Lowassa: Rais Magufuli ni mfano wa viongozi wa Afrika wasio na maono

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,598
36,023
Edward Lowassa leo ameamua kumuelezea ukweli rais Magufuli kuwa ni miongoni mwa marais wa Afrika wasio na maono. Lowassa pia amesema kuwa Tanzania chini ya Magufuli itakosa kabisa ubunifu.

Hayo yanajiri baada ya rais John Magufuli kuzuia mambo mengi kwa lengo la kubana matumizi. Huku wataalam mbalimbali wakikwama kuwekeza kwenye taaluma baada ya kuzuiwa kupata mafunzo mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Aidha rais Magufuli amekuwa akitoa hotuba kwa hisia kali hali inayowafanya wasaidizi wake kuingiwa na woga kwenye uthubutu.

"Magufuli amewafanya wasaidizi wake kukosa kabisa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi. Tanzania chini yake haitakuwa na jipya" amesema Lowassa.

Aidha Lowassa amesema kuwa sera ya elimu bure kwa Magufuli imekuwa "zero" baada ya kuiga.
 
Ni kweli kuna watu wameshindwa kwenda kusoma nje ya nchi kutokana na agizo hili!

Maneno ya Lowassa kwa sasa hayataeleweka mpaka madhara yaanze kujitokeza maana Watanzania hungoja matukio ndio washutuke na kisha waanze mijadala.
 
Politically, Lowassa is finished!

Kwa sasa yuko katika njia ya kisiasa aliyopitia Augustino Mrema.

Kila akisimama kwa sasa atatueleza kuwa eti aliibiwa kura wakati alituambia hakuna hata kura moja itakayoibwa. Huu umekuwa ni wimbo kwa mtu mwenye vision!

Mbaya zaidi kwa usanii wake hajatuambia kama amemtambua Magufuli kama Rais wa Tanzania.

Nilisikia aliwauliza wanaMwanza eti kama wamemsahau! Alidhani watamdekia tena barabara!

Yeye aendelee tu na vision yake ya kifisadi na kisanii.

Yes, Rais Magufuli sio Maraika kwa sababu ni binadamu lakini mapungufu yake kiutendaji ni zaidi ya vision na utendaji wa Lowassa.
 
Politically, Lowassa is finished!

Kwa sasa yuko katika njia ya kisiasa aliyopitia Augustino Mrema.

Kila akisimama kwa sasa atatueleza kuwa eti aliibiwa kura wakati alituambia hakuna hata kura moja itakayoibwa. Huu imekuwa ni wimbo kwa mtu mwenye vision.

Yeye aendelee tu na vision yake ya kifisadi na kisanii.
Kwa LOWASSA mtasubiri sana!
 
Edward Lowassa leo ameamua kumuelezea ukweli rais Magufuli kuwa ni miongoni mwa marais wa Afrika wasio na maono. Lowassa pia amesema kuwa Tanzania chini ya Magufuli itakosa kabisa ubunifu.

Hayo yanajiri baada ya rais John Magufuli kuzuia mambo mengi kwa lengo la kubana matumizi. Huku wataalam mbalimbali wakikwama kuwekeza kwenye taaluma baada ya kuzuiwa kupata mafunzo mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Aidha rais Magufuli amekuwa akitoa hotuba kwa hisia kali hali inayowafanya wasaidizi wake kuingiwa na woga kwenye uthubutu.

"Magufuli ewafanya wasaidizi wake kukosa kabisa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi. Tanzania chini yake haitakuwa na jipya" amesema Lowassa.

Aidha Lowassa amesema kuwa sera ya elimu bure kwa Magufuli imekuwa "zero" baada ya kuiga.
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom