Lowassa aibuka na staili ya CHADEMA

Lowassa aibuka na staili ya CHADEMA

bhou

New Member
Joined
May 4, 2015
Posts
2
Reaction score
16
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameibuka na staili inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuendesha operesheni maalumu za kisiasa, safari hii vijana wanaojihusisha naye wakianzisha vuguvugu la kusaka Ikulu walilolitambulisha kwa jina la ‘4U Movement.

Vuguvugu hilo linafanana na vuguvugu la Chadema lililopachikwa jina la M4C. Hata hivyo, tofauti ni kwamba, wakati M4C ililenga kuiimarisha kisiasa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini, 4U Movement inalenga kumwezesha Lowassa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vijana hao wanaounda 4U Movement walikutana katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Januari 3, mwaka huu na kukubaliana, pamoja na mambo mengine, mbinu za kuhakikisha ushindi kwa Lowassa katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kisha dhidi ya vyama vya upinzani kwenye mpambano wa urais.

Katika kikao hicho, kiongozi wa 4U Movement, Hemed Ally, aliweka bayana utaratibu wa kufanya majadiliano kwa washiriki wote waliohudhuria na mada iliyojadiliwa ni changamoto na mbinu za kufikia watu wengi zaidi kuhakikisha ushindi wa Edward Lowassa unapatikana." Taarifa hizo za Hemed ni sehemu ya muhtasari wa kikao hicho unaopatikana kwenye mtandao wa kikundi hicho; 4U Movement | FRIENDS OF LOWASSA.

Katika kikao hicho cha Januari 3, washiriki walitakiwa pia kuunda makundi sita yenye watu 12 kila kundi kisha wajadili kwa muda usiopungua dakika 30 na mwisho kila kundi lilitoa mshiriki mmoja aliyewasilisha maoni ya kundi lao mbele ya washiriki wote waliohudhuria kikao hicho, baadaye walifikia makubaliano na kuazimia mambo kadhaa.

Miongoni mwa waliyoyaazimia ni pamoja na elimu itolewe juu ya 4U Movement na historia ya kiutendaji ya Lowassa ili iwe rahisi kueleza pindi mtu anapoulizwa swali, basi atoe majibu sahihi na yenye uhakika na zaidi ya hapo, iandaliwe (makala maalumu ya kieletroniki – documentary) itakayoonyeshwa kwa wananchi mijini na vijijini kwa kutumia ‘projectors'.

Washiriki wa mtandao huo walikubaliana kuanzisha kampeni waliyoipa jina la ‘Kurudisha kwa Jamii', kwa lengo la kutoa misaada kwa makundi mbalimbali ya jamii na makundi ya wahitaji.

"Ilikubaliwa utekelezaji wake (kampeni ya kurudisha kwa jamii) uanzie Hospitali ya Temeke ambapo tutaanza na wodi ya kina mama Jumapili Januari 11, 2015. Wajumbe na marafiki wote wa Lowassa watakaoguswa tutajumuika pamoja na chochote tulichonacho iwe sabuni, maji, juisi, matunda kwenda kuwafariji mama zetu ambao wamelazwa katika hospital hiyo," ilisema sehemu ya muhstari huo.

Pia walikubaliana kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na muda utakapofika wahamasishwe kupiga kura.

Wajumbe walikubaliana pia; "Kutanua mtandao wa mawasiliano, ili kuwafikia wengi zaidi hususan wale ambao hawana uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, whatsapp na mingine ya aina hiyo.

"Washiriki walisisitiza uwepo wa databases, uwepo wa mwakilishi kwa kila chuo atakayekuwa anawasilisha ripoti kwa wahusika, mada zijadiliwe ndani ya makundi ya whatsApp na kupunguza mizaha.

