Lowassa: Acha wafu wazikane wenyewe, wametunyima uwanja lakini Majengo kumenoga zaidi

Akiwa leo viwanja vya makumbusho Mh Edward Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Chadema amesema hayo pamoja na kwamba wametunyima uwanja lakini hapa majengo kumenoga zaidi na kusema kwamba
"waache wafu wazikane wenyewe....."
Lowassa bana!anajua vizuri kiswahilli?hiyo kauli kaitoa msibani akiwa anazika maana yake amejiambia mwenyewe!
 
baruti 1 mbegu ya chuki iliyopandikizwa ni fimbo ya kujichapa wenyewe. Chuki baina ya vyama na vyama imeongezeka ndani ya chama tawala ni mbaya zaidi kila mtu ameamua kunyamaza kimya maji yafuate mkondo ili asije kubeba lawama ya mwenzie. Ila Mungu anajibu siyo mbali tutajutia mbegu hii ya yenye sumu kali tunayo ipalilia!
 
Wala haina maana yeyote mbaya in short alitaka kusema pamependeza zaidi kuliko ilivyodhaniwa.Mnaleta makelele utadhani mko Bunge la Porojo.
Huyo.Mwenyewe anaemkosoa anajua kiswahili vema?.Au matumizi ya neno kunoga ndiyo.Issue?
 
Akiwa leo viwanja vya makumbusho Mh Edward Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Chadema amesema hayo pamoja na kwamba wametunyima uwanja lakini hapa majengo kumenoga zaidi na kusema kwamba
"waache wafu wazikane wenyewe....."
Kwahiyo wao ni wafu?....khaaaaaa
 
Huyu Lowasa anafikiria bado anakubalika mbele ya Magufuli? Naona anaota ndoto za mchana eti 2020 saa 2 asubuhi amechukua nchi. Labda achukue Monduli na wapuuzi wengine waliopungukiwa na nywele. Kwa kigezo kipi cha yeye kupewa nchi wakati ameshiriki kutufikisha katika shida ambazo Magufuli anapambana nazo hivi sasa?
 
Back
Top Bottom