Lowassa aongoza kura za maoni ya urais

Lowassa aongoza kura za maoni ya urais

PHILIPP DONIE

Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
61
Reaction score
15
Shirika la New Deal Africa kupitia mtandao wake wa Easypolls.com wanaendesha utafiti (opinion poll) kwa wagombea Urais nchini Tanzania waliojitokeza hadi sasa ambao ni Edward Lowassa wa (CHADEMA /UKAWA) na John Magufuli (CCM).

Hadi leo asubuhi matokeo ya mtandao huo yanaonesha kuwa uchaguzi ungefanyika leo Lowassa angeshinda kwa 64%, na Magufuli angefuatia kwa 31%, huku 5% ya wapiga kura wakiwa hawajaamua wampigie nani kati ya Lowassa na Magufuli.

Bila shaka hawa ni wale wanaosubiri wagombea wa vyama vingine wajitokeze. Kwa maana hiyo ni kwamba wagombea watakaojitokeza kupitia ACT, TADEA, CHAUSTA, na vyama vingine watagawana 05% ya hao "undecided".#AmNotPolitician #AmNotJournalist#RoadToElections2015#PresidentialElectionTZ
 
Kwa maana hiyo ccm wanachezewa nusu uwanja ball possesion yao 31%. Hii inamaana hata goli la mkono haiwezekanI labda wacheze na refa AWAPE PENALT
 
Tuliwashauri CCM watupatie Lowassa ali tumpambanisha na DR. wetu wa ukweli wakagoma. Sasa hili la 25th October ndugu zangu si pambano bali tutakuwa tunapiga tu jalamba la kumwapisha Mzee.
 
Ccm wanahaha kila kona, wanawapoza wana nchi ila wananchi hawasikii
 
Kwa maana hiyo ccm wanachezewa nusu uwanja ball possesion yao 31%. Hii inamaana hata goli la mkono haiwezekanI labda wacheze na refa AWAPE PENALT
Sasa watapewaje penalty wakati hawafiki hata kwenye18 za wapinzani wao??
 
Kwa maana hiyo ccm wanachezewa nusu uwanja ball possesion yao 31%. Hii inamaana hata goli la mkono haiwezekanI labda wacheze na refa AWAPE PENALT

Huyo refa atakuwa kichaa mtu akwatuliwe katkat ya uwanja atowe penalty!!
 
Duh kweli mwamba wa kaskazini noma sana.Yaani anamiliki mchezo kwa asilimia 64. Ina maana Magufuli kazi yake kuzuia tu?
 
Easy polls: 14 August 2015

Lowassa: 77%

Magufuli: 22%


Jamii Forums: 14 August 2015

Lowassa 86%

Magufuli 13%....


Daaaaahh....!!!! Sina usemi...!!!!!
 
Ata wapewe awana mpiga penalty akipewa makufuli atapiga nnjee shigo ile imelala upande.
 
Lowassa ni Rais hamna namna nyingine!
 
Niliwahi kuandika humu ndani wiki moja iliyopita kwamba
Bila kujali Lowasa atasimamishwa Na ukawa au

Matokeo yatakaribiana kuwa sawa Na haya
Nilisema

Ukawa 63% CCM 37%
Nikasema vyama vingine vitachukua asilimia 5 ambayo sikujua itapungua

kutoka kwa Nani !kwa sababu sikufanya utafiti wa NamBa Bali Muono
 
Labda wazuie na maandamano ya kupiga kura

Ninadhani kutakuwa na shida uchaguzi mkuu,
1. Taarifa za kuhakiki kadi za wapiga kura wananchi wengi hawajui hili.
2. Sijajua waliofika na wakatambua kadi zao(majina yao hayapo) wanapaswa kufanya nini.

It is insane katika mitaa mitatu kupata watu tisa tu waliokuta majina yao katika uhakiki.

Uchaguzi mkuu HAUTAKUWA wa amani.
 
Ninadhani kutakuwa na shida uchaguzi mkuu,
1. Taarifa za kuhakiki kadi za wapiga kura wananchi wengi hawajui hili.
2. Sijajua waliofika na wakatambua kadi zao(majina yao hayapo) wanapaswa kufanya nini.

It is insane katika mitaa mitatu kupata watu tisa tu waliokuta majina yao katika uhakiki.

Uchaguzi mkuu HAUTAKUWA wa amani.

Nimepata taarifa za kuhakiki tarehe 10 na mwisho ilikua ni tarehe 11 na nilikua mbali na kata yangu.
Swali langu kwa Tume kama majina hayaonekani je hivi vitambulisho tumevipata wapi?
Wasitake kuleta sababu za kitoto ili kuleta machafuko, kwa upande wangu mimi jina langu liwepo au lisiwepo hakuna atakaenizuia kutimiza haki yangu ya kikatiba labda kadi yangu ipotee na hilo si rahisi kutokea kwani hua siitumii kwa matumizi tofauti na kupigia kura kwani baada ya kuandikishwa tu nimekitunza kama Dawa ( Hifadhi sehemu kavu chini ya nyuzi joto 30, Ikinge na mwanga, mwisho weka mbali na watoto )
 
Sasa utafiti gani huo?

Utafiti wa Lowassa v Magufuli ni sawa na mtu asema kwamba Utafiti niliofanya nimegundua kwamba Marekani ina uchumi mkubwa kulko Tanzania.

Kitu/jambo ambalo liko obvious unawezaje kuliita utafiti?!
 
Back
Top Bottom