Lowassa: Msipingane na msimamo wa Magufuli

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
720
FullSizeRender_8.jpg


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amewashauri Watanzania wasipingane na misimamo ya Rais John Magufuli mpaka itakapofika mwaka 2020.

Alisema wakati huo utafanyika uchaguzi mkuu na ndio wanaweza kufanya uamuzi.

Akihutubia viongozi wa chama hicho kutoka majimbo ya Muleba Kusini na Kaskazini jana, Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia Chadema alisema wanachama hao waache kubishana naye hadi watakapokutana katika uchaguzi wa 2020.

Hata hivyo, Lowassa ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu, hakuitaja misimamo hiyo ya Rais Magufuli lakini tangu aingie madarakani, kiongozi huyo wa Awamu ya Tano ya Tanzania, ameweka msimamo mkali katika suala zima la kubana matumizi ya Serikali, kudhibiti watumishi hewa, safari za ndani na nje zisizo na tija na rushwa. Mambo hayo yamesifiwa na watu wengi.

Lowassa aliwaeleza viongozi hao kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 unaweza kuwa rahisi zaidi huku akitaka wapinzani wapingwe kwa hoja na si kukandamizwa.

“Tupingane kwa hoja bila kuumizana na kutakiana mabaya, tuwasaidie wananchi wanaopata matatizo bila kuwapuuza,” alisema Lowassa.

Akizungumzia sababu ya kutembelea Mkoa wa Kagera, Lowassa alisema ni pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kura walizompigia na kuwapa pole kwa tetemeko la ardhi lililowakumba Septemba mwaka jana.

Kada wa zamani wa CCM aliyeongozana na Lowassa, Hamis Mgeja, licha ya kujivunia kukihama chama hicho alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda, chama hicho tawala kinajifuta taratibu kwa wananchi.

Baadaye, Lowassa, alishiriki kampeni za kumnadi mgombea udiwani katika Kata ya Kimwani, wilayani Muleba.

Kuhusu uhaba wa chakula

Katika mkutano huo wa ndani, Lowassa alizungumzia hali ya ukame inayoikabili nchi na kusema kuna tishio kubwa la uhaba wa chakula hivyo kuitaka Serikali isipuuze majanga yanayoweza kuwapata wananchi, bali iwasaidie kwa kauli na vitendo.

“Wananchi wasipuuzwe, kuna tatizo la njaa kwenye baadhi ya maeneo ya nchi, kwa hiyo wananchi wasaidiwe,” alisema Lowassa.

Wakati Lowassa akisema hayo Muleba, huko Bunda mkoani Mara, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtaka Rais Magufuli kuchukua hatua kukabili hali ya upungufu wa chakula nchini.

Akihutubia mkutano wa ndani wa viongozi wa chama hicho Jimbo la Bunda Mjini uliofanyikia katika Hoteli ya Harieth, Mbowe alisema ni ukweli usiopingika kwamba taifa linakabiliwa na uhaba wa chakula, hivyo ni Rais Magufuli anapaswa akubaliane nao.

Mbowe aliyetumia takribani dakika 12 katika hotuba yake, alisema ukali anaouonyesha Rais kuhusiana na taarifa za uhaba wa chakula nchini unatia shaka.

“Awasikilize Watanzania waliomchagua kwani ndiyo waajiri wake. Wanaposema wana njaa awasikilize na kuwasaidia. Kuna uhaba wa chakula... hili halina ubishi. Ni wajibu wa Serikali kuchukua hatua za haraka,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema si kweli kwamba kuna uhaba wa chakula kutokana na uvivu wa wananchi kwani wengi ni wachapakazi isipokuwa wamefikwa na hayo yote kutokana na mvua kutonyesha kwa wakati.

“Njaa haijaletwa na uvivu wa Watanzania, bali imeletwa na ukame ambao uko nje ya uwezo wao,” alidai Mbowe.

Alizungumzia pia hatua ya Serikali kubana matumizi akisema imechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa Deni la Taifa, kampuni nyingi kufungwa, kushuka kwa mapato ya taifa na uwekezaji pamoja na umaskini miongoni mwa Watanzania na kumtaka alegeze.

Awali, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche kwa pamoja walimwelezea mwenyekiti huyo kuwapo kwa uhaba wa chakula mkoani humo na kumwomba alisemee.

Bulaya alisema wakazi wengi wa wilayani Bunda wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula kutokana na ukame sambamba na mazao yao kuharibiwa na wanyama huku akisema watendaji wa Serikali hawataki kutangaza wakihofia kuondolewa kwenye nyadhifa zao.


Chanzo: Mwananchi
 
Siku tutakua kujua km Lowasa ni system itakuwa ni too late. Kwa afya chadema lowasa asiye front now kwenye chama chenu. Lowasa ni CCM na alikuja kugombea Urais tu ambao ameukosa. Chadema mwandaane mtu mwingine lowasa hatufai. Sasa hivi mmezolota sana chadema hampo relevant km zamani..mnaiga techniques za lowasa za kukaa kimya.. Mnakosea sana.
Hakuna kazi nyepesi km kuwa mpinzani nchi hii..tena kipind hiki kuna mambo Mengi ya kusema na kupinga.

