Jana 29/10/14 Mhe. Lowassa aliingia Mwanza, na Fastjet ya saa 2:30 asubuhi. Akapokelewa na viongozi wa wilaya ya Ilemela akiwepo DC Mama Masenza. Akachukuliwa na gari la Idara ya Maji akifuatana na mpambe wake mkuu Ndg. Mgeja, mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga hadi hoteli ya Gold Crest, akapumzika na kuonana na mkuu wa mkoa wa Mwanza na wakuu wa wilaya za jirani kwa muda wa saa kama moja hivi na baadaye kuondoka kwenda jimbo kuu la Katoliki.
.