"Jinsi ya kupata kipato, washiriki walishauri kuwepo na ada ya usajili ya Sh. 5,000 kwa kila mwanachama wa 4U Movement na ilishauriwa mtandao uwe unafanya fundraising (harambee) kwa ajili ya kufanikisha kuwafikia watu wengi zaidi," ulifafanua muhstari huo wa kikao cha Karimjee.

Washiriki pia walipendekeza kuwe na wawakilishi wa mikoa ili kurahisisha mtiririko wa taarifa na kuwafikia watu wengi zaidi kupitia mgawanyiko huo wa kimajukumu.
Raia Tanzania lilimtafuta kiongozi wa mtandao huo kuhusu mipango hiyo ambaye katika majibu yake, alisema anachokifanya ni kuhamasisha wanachama wengi kujiunga na 4U Movement.

Alifafanua kuwa kundi hilo linaundwa na vijana bila kujali elimu yao, lakini pia kuna wazee waliokubali kuungana nao.

Juhudi za kumpata Lowassa kueleza kama anaufahamu mtandao huo hazikufanikiwa, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu hadi tunakwenda mitamboni.

Chanzo: Raia Tanzania
 
Ningefurahi kama wangeazimia kwamba lowasa awe anawapa fedha za kurudisha kwa jamii!.

Historia ya utendaji ya kutafutiza na kukaririsha watu ili wasikosee!!!!!!!!!!!!!!!!. Haiba ya kutafutiza!!!!!!!!!!!!!!!
Labda ili watu wasikosee kufikisha kwa watu habari hizi za mafanikio ya kutunga, wazuwie kusiwe na maswali ya papo kwa papo kwa sababu, mwisho ya uwongo, ni aibu na fedheha kubwa!.

BTW, tangu January, mbona kijijin kwetu hamjaja kurudisha kwenye jamii hizo sabuni na mafuta? Au ndivyo mnarudisha kwa kuwagawia Cc ya CCMACT, ili wavurugane mtengeneze cc yenu mpya?

KAKOBE ALISHASEMA. MANENO MENGINE YAKISEMWA HAYARUDI TUPU HADI YATIMIZE LENGO!. CCMACT MNAONA?

LA KUVUNDA .........
 
Anazidi kuwapa hofu ccm ili wasimkate jina lake kwenye mgombea wa uraisi lakini kifo cha nyani miti yote huteleza .
 
Wameanza kutoa form za kujiorodhesha..nimebahatika kuziona
 
you cannot fool all the people and all the time
 
This is the beginning of the end of CCM
 
captain bora ungetulia tu kulinda heshima lkn mambo yakienda tofauti tarajia aibu
 
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameibuka na staili inayotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuendesha operesheni maalumu za kisiasa, safari hii vijana wanaojihusisha naye wakianzisha vuguvugu la kusaka Ikulu walilolitambulisha kwa jina la ‘4U Movement.

Vuguvugu hilo linafanana na vuguvugu la Chadema lililopachikwa jina la M4C. Hata hivyo, tofauti ni kwamba, wakati M4C ililenga kuiimarisha kisiasa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini, 4U Movement inalenga kumwezesha Lowassa kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vijana hao wanaounda 4U Movement walikutana katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Januari 3, mwaka huu na kukubaliana, pamoja na mambo mengine, mbinu za kuhakikisha ushindi kwa Lowassa katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kisha dhidi ya vyama vya upinzani kwenye mpambano wa urais.

Katika kikao hicho, kiongozi wa 4U Movement, Hemed Ally, aliweka bayana utaratibu wa kufanya majadiliano kwa washiriki wote waliohudhuria na mada iliyojadiliwa ni changamoto na mbinu za kufikia watu wengi zaidi kuhakikisha ushindi wa Edward Lowassa unapatikana.” Taarifa hizo za Hemed ni sehemu ya muhtasari wa kikao hicho unaopatikana kwenye mtandao wa kikundi hicho; 4U Movement | FRIENDS OF LOWASSA.