Lowasa ni kirusi kwa chadema..lowasa ni system.. Lowasa ni kirusi kwa ustawi wa upinzani wa ukweli. Mshukuruni kwa kuleta wabunge wengi na asiwe mwenye chama.



hebu msome lowasa hapo chini


Lowassa: Msipingane na msimamo wa JPM

“Tupingane kwa hoja bila kuumizana na kutakiana mabaya, tuwasaidie wananchi wanaopata matatizo bila kuwapuuza,”



KIPANDE KIDOGO TU TAYAR KINA HOJA AMBAZO MAGUFULI ANAPATA AIBU KASEMA HAKUNA NJAA HAWEZ KUSAIDIA MTU WAKAT TAASISI ZA KIDINI ZISHAWATANGAZIA WAUMINI WAO SHIDA ILIYOPO NCHINI NANI ANAONEKANA TATIZO KWENYE JAMII?

HUWEZ KUPINGANA NA MAGUFULI KWA NGUVU TUMIA AKILI TU NA HOJA KILA SIKU ATAUMBUKA MANA HATA UKIPINGANA NAE KWA NGUVU HUWEZ KUMTOA MADARAKANI KAMWE NI HOJA TU ZA KUSHAWISHI WANANCHI.
 
Nahis JF imevamiwa kuna watu hawajaelewa.. Hawasomi wao wanaleta ushabiki.. Unajua ukimnyamazia mtu akafanya anachotaka ikifika uchaguzi atashindwa cha kusema maana atakua kashaboronga
 
Jamani jaribuni kumwelewa Lowassa, msitumie kichwa cha habari cha gazeti bila kusoma kilichoandikwa halafu hapo hapo upate majibu. Huo ni uvivu wa kufikiri na wa kutafuta maarifa.
Anachosema Lowassa ni kuwa tusimpinge bwana yule kwa mawe, rungu, mishale, na mikuki Bali tumpinge kwa hoja na kumuonyesha kuwaonyesha watu kuwa sisi ni bora zaidi yake.
Mfano mdogo ni hili swala LA njaa, hoja, Maelezo na ushahidi tayari umeisha mfanya bwana yule kuona aibu na wananchi wameisha anza kujua mbaya wao ni nani.
Haitaji hadi tumwage damu watu kujua hulka mbaya ya mtukufu Bali ni kujitofautisha nae ili watu waone tofauti yetu na hapo watajua pumba na mchele.
Muda ni mwalimu mzuri na unasema na watu watamwelewa Lowassa.
Acheni kukurupuka kama bwana yule, tukifanya hivyo tofauti yetu na yeye haitaonekana hivyo tutawapa watu taabu kuamua.
MWANAUME MJINGA HUVUNJA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE
 
hebu msome lowasa hapo chini


Lowassa: Msipingane na msimamo wa JPM

“Tupingane kwa hoja bila kuumizana na kutakiana mabaya, tuwasaidie wananchi wanaopata matatizo bila kuwapuuza,”



KIPANDE KIDOGO TU TAYAR KINA HOJA AMBAZO MAGUFULI ANAPATA AIBU KASEMA HAKUNA NJAA HAWEZ KUSAIDIA MTU WAKAT TAASISI ZA KIDINI ZISHAWATANGAZIA WAUMINI WAO SHIDA ILIYOPO NCHINI NANI ANAONEKANA TATIZO KWENYE JAMII?

HUWEZ KUPINGANA NA MAGUFULI KWA NGUVU TUMIA AKILI TU NA HOJA KILA SIKU ATAUMBUKA MANA HATA UKIPINGANA NAE KWA NGUVU HUWEZ KUMTOA MADARAKANI KAMWE NI HOJA TU ZA KUSHAWISHI WANANCHI.
Atakufa kihoro tu bora apumzike maana 2020 hatashinda Urais period!!
 
Uzuri wa lowassa hata kama anaouchu wa madaraka ni tofauti na waleee. Yeye hataki kuingia kukiwa na majeraha katika miili ya wananchi. Anachokiamini ni kuwa anapata uongozi kwa amani. Anaposema tushindane kwa hoja hiyo kauli ya busara na yenye upeo sana kwa aliye makini ila kwa vilaza wanaweza wakachukulia poa.
 
Siku tuta kuja kujua km Lowasa ni system itakuwa ni too late. Kwa afya chadema lowasa asiwe front now kwenye chama chenu. Lowasa ni CCM na alikuja kugombea Urais tu ambao ameukosa. Chadema mwandaane mtu mwingine lowasa hatufai. Lowasa ni mwenzao..anabiashara zake Hugo. Lowasa hana bifu na magufuli kabisa..tena anafurahi Namba moja anavyomnanga mtangulizi wake. Lowasa anabifu na jk tu na siyo Ccm. Sasa hivi mmezolota sana chadema hampo relevant km zamani..mnaiga techniques za lowasa za kukaa kimya.. Mnakosea sana.
Hakuna kazi nyepesi km kuwa mpinzani nchi hii..tena kipind hiki kuna mambo Mengi ya kusema na kupinga.

