Lowassa na bomu lijalo

Mazoko

JF-Expert Member
Jul 10, 2009
674
184
Naomba kuleta hoja hii mbele yenu tuijadili hoja kama hoja na sikumjadili Lowassa au nafasi aliyokuwa nayo kama waziri mkuu.

Kuna vitu twaweza kubeza na kunavitu nilazima vifanyiwe kazi kwa faida ya Taifa ili tuendelee kuhubiri amani


Mh.Lowassa mara kwa mara ameonekana kuguswa na vijana ingawa nibaada yakuenguliwa uwaziri mkuu kuwa nilazima kuwaangalia vijana na kuwasikiliza hasa wasiokuwa na ajira rasmi lasivyo nibomu lijalo ambalo likilipuka hakuna atakayeweza kulizima.


Nimefanya ziara fupi isiyo rasmi kuzunguka katika baadhi ya maeneo hapa Dar-es-Saalam kuangalia vijana wenzangu wana fanya nini na nini wamekosa na mawazo yao niyapi juu ya mstakabari mzima wa maisha yao.Kwa kweli inasikitisha hasa ukiona jinsi walivyokata tamaa ya maisha yao ningumu kupata kujuwa wanafikiri nini hapo baadaye.


Sehemu nilizo kwenda ni Kariakoo,Tandale,Ubungo mataa na Tandika sokoni.Kwa wale wazoefu au waliokwisha wahii kupita maeneo hayo wanaweza kukubaliana na mimi kuwa taifa linapoelekea si salama tena.Kwa nini nasema hivyo nikwakuwa watu hawa wanafanya shugulizao katika maeneo yasiyo rasmi na salama kwao na watumiaji wengine wa maeneo hayo.


Mfano eneo la Kariakoo utakuta vijana wamepanga vitu vyao barabarani sehemu ambayo gari linatakiwa kupita lakini wao wanaona ndiyo sehemu yakupata mkate wao wasiku.Juzi nilishuhudia gari likishambuliwa na vijana hao eti gari limekanyaga biashara zao.nilijaribu kuongea na baadhi yawaliokuwa wanafanya vurugu majibu niliyoyapata nikuwa hivi ndivyo wanataka tuishi kwa kufanya biashara barabarani wao na magari yao watajuwa niwapi pakwenda hatuogopi mtu tuko tayari kwa vita huku mwingine akiwaambia mgambo kuwa hapa hamnipeleki wala kuchukua mali zangu labda mniuwe maana mwenzeni kaisha chukua hela (RUSHWA) ilikuwa nipatashika.


Eneo la UBUNGO hapo sasa ndiyo panatisha zaidi kwanza hakuna eneo lakutosha kufanya biashara yoyote kwa kuwa sisalama kwa wao wenyewe kutokana na mitambo iliyopo pale na hata kwa watumia barabara maana kuna njia za watembea kwa miguu na mageti yakuingia kwenye ofisi za mitambo hiyo ya umeme.Najaribu kujiuliza hivi siku akatokea mwehu mmoja akaamua kujitoa muhanga na bomu si nchi nzima inakuwa gizani na taifa kupoteza vijana ambao ndiyo nguvu kazi wanaofanya biashara eneo hilo ambao wanafikia elfu mbili nakuzidi??


Najiuliza viongozi wa nchi hii nao wamekata tamaa kama vijana hawa na kuruhusu kila mtu afanye anavyotaka au wao hawawaoni?? yawezekana Kariakoo hakuna anayekwenda huko maana viongozi wetu wasasa huduma zote ni SUPERMARKETS.Je ubungo mbona nasikia mawaziri wanatembelea mitambo hiyo hawaoni? au wanapoenda Dodoma hawapiti hapo kwa kweli naona wamechoka kama hawa vijana bora siku zipite.Vurugu zilitokea Mbeya vijana wakakubali kumsikiliza mbunge wao Mbilinyi wakatulia ikitokea kwa taifa zima watamsikiliza nani ili watulie??????? HILI NI BOMU linalipuka mda wowote
 
Back
Top Bottom