Lowassa amkosoa Kikwete


kuandika hivi kunatokana na kula ukashiba kupitiliza bila kwenda darasani>Someni Ajenda ya kilimo kwanza muone.Sio chakula cha kula maana watanzania hakuna njaa kiasi hicho!
 
Wajemeni:

Kuna kitabu kinachoitwa The Elusive Quest for Growth by William Easterly. Ukisoma kitabu hiki utaona Lowassa anachemsha BIG TIME. Nchi za kiAfrika ikiwemo Tanzania zimeshainua literacy lakini bado maendeleo ya kiuchumi yapo nyuma.

Hivyo Education is not a panacea. Na ukiniuliza nichague kati ya Elimu na Kilimo nitachagua Kilimo. Na hii ni kwa sababu zifuatazo.
  • Hakuna mwanafunzi anayesoma akiwa na njaa. Tanzania ina upungufu mkubwa wa chakula lakini hivyo usitegemee wanafunzi wenye utapia mlo kuwa makini darasani.
  • Ukosefu wa chakula unaongea unwaranted inflation na matatizo mengine ya kiuchumi yasiotakiwa. Kama serikali inatumia fedha za kigeni kuangiza mchele au mahindi, basi inatumia pesa ambazo zingetumika kwa shughuli zingine za maendeleo.
  • Sekta ya elimu siku zote inaongeza matumizi na ukubwa wa serikali. Ukichikua mipango ya elimu ya Lowassa akiwa waziri mkuu utaona kuwa bajeti ya serikali iliongezeka na hakuna matunda yoyote ya muhimu kwa sababu bado kuna ukosefu mkubwa wa walimu. Kwa upande mwingine kilimo kwanza kinafanywa na watanzania bila kutegemea kulipwa mishahara na serikali. Hivyo kiuchumi sera za kilimo ni bora zaidi kwa sababu kutakuwa hakuna ongezeko la matumizi ya serikali yasiozaa matunda.
  • Vilevile idadi ya watu duniani inakuwa kubwa, hivyo shughuli za kilimo zinaanza kuwa na umuhimu mkubwa katika kutoa ajira.
  • N.k
Watanzania wakiwa na economic engines za kuleta mapato, watajijengea shule wenyewe.
 
huyu jamaa anatafuta mahali pa kuingizia kichwa tu. na akiingiza atoi hata upige ukunga. Na ndio utakua umepewa maumivu hivyo.
 
kuandika hivi kunatokana na kula ukashiba kupitiliza bila kwenda darasani>Someni Ajenda ya kilimo kwanza muone.Sio chakula cha kula maana watanzania hakuna njaa kiasi hicho!
Whaaaat? mshukuru Mungu kama unapaishi kuna chakula kaka.............. Nchi ina njaa kali hii.
 
Hapana jamii forum kweli naikubali!!!!!!!!!!!!!!!Nimecheka kwa kweli mpaka mtoto wangu ananiuliza mama mbona unalia??????????????

Hakikisha mtoto wako anashiba vizuri ili amsikilize mwalimu na akili na mwili vikue sawia usihadaike kuwa mtoto akisoma na njaa ndio anakuwa jiniasi
 
Lowasa alisema kama ni kilimo kwanza basi "Elimu kabla" na hii kauli amekuwa akiirudia mara kwa mara. Pamoja na mengine miaka miwili ya JK na Lowassa shule nyingi za kata zilijengwa na kulikuwa na presha sana kwa wakuu wa mikoa kujenga hizi shule. Tatizo kubwa la nchi hii hakuna dira ya taifa, kila kiongozi akiingia madarakani anaingia na agenda yake, na yale yaliyopita ya kiongozi kabla yake ndo yanakuwa kikomo.
 
hata kuoza kwa papai kunategemea sana uozaji wake,
kwa eneo hilo lowasa ameonesha kuwa yeye ni papai lililooza upande mmoja tu.
ni mawa yangu tu............teteteteteee!!!

HAPO Mh kanena, Elimu kwanza, kwani hata kama ni kuelimisha wananchi inaweza kutumika elimu ya watu wazima nchi nzima kuwaelimisha kuhusu kilimo kwanza jinsi ya kukabiliana na mkakati huo.

Hafu pia mi sioni tatizo la LOWASA kugombea Urais mwaka 2015, Anafaa jamani, UNAJUWA kama ana makosa hawezi kuyaendeleza akiwa rais.
 
