Lowassa afunguka akiwa Dodoma

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956

Waziri Mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza wakati wa mahojiano na waandishi wa gazeti hili mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

“
KWA UFUPI
  • Yafuatayo ni mahojiano ya Mwananchi na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa. Hata hivyo Lowassa hakuwa tayari kuzungumzia masuala yanayohusu uchaguzi mkuu ujayo na mambo yanayohusiana na hilo kwa sababu anatumikia adhabu ya kusimamishwa mwaka moja na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Yafuatayo ni mahojiano ya Mwananchi na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa. Hata hivyo Lowassa hakuwa tayari kuzungumzia masuala yanayohusu uchaguzi mkuu ujayo na mambo yanayohusiana na hilo kwa sababu anatumikia adhabu ya kusimamishwa mwaka moja na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Swali: Umekuwa ukisema mara kwa mara kuwa tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kupasuka, je serikali ifanye nini kukabiliana na tatizo hilo?

Lowassa: Duniani kote vyama vya siasa vinapotaka kuingia madarakani huangalia masilahi ya watu, huangalia ni jambo gani la msingi ambalo chama kikiingia madarakani kitayafanya. Suala la ajira lipo karibu katika kila nchi, kila chama kinachoingia madarakani hulizungumza hilo.

Labda niseme mfano mmoja, Mwalimu (Julius) Nyerere alipokuwa anaanzisha elimu ya kujitegemea mwaka 1967 alikuwa anaangalia ajira. Aliangalia akaona hatuna viwanda, kwa hiyo elimu ikawa lazima iwe ya kujitegemea. Unamuandaa mwanafunzi kwa maisha ambayo yatamuajiri vijijini. Mwaka 1967, Mwalimu Nyerere alikuja na elimu ya kujitegemea, kwa hiyo ni lazima na sisi tuje na mawazo mapya ya ajira. Kwanza hakuna ubishi kwamba watu wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, vyuo, vyuo vikuu na kadhalika ni wengi sana. Watu wote hawa wanaangalia kwamba wanafanyiwa nini katika ajira.

Kwa hiyo mimi sisemi tu ni bomu, ila nasema ni bomu linalotarajia kulipuka wakati wowote. Lakini ni bomu ambalo tunahitaji kulishughulikia. Lengo langu la kupiga kelele ni kuitaka jamii ishughulikie jambo hili. Nashukuru nilipopiga kelele kidogo, wizara zilitoa takwimu na kila wizara ikatakiwa kuangalia kwenye eneo lake inatengeneza ajira kiasi gani, mimi nasema huo ndiyo mchakato.

Lakini kwa maoni yangu, ajira ya Tanzania lazima iangalie kwenye eneo kubwa la kilimo. Kilimo ndicho kinachochukua ajira ya watu wengi nchini. Lakini sasa tukiwapeleka vijana kwenye kilimo tutengeneze mazingira ya kumfanya mwanafunzi anayemaliza chuo kikuu awe tayari kuishi mazingira ya kilimo.

Nilipokuwa Waziri wa Maji nilitembelea Misri, kule mwanafunzi anapomaliza chuo kikuu anapelekwa Mto Nile anapewa ekari tatu za kulima mizabibu, anapewa trekta na vyombo vingine na anapewa mkopo ambao ataanza kuulipa baada ya miaka mitatu.

Pia tangu akiwa chuo, anajua ajira yake ni kilimo na kwamba atapewa mazingira ya kufanya kilimo; si cha jembe la mkono ila kilimo cha kisasa. Anakopeshwa na anawezeshwa. Kwa hiyo mimi nasema jambo moja kubwa sana la kufanya ni kuhakikisha tunawapeleka vijana kwenye kilimo, lakini kilimo chenye mabadiliko. Kilimo ambacho ni cha kisasa zaidi ambacho atakifurahia na ambacho kitamletea maisha bora katika maisha yake.

Eneo jingine mimi nadhani tungefanya uamuzi magumu ni kutenga maeneo tukapanda michikikichi (mawese), kama ilivyo Kigoma.

