THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Katika hali ya kushangaza mbunge wa Monduli mh.Edward Lowassa ameingilia ratiba ya mikutano iliyopangwa kwa ajili ya kampeni za serikali za mitaa na kufanya mikutano ya chama chake maeneo ambayo CHADEMA ilipaswa ifanye mikutano.
Leo katika kijiji cha Losirwa kilichopo kata ya Eslalei vijana wa CHADEMA walishtushwa kuona CCM wakivamia na kuanza kufunga vyombo na vifaa vya kampeni kwenye eneo walilokuwa wakiliandaa kupigia kampeni kwa madai kwamba mbunge ndiye anayekuja kuhutubia huku wakijua fika kwamba ratiba haiwaruhusu.
Viongozi wa CHADEMA walipolifikisha suala hili kituo cha polisi Mto wa Mbu OCS wa kituo hicho alijaribu kuwasiliana na mtendaji wa kata na mtendaji wa kijiji ambao wote waligoma kutoa ushirikiano kwa madai kwamba wapo wilayani Monduli.Hata hivyo viongozi hao wa CHADEMA walishangazwa sana na kauli ya OCS huyo kwamba mbunge ana haki ya kufanya mikutano bila kujali ratiba.
Juzi pia mh. Lowassa aliingilia ratiba ya mkutano wa CHADEMA uliokuwa ufanyike Mto wa Mbu na hivyo CHADEMA kulazimika kutumia siku iliyofuata ambayo ilikuwa ndiyo ya CCM katika ratiba. Uongozi wa CHADEMA wilaya ya Monduli tayari umeshafikisha malalamiko katika ofisi ya mkuu wa wilaya leo kuonesha kutoridhishwa kwake na jinsi mbunge huyo anavyokandamiza demokrasia wilayani Monduli.
Mbunge huyo anahaha kukinusuru chama chake wilayani Monduli baada ya chama hicho kuzidiwa nguvu na CHADEMA wakati mbunge huyo alipokuwa nje ya nchi.
Wiki iliyopita pia uongozi wa CHADEMA wilaya ya Monduli uliiandikia ofisi ya mkuu wa wilaya barua inayoelezea njama na hujuma zinazopangwa juu ya viongozi na wagombea wa CHADEMA wakati huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa.