KirilOriginal
JF-Expert Member
- Feb 13, 2012
- 2,161
- 1,147
umetumwaa ee aliyekuambia lowasa fisadi ni nani.uliona escrow ili mtaja waziri mkuu na nani?
kama humpendi ni ww mwenyewe... niko hapa nairobi moi Avenual kila kona nasikia wakisema kule tz next prezidaa ni Lowassaaaa
Mkuu kwani Katiba imebadilika? Mimi mijuavyo ni kwamba hata kama hatagombea na kuwa mbunge lakini EL akichukua nchi, Serukamba atateuliwa kuwa Mbunge na atachukua Wizara nyeti na siyo ukuu wa mkoa. Take my wordsNaona ukuu wa Mkoa unamnyemelea kama jamaa kiwa Rais
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema huenda akamzuia Mbunge wa Jimbo la Kigoma, Peter Serukamba kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ili amsaidie jukumu muhimu kwenye safari yake ya matumaini.
Hivi watu mnaelewa maana ya kustaafu? Mbona hili neno kustaafu (retirement) linapotoshwa? Hivi Lowassa alistaafu uwaziri mkuu au alijiuzulu (resign)? Tuwekane sawa juu ya hili jamani
Akizungumza wakati wa kuomba udhamini kutoka kwa wanachama wa CCM mkoa Kigoma katika ofisi kuu ya CCM mkoa, Lowassa alisema Serukamba ni mmoja wa wanakamati katika safari hiyo ya matumaini.
Lowassa, anayewania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM alisema katika safari hiyo kama mwanakamati Serukamba anayo majukumu muhimu ambayo anapaswa ayatekeleze zaidi ya kugombea ubunge.Ndugu zangu wananchi wa Kigoma nimekumbuka jambo moja ninaye mwana kamati ambaye ni mtoto wenu hapa Kigoma, Mbunge wenu Serukamba, yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati yangu alikuwa na dhamira ya kugombea tena ubunge, lakini mnaweza msimuone maana atakuwa na majukumu makubwa ya kunisaidia kwenye kamati, alisema Lowassa.
Pamoja na kutogombea ubunge kiongozi huyo alisema Serukamba anayo dhamira ya dhati katika kuwatumikia wananchi wa mkoa Kigoma na ili kutimiza lengo hilo ameomba wasali na kumuombea sana ili aweze kupitishwa na chama chake kugombea Urais, lakini pia kushinda katika uchaguzi mkuu.
Serukamba ambaye kwa sasa anamaliza muhula wake kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anatarajia kugombea tena ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini.
Chanzo: Habari Leo
I can connect the dots now. Nilikuwa nikijiuliza inakuwaje Zitto Kabwe alitake jimbo la Serukamba?Wana ugomvi?kumbe yalikuwa makubaliano ya muda mrefu tu,kwamba Zitto gombea hapo mjini kwakuwa Mr F.u.c.k you atapangiwa majukumu mengine ndani ya chama chetu cha ACT. Kumbuka kwamba Lowassa alishasema hajajiandaa kushindwa,this means akipigwa rungu kule CCM he will fall back on ACT to fulfill his Presidential ambitions.
Lowassa ameongea kama vile ana uhakikia kwa asilimia 100 kuwa atateuliwa kugombea kupitia CCM. Tusubiri.
Rekebisha. Lowassa sio waziri mkuu aliye staafu bali ni waziri mkuu aliyelazimika kujiuzuru. Alilazimika hivyo baada ya kuonekana kuwa sehemu ya dili ya Richmond. Hadi sasa aliyefaidika sana ni Rostam Aziz na tangu hapo wamekuwa marafiki kupindukia kwamba Rostam anahaha awe Rais ili madili yaendelee kupigwa tu. Tutaendesha kampaini usiku na mchana kuzuia hili lisitokee.
CCM wakimpitisha Lowasa kama ndio mgombea wao, mi ntasubiri majukwaani tu kwenye kampeni.
Watamnadi vipi?watamsafisha Kwa njia ipi?, maana wenyewe ndio walisema yeye mchafu (Fisadi). Sasa nasubiri kuona kama atapitishwa na CCM, njia ipi itatumiwa kuwaambia wananchi (kumsafisha) kuhusu yeye.
Na akipitishwa na CCM, basi hapana Shaka CCM itakuwa imefanya dharau kubwa kwa wananchi wake.
Maana wenyewe walisema hafai, baadae wanakuja kuwaambia wananchi wao kuwa anafaa na kutaka kumpa nchi aongoze, BONGE LA DHARAU HILO. Na akipitishwa na CCM, halafu wananchi wakamchagua kushika madaraka, basi patakuwa hapana shaka yoyote tukiingizwa kwenye GUINESS BOOK.
Maana kitachotokea Tanzania, kwa nchi zilizo makini na wanachokifanya hakiwezi kutokea kamwe.