Tuchukue ekari kama milioni 10 tupande michikikichi, michikichi hii tuigawe. Kwa mfano tungeweza kufanya kazi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), iwe ni kuhakikisha wanaanzisha mashamba ya michikichi. Mkishaanzisha mashamba ya michikichi, mnawakabidhi vijana ambao hawana ajira waendelee na michikichi na baada ya miaka mitatu au minne watakuwa wamevuna, hali yao itakuwa nzuri na utakuwa na mafuta ya chakula nchini, tutakuwa na mafuta ya ku-export (kuuza nje) na utakuwa umetengeneza ajira kwa vijana wengi.

Vilevile la tatu ni eneo kubwa ambalo linategemewa na watu; ni viwanda. Na mtakumbuka wakati (Rais wa Marekani, Barack) Obama anagombea urais kwa mara ya pili wale wafanyakazi wa General Motors (kiwanda kikubwa cha magari Marekani) waliandika bango ‘You saved our jobs in September, this year we will save your job in November (Uliokoa ajira yetu Septemba nasi tutaokoa ajira yako Novemba) wakimkumbuka alivyofanya uamuzi ambao si wa kibepari; ulikuwa ni wa kijamaa, kwamba serikali inawekeza kwenye viwanda.

Kwa siasa za kibepari jambo hilo halipo, lakini serikali ililazimika kuwekeza kwenye viwanda ili ajira ziendelee na viwanda viendelee. Sasa mimi nasema tunaweza na sisi tukajenga viwanda makusudi vya nguo ambavyo vinachukua ajira ya watu wengi au viwanda vingine tutakavyoona vinafaa vinavyochukua ajira ya watu wengi. Naliweka suala hili hadharani tulijadili. Kwa sababu kama mabepari wanaendeleza sera za kijamaa kuokoa ajira zao na sisi tuendeleze sera hizohizo kuokoa ajira za watu wetu.
Utaniambia serikali itatoa wapi fedha? Jibu langu rahisi sana, tuna gesi Mungu ametubariki na sisi tuna gesi. Tuna uhakika wa kupata gesi trilioni 50 cubic metre. Unaweza kukopa kutokana na gesi uliyonayo ardhini. Unakopa fedha hizo unakwenda kuziwekeza kwenye miundombinu ya viwanda na sehemu nyingine ambazo zitaleta ajira. Tunaweza ni suala la uamuzi tu. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumetengeneza ajira nyingi za vijana.

Swali: Ulikuwa kinara wa uanzishwaji wa shule za kata. Je, unadhani mwelekeo uliokusudia ndiyo huo au una ushauri ambao unadhani kama ungezingatiwa elimu na miundombinu ya shule hizo ingekuwa bora zaidi?

Lowassa: Kwanza nakishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kunipa heshima ya kubeba bango la kutekeleza sera tuliyoiamua katika Ilani ya Uchaguzi kwa kujenga shule za sekondari za kata. Msingi wa uamuzi huu ni kujenga usawa katika jamii, shule za sekondari za kata, tuliazimia kwa misingi kwamba itajenga haki na usawa katika jamii ya Watanzania. Ukijenga shule kwenye Kata ya Moshi, wanakuwa na shule yao pale kwenye kata moja ya Moshi. Ni sawasawa na kata nyingine ya Masaini ambako wapo nyuma; kwenye kata ya Bukoba; ni sawasawa na kata nyingine ya Ugogoni iliyo nyuma sana.

Lakini kwa msingi huo wa shule kwenye kila kata, tunajenga usawa katika nchi kwamba kila kata ya nchi yetu ina shule ya sekondari ya kata. Mimi nadhani uamuzi ule ulikuwa ni wa maana sana. Huwa mimi ninapenda kusafiri kwa magari. Ninapopita saa 9:00 au saa 10:00, utakuta vijana kwa mamia wanatoka madarasani shuleni.

Jiulize, kama isingekuwa hizo shule za kata, vijana hawa wangekuwa wapi? Kwanza wangekuwa wameshakwenda kuolewa na kuzaa watoto, wengine wangekuwa wameshakuwa majambazi... kwa sababu hawakupewa fursa ...lakini vijana hawa ni wengi sana, mimi nashukuru kwamba shule hizi tulizisimamia na zikawa na majibu mazuri. Sehemu kubwa walijenga, nasikitika baada ya kuondoka uwaziri mkuu, kuna maeneo ambayo walilegeza masharti, walilegea kwa sababu walitegemea kusukumwasukumwa tena.