Unajua huyu Lowassa anataka kuzuga watu wasioangalia vitu kiundani. Hakuna makosa kabisa kusema elimu ni muhimu, lakini tulipofikia TZ sasa hivi umaskini ndio ugonjwa mkubwa kuliko magonjwa yote. Tunao vijana wengi sana walioelimika lakini hawana ajira na umaskini unazidi kushamiri.

Kilimo kwanza ndani yake kuna mafunzo ya kutumia vifaa bora, mbegu bora, umwagiliaji na mambo megine mengi yanayoendana na masoko. Sasa hivi vyote ni rahisi kutumia mabwana shamba waliopo na hata vijana walimaliza form six kuwa trained kidogo waende uko vijijini kuwafundisha wakulima ili umaskini uondoke na uchumi ukue.

Sasa huyu kilaza Lowassa anangangania elimu kwanza, Je itachukua miaka mingapi kuwaelimisha watu zaidi?? around 10++
Kilimo kwanza matunda yake yanaweza kuonekana within 3 yrs kwa vipato vya wakulima kuongezeka, na hao wakulima kuweza kupeleka watoto wao shule na kulipa ada.

Tuna utitiri wa shule feki za kata, hizo shule bila wakulima kuwa na kipato hazitaweza kuendelea kwani huko vijijini watu wanalazimishwa kuchangia lakini hawana hela.

ALL in ALL KILIMO KWANZA kiwe ndio priority, na huku tukiendelea na Track iliyopo ya ELIMU.
 
Kuna shida gani kilimo na elimu kupewa msukumo kwa pamoja? Vyote si vipaumbele muhimu? Twahitaji elimu bora pamoja na kula vizuri. Huwezi kuwa na maisha mazuri without either.
 
Lowassa kumkosoa Rais Kikweye mbele ya kadamnasi, si dalili ya mtumwenye elimu na busara. Kama Lowassa anaamini kwamba Elimu ni lazima kwanza ndipo wananchi waweze kuongeza kilimo, basi hiyo elimu si kwa wakulima tu bali ni kwa watu wote wa sekta mbalimbali. lakini wakati mwingine itategemea ni elimu ya aina gani wananchi wapewe kama ni kuinua kilimo. Kuna elimu ya utapeli na kuna elimu ya maendeleo. Kwa mfano serikali iliyopita ya Kikwete, wengi walikuwa ni wenye elimu tena ya juu, hata yeye lowassa na wengine wengi. Je hiyo elimu waliyokuwa nayo ilililetea taifa maendeleo gani? Rushwa, ufisadi, wizi wa wazi n.k.. Mpaka leo haohao wenye elimu ndio waliiba pesa za wananchi za EPA, ndio walianzisha kampuni hewa ya Richmond n.k.
Mimi sidhani kitendo cha Lowassa kumkosoa Rais wake mbele za watu kilikuwa cha mtu msomi , ni unafiki tu wa kuficha madhambi yake yeye mwenyewe. Je huko Monduli kuna wakulima wasomi kama yeye? Hebu atupe takwimu za maendeleo yao kuhusu kilimo au mifugo. Weee Lowassa, acha laghai bwana.
 
huyu jamaa anatafuta mahali pa kuingizia kichwa tu. na akiingiza atoi hata upige ukunga. Na ndio utakua umepewa maumivu hivyo.

Hii ni kweli anatafuta mlango wa kuingilia na baada ya hapo kama hadithi ya mwarabu na ngamia.......................atawatolea wote nje ili kuhitimisha azma yake......................
 


kilimo kwanza maana yake nini? mtu anenda shamba hajui atalima vipi, atavuna vipi hana elimu yoyote unamwambia kilimo kwanza, SHAME! acha ushabiki wa kisiasa, zakuambiwa changanya na zako! KWA WENZETU mfano Israel not more than 5% wako katika kilimo wengine wote wanafanya shughuli nyingine za maendeleo, na hao wakulima wanazalisha kwaajili ya nchi yao na ku export, walianzia wapi, walipatiwa elimu kwanza jinsi ya kufanya kilimo chenye tija and the like, siyo mnasema kilimo kwanza mwanakijiji hajui A wala B kuhusu kilimo, mnapoteza nguvu kazi. get up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…