Lowassa asema jambo juu utendaji wa Rais Magufuli, asema kuna mazuri na mabaya kayafanya

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
ALICHOSEMA LOWASSA KUHUSU UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI HADI SASA

Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa Rais Dkt Magufuli alianza kwa kufanya kazi vizuri lakini licha ya kuwa amefanya baadhi nzuri, lakini bado kuna mengine mabaya aliyoyafanya.

Lowassa aliyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji wa Azam Tv aliyetaka kujua hadi hapa tulipofikia, ni mambo gani anayoweza kusema kuwa Rais Magufuli amefanya vizuri na yeye anajivunia hilo.
Lowassa alisema hawezi kukataa kuwa kuna mambo mazuri yamefanyika hadi sasa lakini kuna mengine mabaya pia.

Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, wakati unafagia uwanja, kuna wakati unaweza ukafagia shilingi katika ya uchafu, alisema Lowassa akijaribu kuelezea kauli yake kuwa wakati unafanya mambo mazuri, unaweza ukajikuta pia unafanya mengine mabaya.

Aidha, Lowassa aliwataka watanzania kutomhukumu Rais Magufuli sasa, bali wamuache na baada ya kipindi fulani ndipo wanaweza kufanya hivyo.

Itakumbukwa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, Lowassa alikuwa ndiye mpinzani mkubwa wa Rais Magufuli katika uchaguzi ambapo alikuwa akipeperesha bendera ya CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.
 
What a wise man Lowassa! Lowassa hana siasa za ajabu ajabu.

Lowssa hana siasa za kuchafuana, haamini katika kuchafuana, ndio maana pamoja na baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi kumchafua na kumkashfu hajawahi kuwajibu.
 
Ni bora huyo kasema ukweli maana hata mm nakubaliana nae. Kuna mazuri yamefanyika ila pia kuna mapungufu yanaonekana dhahiri. Sasa ni jukumu lao kuyafanyia kazi hayo mapungufu maana 2020 wapiga kura tutawauliza waliyoyaahidi kama wameyatekeza au la
 
mfalme anaependa misifa kwa sifa hizi atalewa na kulala usingizi wa pono kuja kushtuka UKAWA wanaongoza nchi
 
Back
Top Bottom