Mheshimiwa Edward N.Lowasa, Mbunge wa Monduli na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu ktk awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais anayemalizia muda wake sasa Jakaya M.Kikwete. Nilifuatilia mchango wake alioutoa bungeni majuzi alipokua anachangi hoja moja wapo bungeni Dodoma. Kwanza alijikita moja kwa moja kwenye hadhira ya kuutaka Urais ujao. Amejenga kujiamini ili kuushawishi uma kuwa yeye ndio 'Action Man' (mtu wa maamuzi) pekee nchini anayepaswa kupewa ridhaa ya kuongoza umma. Alionekana wazi kutoridhishwa na ukimya uliokuwa umetanda nchini dhidi ya sitofahamu ya EAC. Alipigia Chapuo SADC, na ukanda wa biashara Kongo na kuonekana wazi kuichana EAC. Swali hapa linakuja iweje tena leo anakuja na hoja ya kumuunga mkono Kikwete baada ya hotuba yake kwa umma kupitia Bunge na msimamo wa Taifa kuendelea na EAC. Kumbe Lowasi ni sawa na mimi tu wote tuko nyuma ya PAZIA. Hongera Kikwete kwa kumaliza ukimya.