Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,940
- 19,129
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowasa amesema Magufuli anafanya ubabe kuwatishia wanachama wa CCM na vyombo vya habari.
Amesema kama ni kweli rais alitamka maneno ya kuwa wabunge wa CCM ni wasaliti kwa kumuona mbunge Godbless Lema basi afute kauli yake na kama hakusema basi akanushe kuwa hakusema.
Amesema ukiwa Rais haina haja ya kufanya ubabe wowote kwa kuwa wewe tayari ni rais na upo juu ya kila mtu.
Amedai nchi hii imejengwa kwa misingi ya ya umoja tangia kipindi cha Nyerere na tusibaguane kwa misingi ya vyama kwakuwa vyama ni vya mpito tu.