samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 215
mpinga ufisadi anayepanda jukwaa moja na fisadi ni fisadi pia.
E.L bado ana nguvu na anakubalika kwa wananchi, Atakumbukwa kwa mengi kuumwa kwake kumechangia kushindwa. Pengo lake linaonekana. Mzee wa vitendo hakika ndo karata ya mwisho 2015. Wanasiasa watendaji kama huyu mzee namfananisha na Rais Kagame.Maneno mengi co kipaumbele cha kizazi hiki. Action speeks louder than words. Lwaigwanani for presidency 2015
This is not a classic analysis...hata siku moja haiwezekani sitta kuwa kambi moja na lowassa...lowassa ndiye aliweka kambi ymtu wake arumeru....ole sendeka alisharudi kny kambi ya lowassa zamani sana kwani nimbunge maslahi ancheki upepo unavovuma.....so ni kambi mbili za lowassa(arumeru) na sitta (kirumba na mbeya )ndo zimeshindwa.......classic analysis and well thought, big up mjomba wa DS.
Yes wakakae wakijua wako ndani yachama dhaifu, watoke wajiunge na CDM wapambane nje hawawezi kujifungia ndani na kusemana kwa maovu ndani ya chama wakitoka nje wanasema Kidumu cha cha mapinduzi" If can not fight withiin the system then get out Unafanya nini" tuendako ukivaa jezi ya kijani ushujaa wako automatically unaporomoja
Pole CCM na Hongera CDM
ARUMERU alikuwapo fisadi LOWASA na ndiyo maana wananchi wakatoa somo kuwa hataki Tanzania yenye mafisadi,mzee sitta anaipenda CDM ndiyo maana alikataa kuiba kura kama walivyopanga magamba,mzee ni msafi sana.Kambi ya wale wanaojiita wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama tawala cha CCM imepata pigo kubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki na chaguzi za udiwani katika kata 8 tofauti. Kambi hiyo ilitoa wafuasi wake watatu kushiriki katika kampeni za chaguzi hizo mbalimbali. Samuel Sitta ambaye ndio kiongozi wa kambi hiyo alipiga kambi jijini Mwanza na kuongoza kampeni katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kirumba na kushindwa kuwashawishi vilivyo wakazi wa Kirumba ambao walimchagua mgombea wa CHADEMA kuwa diwani wao. Naye Anne Kilango alipiga kambi huko kiwila kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwira lakini naye aliangukia pua kwani mwisho wa siku mgombea wa CHADEMA aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa CCM. Kama hiyo haitoshi, Christopher Ole Sendeka alikuwa mmoja wa wana ccm walioshiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki lakini pia ushawishi wake na ule wa makada wengine wa ccm haukutosha kubadili mawazo ya wananchi wa Arumeru ambo bila ajizi wamemchagua Joshua Nassari wa CHADEMA kuwa mbunge wao. Matokeo hayo kwa ujumla ni pigo kubwa kwa kambi ya Samuel Sitta ambayo wakati Fulani ilionekana kuaminiwa na wananchi hasa wakati huu ambapo Samuel Sitta ameshaeleza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sasa wananchi wameonesha kwamba hawana imani hata na wana CCM wanaojipambanua kama wapinga ufisadi. Sasa nani aaminiwe katika CCM????!!!!!!!
Yes wakakae wakijua wako ndani yachama dhaifu, watoke wajiunge na CDM wapambane nje hawawezi kujifungia ndani na kusemana kwa maovu ndani ya chama wakitoka nje wanasema Kidumu cha cha mapinduzi" If can not fight withiin the system then get out Unafanya nini" tuendako ukivaa jezi ya kijani ushujaa wako automatically unaporomoja
Pole CCM na Hongera CDM