Wenzangu hawakuona sababu ya kuwasukuma sana, lakini kidogo wakapunguza mwendo. Lakini nafurahia hivi karibuni Rais ametoa tamko tena la kuwataka wasimamie maabara na ametoa masharti.

Kwa sababu ni kauli ya Rais, nadhani itatekelezwa na suala hili likipata msukumo nadhani itakuwa vizuri. Lakini nadhani bado nasema shule za kata zilikuwa za msingi na mtu ambaye anazibeza atakuwa na lake jambo. Kuna wengine waliziita ‘shule za fasta’, ‘voda fasta’, ‘shule fasta’, lakini mimi nadhani sasa wanaona yanayotokea ni kinyume chake na sasa wanatoka vijana waliosoma vizuri.

Tulikuwa na tatizo kubwa sana la walimu, lakini tulikuwa na mkakati wa kuzalisha walimu wa kutosha na mpaka mwaka huu shule zina walimu watano, kumi na kuna shule Dar es Salaam zina walimu 40.

Tatizo la walimu limeanza kuisha. Na mimi ninadhani tutakwenda taratibu na kama suala hili likiendelea kusimamiwa vizuri huu ni ukombozi mkubwa sana kwa Watanzania kwa sababu ni shule ambazo zinafika waliko tu. Lakini nimefurahi sana kwamba katika waliofanya vizuri ni kutoka shule za sekondari za kata… zimefanya vizuri sana katika matokeo ya mitihani kuliko ambavyo ilikuwa imetarajiwa kwa hiyo kumekuwapo na kulegeza kamba kidogo.

Hata hivyo naamini Rais akilisukuma kidogo kama alivyosukuma mwaka jana, tutafanikiwa kufika malengo. Lakini nasema ni uamuzi mzuri, uamuzi sahihi ambao umesaidia sana Watanzania walio wengi na imetusaidia kujenga usawa katika jamii yetu ya kutoa elimu. Hili ni jambo la msingi sana, la haki ya msingi ya binadamu ya kupata elimu. Tutafanikiwa kwa utaratibu huo.

Swali: Nini maoni yako kuhusu Kilimo Kwanza. Uliwahi kukaririwa ukisema Elimu Kwanza kabla ya kilimo. Unadhani ndiyo maana hadi sasa mkakati huo haujazaa matunda yaliyokusudiwa? Lowassa: Kwanza bahati mbaya sana, suala la elimu kwanza lililetwa baada ya kuanzishwa kwa shule za kata baada ya mimi kuondoka madarakani ndio ikaja elimu kwanza. Sikukubaliana na suala hilo na nikalisema kwenye Halmashauri Kuu ya chama changu kwamba mimi sioni busara za kusema Kilimo Kwanza kabla ya elimu, nikasema hata tutafute lugha gani ya kutafsiri, lakini tusipoangalia tutakuwa tunakosea.
Sioni tutaendeleaje na Kilimo Kwanza bila kuwa na elimu kwa hiyo nikashauri tubadilishe msamiati tuseme ‘elimu kabla, kilimo kwanza’, yaani preface (dibaji). Unapoandika kitabu unaandika preface elimu kabla ndio ifuate kilimo kwanza, lakini namba wani iwe ni elimu. Huwezi kumpata mkulima bora kama hana elimu. Huwezi kumpata mfugaji bora kama hana elimu, huwezi kumpata mvuvi bora kama hana elimu. Ukiwapa elimu hawa watakuwa wakulima bora, wafugaji bora na wavuvi bora. Lakini ukienda tu bila elimu ya msingi haiwezekani, utakuwa unapoteza muda wako.

Swali: Kuna madai kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kilijengwa kwa shinikizo la Serikali hususani wewe ulipokuwa Waziri Mkuu kwa kushinikiza wakuu wa mifuko ya jamii kuchangia.

Lowassa: Sikuwashinikiza nilitaka watumie busara zao tu. Ilikuwa hivi wakati ule Rais alifanya uamuzi kuwa tunajenga chuo kikuu cha Dodoma. Alikuwa ametoka Marekani yule tajiri mkubwa Bill Gate alikuwa amemuahidi angemjengea Centre of Excellence na Teknohama akamuahidi kwamba angejenga, lakini alipokwenda Marekani kwenye ziara aliporudi hakupata matumaini makubwa kama ilivyokuwa pale mwanzo kwa hiyo akanieleza tufanye jitihada ambazo tunaweza ili tujenge chuo kikuu kwa sababu tumeshawaahidi wananchi, kwa hiyo hatuna budi kujenga.

