni kuombea taifa amani ili hawa ccm waikabidhi nchi ikiwa salama,jamani hizi ni mbio za kupokezana vijiti,ccm wamekimbia kwa miaka 50,na wamefanya mengi mazuri na mengi mabaya,sasa wakabithi tena kijiti kwa ukawa na wao wakimbie tuone watatufikisha wapi,then mchezo ukiwashinda tunarudisha kijiti kwa ccm ndo hivyo tu,maana wote tunachohitaji ni maisha bora na pesa tuione,sio wachache wahodhi kila kitu bila kuulizwa,hilo ndo hatutaki kabisa tena kulisikia

Mataifa ya nje wako macho sana katika uchaguzi huu Mkuu..... Kuna watu wasipoangalia watashitakiwa haraka sana....
 
Mmeshikana pabaya ukawa wenyewe,hakuna wakuwashika pabaya watu wenye akili hata siku moja,mwizi mwizi tu hata awe handsome,mbona hamkemei ufisadi?adui namba nne baada ya ujinga,maradhi,na umasikini.

Ni kweli Nyerere alituachia maadui watatu, nani kutuongezea adui namba nne?
 
Ccm kushindwa imejitakia. Hata wagombea wa wapo very disorganised kwa kwa kuishushua serikali iliyopo madarakani mbele ya wapiga kura. Huwa najiuliza Jakaya ana moyo wa aina gani kwani Magufuli anamtungua za uso kuhusu ulegelege, wizi na ufisadi mbele yake yeye kaganda tu na kujichekesha. Ningekuwa mie nampora kipasa sauti na kumjibu kuwa hata wewe ni mmoja wetu. Wanajichanganya na kutumia raslimali za nchi vibaya.
 
jamani ukawa na na malofa wengine fanyeni research!!reseach always bring a goog answear!!!njoeni na tafiti hapa c porojo za robot!!!ni mikoa ipi lowasa ataongoza kwa asilimia 90 na ipi pombe magufuli ataongoza kwa 90%!!!!!kwa mfano dar es salaam wamejiandikisha watu 2.8 milion!!wakati dar kuna wakazi 8 milion!!!acheni mambo ya media na upambe!!!dr magufuli ndiye rais mpaka sasa!!!research zinaonyesha anaungwa mkona kwa 90% mikoa ya simiyu,ruvuma,njombe,katavi,pwani,morogoro,dodoma,tanga,geita,tabora,shinyanga,mara,na rukwa!!!lowasa ana ungwa mkona kwa 90% manyara,arusha,kilimanjaro,singida,na iringa!!!!!na kwingine tanzania wanazidiana kwa karibu sana
 
kweli kwa sasa ukitaka kuwa ukawa lazima ujipime usije ukawa na akili kama za NYUMBU WA SERENGETI NATIONAL PARK!!!njoon na thread za kweli
 
ccm haiondoki madarakani leo wala kesho. poleni sana
 
Ni kweli Nyerere alituachia maadui watatu, nani kutuongezea adui namba nne?

Kwa maneno yako inaonesha kwamba Nyerere alishindwa kuondoa hao maadui watatu na ndio maana unasema ...alituachia...

Kwa maana hio unasema kwamba mpaka leo hii maadui ni wanne. Hivyo maadui wale watatu bado wapo.

Huoni kwamba unakubali hoja kwamba serikali iliopo madarakani imeshindwa kuondoa maadui hao watatu/wanne kwa miaka yote iliyokuwa madarakani?
 
watu kama vile wamechqanganyikiwa sijuwi ccm imewafanya nini asilimia kubwa ukiwauliza watu kuhusu ccm wanakuwa na majibu ya hasira dhidi ya ccm na hasira ambayo haiwezi kwisha kwa miezi 12 au zaidi!
 
Back
Top Bottom