Katika kikao hicho cha Januari 3, washiriki walitakiwa pia kuunda makundi sita yenye watu 12 kila kundi kisha wajadili kwa muda usiopungua dakika 30 na mwisho kila kundi lilitoa mshiriki mmoja aliyewasilisha maoni ya kundi lao mbele ya washiriki wote waliohudhuria kikao hicho, baadaye walifikia makubaliano na kuazimia mambo kadhaa.

Miongoni mwa waliyoyaazimia ni pamoja na elimu itolewe juu ya 4U Movement na historia ya kiutendaji ya Lowassa ili iwe rahisi kueleza pindi mtu anapoulizwa swali, basi atoe majibu sahihi na yenye uhakika na zaidi ya hapo, iandaliwe (makala maalumu ya kieletroniki – documentary) itakayoonyeshwa kwa wananchi mijini na vijijini kwa kutumia ‘projectors’.

Washiriki wa mtandao huo walikubaliana kuanzisha kampeni waliyoipa jina la ‘Kurudisha kwa Jamii’, kwa lengo la kutoa misaada kwa makundi mbalimbali ya jamii na makundi ya wahitaji.

“Ilikubaliwa utekelezaji wake (kampeni ya kurudisha kwa jamii) uanzie Hospitali ya Temeke ambapo tutaanza na wodi ya kina mama Jumapili Januari 11, 2015. Wajumbe na marafiki wote wa Lowassa watakaoguswa tutajumuika pamoja na chochote tulichonacho iwe sabuni, maji, juisi, matunda kwenda kuwafariji mama zetu ambao wamelazwa katika hospital hiyo,” ilisema sehemu ya muhstari huo.

Pia walikubaliana kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na muda utakapofika wahamasishwe kupiga kura.

Wajumbe walikubaliana pia; “Kutanua mtandao wa mawasiliano, ili kuwafikia wengi zaidi hususan wale ambao hawana uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, whatsapp na mingine ya aina hiyo.

“Washiriki walisisitiza uwepo wa databases, uwepo wa mwakilishi kwa kila chuo atakayekuwa anawasilisha ripoti kwa wahusika, mada zijadiliwe ndani ya makundi ya whatsApp na kupunguza mizaha.

“Jinsi ya kupata kipato, washiriki walishauri kuwepo na ada ya usajili ya Sh. 5,000 kwa kila mwanachama wa 4U Movement na ilishauriwa mtandao uwe unafanya fundraising (harambee) kwa ajili ya kufanikisha kuwafikia watu wengi zaidi,” ulifafanua muhstari huo wa kikao cha Karimjee.

Washiriki pia walipendekeza kuwe na wawakilishi wa mikoa ili kurahisisha mtiririko wa taarifa na kuwafikia watu wengi zaidi kupitia mgawanyiko huo wa kimajukumu.
Raia Tanzania lilimtafuta kiongozi wa mtandao huo kuhusu mipango hiyo ambaye katika majibu yake, alisema anachokifanya ni kuhamasisha wanachama wengi kujiunga na 4U Movement.

Alifafanua kuwa kundi hilo linaundwa na vijana bila kujali elimu yao, lakini pia kuna wazee waliokubali kuungana nao.

Juhudi za kumpata Lowassa kueleza kama anaufahamu mtandao huo hazikufanikiwa, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu hadi tunakwenda mitamboni.

Chanzo: Raia Tanzania

Sina comment ila nimekugongea like walau ihesabike una like mokja mazee bhou
 
Hivi huyu jamaa akiukosa urais nini kitatokea ?? binafsi nahofia atabasti moyo
 
Jipeni moyo mnaotamani akatwe na wote mnajulikana kama ilivyo siasa haina adui wa kuduma akiwa rais tutawakuta viti vya mbele ikulu. .
 
huyu mzee hajui kuwa simba mwendapole ndio mla nyama, tatizo lake ana haraka sana na kulazimisha mambo
 
Back
Top Bottom