Huyu Mh. Lowasa atakuwa amefanya jambo la uhakika kama atatoa mchanganuo wa kura zake 10,268,795 anazodai alipata kwa kuonyesha kura kwa kila jimbo. Pia kwa vile anadai hizo kura ni 60% ya kura halali ina maana kura zote halali zilikuwa 16,562,573. Tume imeonyesha kuwa kura halali zilikuwa 15,193,862. Mh. Lowasa atafanya la maana sana kama atatueleza hiyo tofauti ya kura 1,368,711 imeenda wapi au ilifichwa wapi isionekane katika idadi ya wapiga kura za urais wala za ubunge nchi nzima. Akishindwa kuonyesha hayo na akaendelea kuhadithis ngonjera zake "nimeibiwa" bila ushahidi wa data atakuwa anaendelea kujidhalilisha na wenye akili wote wataendelea kumpuuza.