Kwa hiyo siku moja nikawaita wakuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Niliwaita katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma, tukazungumza, tulizungumza vizuri, lakini hatimaye niliwaambia kwamba tumepewa kazi na serikali ya kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Hatuna rasilimali wala fedha za kujengea, isipokuwa kuangalia hii mifuko ya jamii mnaweza kutusaidiaje? Kila mmoja akazungumza.

Wako waliokubali, wapo waliokataa. Wengi walikataa wakiniambia kwamba wamewekeza sana katika real estate (ujenzi wa nyumba) na pengine ni vizuri wakapunguza. Sikukubaliana na taarifa hizo kwa sababu nilikuwa najua kuwa wanawekeza kwenye majumba ya watu binafsi na mashirika ya umma. Hili kwangu mimi lilikuwa ni suala la kufa na kupona, ni uamuzi ya rais na tuna mahitaji ya wanafunzi kusoma.

Dunia yote watu wanaosoma wapo vyuo vikuu, sisi tuna population (idadi ya watu) inayokua kiasi hicho, tusipoongeza vyuo vikuu itakuwa taabu sana. Kwa hiyo nikawasikiliza nikawaambia, nimewasikiliza lakini sikubaliani nanyi. Nikawaambia huyu hapa vice chancellor (makamu mkuu wa chuo).

Nikawaambia huyu ndio Vice Chancellor. Huyu bwana anajua eneo lote ambalo tunataka kujenga chuo kikuu nendeni naye, kila mmoja atamuonyesha mlima (eneo) wake. Angalia mlima wako, chaguo mlima wako, fikiria, halafu tukutane kesho asubuhi.

Yule ambaye anataka kujenga tutaingia naye mkataba, yule ambaye hayupo tayari kujenga aje na barua yake ya kuacha kazi na kuchukua dhamana ya kukubali kujiuzulu kwake. Wote wakakubali na chuo kikajengwa.

Tumejenga kuliko uwezo na naambiwa sasa hivi kuna majengo yapo wazi.Tunajifunza nini, kwamba tuna uwezo wa kufanya vitu katika nchi yetu. Tukiamua kufanyia uamuzi, tunaweza kufanya makubwa zaidi.

Swali: Kuna wanaodai hiyo ndiyo sababu ya mifuko hiyo kuyumba kutokana na serikali kutolipa madeni?

Lowassa: Sijasikia kama mifuko inayumba. Swali:Wako wanaosema hilo lilikuwa ni wazo la kimapinduzi. Nini maoni yako?
Lowassa: Nakubali kuwa ni kweli lilikuwa wazo la kimapinduzi.

Swali: Wakati ukiwa Waziri wa Maji ulinukuliwa ukisema eneo lote la Kanda ya Ziwa na Kati litapata maji kutoka Ziwa Victoria na ulitekeleza hilo katika maeneo ya Shinyanya na Kahama, lakini baada ya kuondoka mradi ule umekufa. Unadhani tatizo ni nini hasa?

Lowassa: Kwanza si kweli kwamba ule mradi umekufa. Nimesikia bungeni wakieleza kwamba wameendeleza mpaka Tabora na Igunga, kwa hiyo nashukuru Mungu kwamba mradi ule unakwenda vizuri, bado upo na haujafa.

Labda niseme tu kwamba kwa miaka mingi tangu tupate uhuru, kumekuwa na jitihada za serikali za kutafuta maji yale ya Ziwa Victoria yatumiwe na wananchi walio karibu na ziwa hilo, lakini kwa miaka mingi tangu tupate uhuru jambo hilo halikuwezekana kwa sababu mkataba uliokuwepo ambao uliwapendelea Misri na Sudan na kwamba nchi zilizopo kusini mwa maji haya yaani Ziwa Victoria, zikitaka kutumia maji haya, lazima ziombe kibali Misri na Sudan.

Jambo hili ndiyo lilifanya serikali ya Tanzania kwa miaka mingi sana ikashindwa kupata maji haya. Wakati nikiwa Waziri wa Maji, Rais (Benjamin) Mkapa chini ya uongozi wake na nimewahi kusema mtu wa kushukuriwa kwenye suala hili la maji ya Ziwa Victoria ni Rais Mkapa.

