Jamaa wajanja sana. Wamesubiri Bunge linaelekea ukomo wake ndipo wameanza kurusha mahojiano ya kujisafisha maana wanajua wangerusha kabla, swala lingerudi mjengoni na huenda mambo yangekuwa mabaya zaidi.
Lakini sasa wana uhakika kwamba hata wakiropoka hakuna kitakachorudi mjengoni. Come Nov 2010, Bunge litakuwa chini ya uongozi wa Spika mpya, ndipo sasa Richmond itakaporudishwa Bungeni Upya ili kukamilisha shughuli ya usafi na kuweka sawa mazingira kwa ajili ya 2015.
Kwa jinsi wabunge wetu wa CCM walivyo, wala sintashangaa iwapo watakaa kimya pindi ngoma ikirudishwa mjengo hapo 2011. Maana sijawahi kuona wabunge wa ajabu kama hawa wa CCM. Leo wanaweza kupitisha azimio/maamuzi fulani na serikali ikigoma kutekeleza, wao wanaufyata.
Kikwazo cha kurudisha hoja ya Richmond Bungeni ilikuwa ni Spika Sitta, kwa kuwa yeye anajinadi kuwa ni Mzee wa Kasi na Viwango, na kwamba ni mpambanaji wa ufisadi, asingekubali kurudisha hiyo hoja kwa ajili ya kumsafisha Lowassa. So, the right time is March/April 2011 chini ya Uongozi wa Spika Mpya na utasikia wanasema Lowassa alionewa. Wakati huo, si ajabu wajumbe wote waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mwakyembe watakuwa hawako mjengoni tena.