mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,183
- 1,083
Uchanga demokrasia ktk nchi zetu za kiafrika umepelekea harakati za kisiasa kuwagawa wananchi badala ya kuwaunganisha..sana sana pia uadui wa kisiasa umekuwa na makovu yasiofutika katika mioyo,nafsi na miili ya wanasiasa,wakeleketwa wao,wapinzani wao n.k. Mifano hai yapatikana Zambia,Zimbabwe,Ivory Coast,Sudan Kusini,Uganda,Jamhuri ya Afrika ya kati,Msumbiji,Malawi n.k.Magonjwa sugu ya kisiasa likiwemo la Saratani za chuki,visasi,mapambano,ushindani,mivutano kisiasa mengi yamekuwa yakidumaza ustawi wa mataifa mengi ambako demokrasia bado ni changa kwa sababu ya changamoto mbalimbali za kihistoria,kiuchumi,kikatiba,kiitikadi na kimfumo.
Kwa heshima kubwa na Taadhima natoa ushauri kwa Mh. Edward N. Lowassa kustaafu na kujitenga kabisa na shughuri,mikakati ya kisiasa,michakato,Harakati za kisiasa .Ni ukweli usiopingika ya kuwa vuguvugu la uchaguzi mkuu uliopita lilikuwa kubwa mnooo kuwahi kutokea ktk historia ya nchi yetu.Idadi kubwa ya wanajamii iliweka wazi hisia zao juu ya nani wako nyuma yake hasa ktk mbio za kuusaka urais wa JMT.
Hatua ya Kapteni Mstaafu Lowassa kustaafu siasa itawafanya wengi waokoke {kuokoka ni kuzaliwa upya} kisiasa hivyo kufuta machungu,maumivu,mapigo,hisia za visasi,hisia za kuonewa,hisia za kukandamizwa na hisia za kuchukiwa sababu tu ya kumuunga mkono Lowassa wa Ukawa.Pia Kitendo cha Lowassa kustaafu kutapelekea wengi kusamehewa na vyama vyao {tuhuma za usaliti},jamii zao,rafiki zao,washirika zao,viongozi wao.Zaidi sana Kustaafu kutamfanya apumzike kwa amani kwa kujiweka mbali na mishale ya mashambulizi ya kisiasa,propaganda,ajali za kisiasa,mikakati ya kumdhoofisha dhidi ya malengo na maono kisiasa.
Kustaafu kwa Mh. Lowassa kutapelekea vyama kufanya maridhiano yahusuyo kutibu saratani ya kisiasa wanayougua wengi kimya kimya ndani ya vyama vyao ambo ni waathirika wa mikwaruzano,misuguano,kuchomekeana,kuchafuana,kukatana,kutia nia,kuchokonoa nia,kutenguliwa,kuhujumiwa,kuenguliwa,kura kutokutosha na mengineo.
Lakini ni ukweli usiopingika ya kuwa mengi ya madhara tajwa hapo juu ni matokeo ya siasa za nchi yetu kipindi hiki na kilichopita kujiegemeza kwa mtu zaidi kulikochama {kumtegemea mtu/mtu kuwa maarufu kuliko vyama au chama cha siasa}.Kwa mfano mfumo uliozoeleka wagombea wa nafasi ya Urais kutanguliza chama kwanza kisha wagombea/watia nia baadae haukuwa na hatamu kabisa bali utashi/mvuto/upako wa mgombea ndio uliokuwa dira ya kushinda au kushindwa.