Lowassa jiangalie utakatwa na huko UKAWA kwa kujitangazia kugombea Urais 2020, kwani wengine hawapo?

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,650
“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.
****************************

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema njia ni nyeupe kwa Chadema kuingia Ikulu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.



“Kuweni watulivu na mwaka 2020 mjitokeze kupiga kura na kama nitakuwa hai nitakuwa mgombea tena wa urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani,” alisema.



Akizungumza nyumbani kwa kada wa Chadema, James Lembeli katika kijiji cha Mseki, Kahama, Lowassa (pichani) alisema ameshindwa kuzungumza na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho akihofia kukamatwa na polisi kama alivyokamatwa Geita na kuwataka wawe wavumilivu hadi uchaguzi wa mwaka 2020.



Kadhalika, Lowassa aliwataka vijana wasikubali kuibiwa kura kwa madai uchaguzi uliopita hawakutendewa haki na ndio maana walikosa ushindi.

*By Shija Felician, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz*

MY TAKE: Hivi kwanini Lowasa usisubiri mchakato ufike? Kwanini unajimilikisha ugombea urais? Utakatwa na huko CHADEMA.
 
Ila siasa za bongo pasua kichwa yaan mtu anajitangaza kugombea uraia kabla hata muda kufika? Sifahamu katiba ya chadema inasemaje kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais ila kwa style hii kwa sisi wapenda democracy inatutia mashaka
 
Sijaona kosa hapo, kama katiba ya Chadema haikatazi kujitangaza mapema basi ni haki yake. Cha msingi ni Chadema kuwa na utaratibu mzuri unaotowa haki kwa mwanachama yoyote mwenye sifa ya kugombea na mgombea ashinde kihalali, sio yale ya kunyanyua mkono juu, halafu kapita. NO
 
Chadomo ni chama mfu sasa hivi.

Nyong'o ya mamba imepasukia mtoni maji yote hayafai.

Wanao bweka wameficha mikia yao nyuma.

Network seach upinzani, siwezi kuwa rofaaaaaaaaaaaa daima.

Mjomba nae anapigilia msumali wa kichwa. Mungu akupe maisha marefu mjomba.

Matako ya sufulia hayaogopi moto... mmeshakuwa cha cha mafisadi, mnadaiwa mpaka rent.

Tumeshtuka bora turudi kwa baba na mama Chichiem oyeeeeeeeeeeeeee
 
Ukinunua nyumba yenye wapangaji...lazima wawe wapole na wafuate matakwa yako...la sivyo wahame...yeye kwa sasa ni mmiliki halali wa chadema hvo yeye ndo kusema...hutaki ondoka....' OVER
 
Lowasa ndiye mwenye chama ameweka zaidi ya billion 5 hapo na zitakwisha 2030 hivyo wakimkata patachimbika kabisa..............
 
Hakuna mtu wa kumkata Lowasa ndani ya Chadema, ndiyo maana ana jeuri ya kujitangaza wakati wowote.

JK aliwatupia zigo Chadema akaondoka zake sasa wanahangaika nalo.
 
Hakuna mtu wa kumkata Lowasa ndani ya Chadema, ndiyo maana ana jeuri ya kujitangaza wakati wowote.

JK aliwatupia zigo Chadema akaondoka zake sasa wanahangaika nalo.
Nikama mtu akususie jini unabaki unahangaika nalo. Nimekusoma mkuu, hahahahaaaa.
 
Back
Top Bottom