Kwa taarifa tu ni kwamba CHADEMA inajengwa zaidi na udhaifu wa CCM! Udhaifu wa CCM na kushindwa kutekeleza mambo ya msingi yanayowafanya watanzania waendelee kuwa masikini ndicho kinachoijenga CHADEMA. Sote tunalala gizani, sote tunakunywa maji ya tope, sote tunalala chini tukienda mahospitalini, sote tunasota na foleni Dar, sote tunaishi kwenye mitaa michafu yenye harufu kali ya uozo na makelele kila mahali. Tumekuwa kiishi hivi kwa miaka 50 iliyopita, na ninaweza kukuhakikishia kwamba kama CCM itachaguliwa tutaendelea kuishi katika hali hiyo. Si kwamba CCM haijafanya kitu, hapa ndipo mashabiki wa CCM wasipoelewa wanapokosolewa. Miaka 50 ni mingi sana katika kutatua matatizo ya msingi kama elimu, maji na afya. Kama asilimia zaidi ya 70 ya watanzania wanakunywa maji ya tope, kama asilimia zaidi ya 50 ya wanafunzi wanakaa mavumbini, kama asilimia zaidi ya 70 wanatumia vibatari kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru, je bado tuseme CCM imefanikiwa? Watanzania TUAMKE kutoka usingizini!