Mimi nilikuwa mtekelezaji tu wa Rais Mkapa. Lakini mtu aliyefanya uamuzi na kunipa nguvu ya kwenda kutekeleza ni Rais Mkapa. Tulizungumza akaniambia kama tunaweza kufanya tufanye, kutakuwa na mambo ya kidiplomasia ila tutayashughulikia. Kwa hiyo tukakubaliana.

Namshukuru Mungu tuliusimamia vizuri utaratibu ule na maji yakaenda mpaka Shinyanga, Nzega, Kahama, sasa yanaelekea Igunga na Tabora. Ni Jambo zuri, namshukuru Mungu kwamba jambo ambalo lilikuwa limezuiwa kwa siku nyingi, lilifanikiwa.

Swali: Tangu enzi za awamu ya kwanza, umekuwa ukihusishwa na utajiri. Dhana au madai haya yana ukweli kiasi gani?

Lowassa: Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa.

Wakati huo kama sijaondoka nafasi ya uwaziri mkuu walileta shutuma kuna maduka fulani wakasema ya Lowassa tu haya. Kwenye familia tuna kampuni ya Alphatel ya kufua, kuna mtu mmoja mwenye asili ya Asia alijenga jengo kubwa kule Kinondoni limeandikwa Alpha, ikaonekana ni jengo langu.

Kule Mbezi kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa, yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza, mimi sina nyumba maeneo hayo. Kwa hiyo wamesema uwongo mwingi sana. Mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki zangu nyingine. Swali: Unaweza kututajia mali zako kubwa unazomiliki zinazoonekana?
Lowassa: Mimi ni mfugaji, nina ng’ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli.

Swali: Kumekuwa na maneno kutoka kwa baadhi ya watu kuhusu afya yako na hilo limekuwa likitumiwa na baadhi ya mahasimu wako kisiasa. Unalizungumziaje suala hilo?

Lowassa: Hilo ni kama lile la utajiri, watu wanapenda kunitakia afya mbaya. Kwani wewe unaionaje? Wanatunga tu naumwa, nikifanya mazoezi nikapungua kidogo wanasema huyu amepata stroke (kiharusi) amepelekwa Ujerumani. Lakini nataka nikuhakikishie kuwa afya yangu ni nzuri sana. Namshukuru Mwenyenzi Mungu ambaye ananipigania afya yangu.

Swali: Umekuwa ukionekana kwa TB Joshua Nigeria, wewe ni muumini wake?

Lowassa: Kila mtu ana uhuru wa kuamini na kushirikiana na imani anayofikiri inafaa. Namuona TB Joshua kama muumini na mwombaji mzuri ninayekubaliana naye katika vitu vingi, kwa hiyo nasikia faraja kwenda kwa TB Joshua na ninataka kuwahimiza watu wanaotaka kwenda, waende. Ni muombaji mzuri sana.

Swali: Ni jambo gani kubwa katika maisha yako ambalo unadhani utakumbukwa nalo daima?

Lowassa: Jambo la kukumbukwa nitawaachia Watanzania wanaonikumbuka waamue wenyewe.

Swali: Ni jambo gani katika maisha limewahi kukufurahisha zaidi?

Lowassa: Kwamba ninaishi, na kwamba Mungu amenikirimu sana katika uhai wangu

Swali: Ni jambo gani ambalo limewahi kukuhuzunisha zaidi?

Lowassa: Ni siku mama yangu alipofariki mwaka 1994. Nilimkosa mtu muhimu sana katika maisha yangu. Alinipenda sana, nami nilimpenda sana. Wakati huo nilikuwa mbunge na Waziri wa Mazingira. Swali: Simba na Yanga wewe timu gani
Lowassa: Si yoyote na ninazitakia zote kila la kheri.

Swali: Kombe la Dunia sijui kama unaangalia?