Lowasa ni kirusi kwa chadema..lowasa ni system.. Lowasa ni kirusi kwa ustawi wa upinzani wa ukweli. Mshukuruni kwa kuleta wabunge wengi na asiwe mwenye chama. Ni bora kuwa na zito kuliko lowasa..mpinzani gani hang'ati. Yupo yupo tu..! Lowasa anatabia ya kujijenga yeye badala ya chama. Mwaka 2020 mtashangaa. Mtoeni mapema front line. Awe mzee wa chama tu km mtei.

Sio Lowassa tu, hadi Mbowe pia wamtoe front row, hawa jamaa wawili wana kitu fulani kinachofanya wasiaminike kwa jamii kabisa, moja kati yao akirudia uchaguzi CDM wasahau kabisa kuchoma ikulu, hii miaka wangekaa wanamuandaa mtu mwingine kabisa mapema kimya kimya.
 
Siku tuta kuja kujua km Lowasa ni system itakuwa ni too late. Kwa afya chadema lowasa asiwe front now kwenye chama chenu. Lowasa ni CCM na alikuja kugombea Urais tu ambao ameukosa. Chadema mwandaane mtu mwingine lowasa hatufai. Lowasa ni mwenzao..anabiashara zake Hugo. Lowasa hana bifu na magufuli kabisa..tena anafurahi Namba moja anavyomnanga mtangulizi wake. Lowasa anabifu na jk tu na siyo Ccm. Sasa hivi mmezolota sana chadema hampo relevant km zamani..mnaiga techniques za lowasa za kukaa kimya.. Mnakosea sana.
Hakuna kazi nyepesi km kuwa mpinzani nchi hii..tena kipind hiki kuna mambo Mengi ya kusema na kupinga.

Lowasa ni kirusi kwa chadema..lowasa ni system.. Lowasa ni kirusi kwa ustawi wa upinzani wa ukweli. Mshukuruni kwa kuleta wabunge wengi na asiwe mwenye chama. Ni bora kuwa na zito kuliko lowasa..mpinzani gani hang'ati. Yupo yupo tu..! Lowasa anatabia ya kujijenga yeye badala ya chama. Mwaka 2020 mtashangaa. Mtoeni mapema front line. Awe mzee wa chama tu km mtei.
Aise kumbee eeeh
 
Jaman leo hajaongea huko makanisani nategemea atawajibu tena kwa lugha kama aliyotumia huko kagera watumish wa Mungu
 
. Lowasa hana bifu na magufuli kabisa..tena anafurahi Namba moja anavyomnanga mtangulizi wake. Lowasa anabifu na jk tu na siyo Ccm. Sasa hivi mmezolota sana chadema hampo relevant km zamani..mnaiga techniques za lowasa za kukaa kimya.. Mnakosea sana.
Hakuna kazi nyepesi km kuwa mpinzani nchi hii..tena kipind hiki kuna mambo Mengi ya kusema na kupinga.

.


Duh! Uelewa wako wa Siasa ukoje? Kwa hiyo ulitaka Lowasa awe na chuki binafsi dhidi ya Raisi Magufuli ndo awe mpinzani? Hivi Mbowe anawafundisha nini?
 
Alichomaanisha lowasa ni hiki usipingane na mtu njoo na hoja


Tanzania inatafuta mkopo wa dola milioni 200 kutoka benki ya dunia kwa ajili ya shirika lake la umeme Tanesco linalokabiliwa na mzigo wa madeni. Hayo yamesemwa na wizara ya nishati na madini leo, wiki mbili baada ya rais wa nchi hiyo kulikatalia shirika hilo kupandisha bei ya umeme ili kufidia gharama za uendeshaji. Rais John Magufuli anataka umeme wa bei nafuu ili kuwezesha ukuzaji wa sekta ya viwanda, lakini benki ya dunia inatazamiwa kusisitiza kuwa shirika hilo linaloendeshwa kwa hasara lipandishe bei ili kufidia gharama za uzalishaji umeme na kuanza kutekeleza mageuzi yanayohitajika. Wizara ya nishati imesema katika taarifa kuwa shirika la Tanesco lina madeni ya dola milioni 363, yakiwa yamepanda kutoka dola milioni 250 mwishoni mwa mwaka 2015. Mamlaka ya udhibiti wa sekta za maji na nishati nchini Tanzania EWURA, iliidhinisha kupandishwa kwa bei ya umeme kwa asilimia 8.53 Desemba 31, ongezeko ambalo ni chini ya nusu ya kile ambacho Tanesco ilisema ilihitaji ili kukidhi gharama.



Hauna asiyejua kama tanesco inaendeshwa kwa hasara rais anatakiwa kuamua mambo kwa busara aibu ya nani sana hata kama wakikopa hizo pesa zitalipwa na mtanzania sio magufuli wala ccm...
 
Back
Top Bottom