Judi wa Kishua
JF-Expert Member
- Apr 15, 2012
- 1,066
- 1,048
Chadema ilikuwa ni chama kinachopambana na kuchukia ufisadi kwa nguvu zote. Leo Chadema wamekuwa watetezi wakuu wa mafisadi. Leo hii kila anaeguswa Chadema watakuja kumtetea kwa visingizio kibao mara dagaa,au kafara au kwa kuwa rafiki wa lowassa (sio chadema) au wengine wanaconclude tu serikali inakurupuka. Ilimradi ni utetezi tu kwa mafisadi na watu wasiofata sheria na taratibu.
Nakumbuka kabla ya uchaguzi kilikuwa ni chama tahasisi na kilipinga sana dhana ya mtu mmoja kuwa mkubwa kuliko chama na kujikita kujenga chama. Zitto ni muhanga wa siasa za tahasisi against mtu, Zitto alipigwa vita mpaka kuondolewa chamani sababu kubwa alionekana anajijenga yeye na sio chama. Ili linajirudia kwa Lowassa, tofauti na Zitto kwa Lowassa linashangiliwa kwa nguvu zote.
Lowassa ameteka kila kitu chamani ameshajitangaza mgombea urais wa 2020 (hii ilimletea Zitto matatizo makubwa). Lowassa amesema atafukuza meya yoyote atakaezembea. Lowassa ndio anawapa seminar elekezi mameya.
Lowassa kaitisha kikao cha kuisuka upya Chadema, kikao kimefanyika Moshi (sio Mtwara, Musoma, Morogoro wala Mbeya mhhh! ). Tulizoea aya zamani yanafanywa na chama sio mtu mmoja tena asiye na nyadhifa yoyote kwenye chama.
Lowassa aka rais wa mioyo ya wanachadema, mpambanaji mpya wa wanachadema, jembe la wanachadema. Tunasubiri kuona bungeni namna chadema mpya ya Lowassa itakuwa inapigania maslahi ya nani? Watanzania wazalendo au mafisadi?
Chadema ya leo itathubutu kuwanyoosha kidole marafiki wa kweli wa Lowassa kina Rostam aziz?
Swali linabaki nani kambadilisha mwenzie kati ya Lowassa na Chadema?