Lowassa: Sihusiki na Richmond, ilitungwa kunichafua. Sitohama CCM!

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Waziri Mkuu aliejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;

1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.

2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki naye alikuwepo. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?

3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.

4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.

5. Anasema: Hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndie aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.

6. Amesema: Hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.

7. Amesema: Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
Lowassa: Nimeingia CCM tangu mwaka 1977. Maisha yangu yapo CCM; Mafanikio ilyopata CCM yasiifanye ikabweteka mwaka 2015; upinzani umeimarika

8. Amesema: Toka nimetoka Serikalini; tumekuwa wagumu wa kufanya maamuzi. Kila kitu ni legelege! Waganda, wakenya na wanyarwanda wanatupita!

9.Amesema: Afya ni neema toka kwa Mungu, nawahakikishia watanzania kuwa "Am fit and Kicking" nashauri watangaza nia wote tupimwe wote afya

10.Amesema: Arusha itawaka moto tarehe 30 Mei 2015; watanzania tegeni sikio kwani nitaanika kila kitu kuhusu mustakabali wa nchi hii!

Hayo ni kwa ufupi. Wahariri wakuu katika media zote kupitia Jukwaa la Wahariri walikuwepo, na Absalom Kibanda (New Habari) na Nevil Meena (Free Media) ndio walikuwa waratibu wakuu wa mkutano huu.

Bonyeza HAPA kumsikiliza
 

Attachments

  • JamiiForums.mp3
    2.7 MB · Views: 2,522
Mwana Mpotevu

Jamani TZ,Lowassa anataka tuamini kuwa watz kupitia bunge letu ni stupid.Lowassa akiwa waziri mkuu alionyesha ni mtu ambaye atakumbatia rushwa,suala la richmond kwa watu tunaojua jinsi serikali inavyofanya kazi inamuweka kwenye hatia,kama hakuwa yeye basi alikuwa nani?.
 
Last edited by a moderator:
Jamani TZ,Lowassa anataka tuamini kuwa watz kupitia bunge letu ni stupid.Lowassa akiwa waziri mkuu alionyesha ni mtu ambaye atakumbatia rushwa,suala la richmond kwa watu tunaojua jinsi serikali inavyofanya kazi inamuweka kwenye hatia,kama hakuwa yeye basi alikuwa nani?.

Unayajuwa madudu ya Mwakyembe? Kaa kimya kazi imeanza.
 
Wote hawa Ma CCM hawafai

Kama wanaipenda nchi haikupaswa kukaa siku zote kutoanika wahusika wakuu wa Richmond hadi muda wa kampeni

Hata kama ukimtaja JK kuhusika na Richmond....what does it help?

Hatutaki sarakasi hapa

Bottom Point ni kwamba Kansa ya taifa hili ni Management Mbovu ya serikali ya CCM

Tiba pekee ni kuwaweka CCM pembeni

Nasisitiza hata at "a gun point" bila kuiweka CCM pembeni nchi yetu itazidi kuangamia
 
Kila nikumbuka historia ya Sauli, Goliati na Daudi huwa nawaza mara mbili.. Yote kwa yote mioyo yao imefanywa migumu ili lililokwisha kutabiriwa litokee..
 
Lowassa amechanganyikiwa, kwamba serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo kwanza badala ya elimu kwanza. Hivi ujenzi wa shule za Kata nchi nzima , ujenzi wa vyuo vikuu na ongezeko la udahiri wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu na kilimo kwanza nini kilitangulia?
 
Back
Top Bottom