Lowassa: Ninangalia lakini sitaki kutabiri. chanzo.http://www.mwananchi.co.tz/habari/h...24700/2371774/-/item/5/-/12a5dig/-/index.html




 
Lowasa ninavyomjua huwa ni mwerevu sana katika kauli zake..
tB joshua hata Mwigulo aliwahi kwenda anyway sio ishu sana.... Bado Lowassa Ni scientific katika majibu
 
Aliwaita ili mmhoji au ndio kupaishana, ulishawahi kumhoji mwizi akakubali kuwa ni mwizi. Hebu tuendelee na juhudi za ukombozi wa taifa hili, mengine ni ngonjera zisizo na maana yoyote
 
Miongoni mwa viongozi binafsi nawaamini
.Lowwasa ni kiongozi mtulivu asiyepemda kuropoka

Lowasa ninavyomjua huwa ni mwerevu sana katika kauli zake..
tB joshua hata Mwigulo aliwahi kwenda anyway sio ishu sana.... Bado Lowassa Ni scientific katika majibu

Jamaa ni mjanja sana inaopnekana hapendi kuzi watu, kila kitu tunachoamini alifanya yeye au bila yeye kisingewezekana, amekuwa akiwapa sifa wenzie mfano maji na mkapa, pia shula za kata kaipa sifa kamati kuu ya ccm.
angekuwa mwingine angeropoka na kuponda sana watu waliopo sasa kuwa wameshindwa.
 
Lowasa ni mnafiki..amekuwa kiongozi wa serikali wizara mbali mbali je ina maana hakuliona hili tatizo la ajira kwa vijana mpaka ameamua kugombea urais?
LOWASA AACHE INAFIKI, UONGO NA UZANDIKI.
KWA KIFUPI HADANGA NYIKI MTU..magamba ni majanga.
 
Lowasa ni mnafiki..amekuwa kiongozi wa serikali wizara mbali mbali je ina maana hakuliona hili tatizo la ajira kwa vijana mpaka ameamua kugombea urais?
LOWASA AACHE INAFIKI, UONGO NA UZANDIKI.
KWA KIFUPI HADANGA NYIKI MTU..magamba ni majanga.

asiye mnafiki nani nitajie tafadhali
 
Ni aibu sana kwa chombo kikubwa kama Mwananchi kutumika kwa aina hii. Kwanza majibu na maswali yameandaliwa kwa kila hali KUTIMIZA malengo ya wahusika. Pili chombo kama Mwananchi hakiwezi kuambiwa eti utajiri wake ni ng'ombe tu na wao wasihoji mambo ya wazi ambayo uki Google unapata maswali ya kumtaka anafafanue Alphatel, Barare na Integrated kwa uchache ambayo kuna documents hata hapa JF https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/110957-lowassa-ni-msafi-lakini-kuna-kitu-hiki-5.html ambazo angezitolea ufafanuzi. Chombo makini Kama MCL chini ya Nation Group hapana!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/110957-lowassa-ni-msafi-lakini-kuna-kitu-hiki-5.html
 

Hahaa! Kawapa sifa wengine baada ya kusema a alifanya yeye na bila yeye yasingewezekana. Yote ni sanaa tupu na wewe umenasa
 
 
He is indeed a presidential material ... Vitu alivyovifanya ni tangibles viko wazi! Faida inaonekana wazi! Amenifurahisha sana alivyoweza kucheza na Miuungu watu waliko NSSF, PPF et al! Huyu ndo kiongozi mwenye maamuzi magumu! TOR yake anaisimamia na kuitekeleza kwa gharama yoyote ile! Hoja ya UFISADI ameweza kuipangua kwa style ya aina yake! Yeye si Mbadhirifu na anajua kutengeneza utajiri kupitia kipato chake! Wale wenye kuiba na kuficha kwenye kisiwa cha Jersy na Uswis wangetakiwa waige mfano wa Lowassa kwa kuzalisha ajira nchini... So far ukitoa Salim, Warioba sijaona mwenye afadhali ndani ya CCM zaidi ya Lowassa....Natamani wamnyime ili CCM ipasuke vipande vipande ....
 

we ulitaka nani ahojiwe?

Gongo ni hatari kwa afya
 
Pole sana. Majibu mepesi kwa hoja nzito. sikusema asihojiwe. Nimeweka mambo ya kuulizwa kwa chombo makini. Ushabiki hausaidii nchi hii. Kama anafaa amalize hoja za Barare, Alphatel na Integrated soma link hapo juu. KAMA Gongo itasababisha mtu akumbuke link basi Dk. Slaa alikua sahihi kutaka ihalalishwe ila kama ndio inapofua watu wajibu bila kusoma haifai KABISA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…