Lowassa aanza kuvuna jiji la Arusha

amina ngalo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
309
170
Radio 5 inayomilikiwa na waziri mkuu wazamani aliyejiuzulu kwa kashifa ya Richmond kwa mara yakwanza ndiyo imeanza kula matunda ya umeya wa jiji la Arusha

Mh Raisi magufuli iangalie upya halmashaur ya jiji la Arusha kuna majipu pale

TAARIFA KWA UMMA.

Kituo cha Radio 5 Arusha kitarusha live mkutano wa Baraza la Madiwani; Halmashauri ya Jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 07/05/2016.

Wananchi wote mnashauriwa kufuatilia kwa karibu mijadala itakayokuwa inaendelea kwenye Baraza moja kwa moja kupitia Radio 5 au kufika Halmashauri ya Jiji la Arush siku hiyo Baraza la Madiwani linapokaa.

Hii ni kwa mara ya kwanza katika Historia y Jiji kwa Mkutano wa Baraza kurushwa moja kwa moja na kituo cha redio ili kuweka uwazi wa mijadala katika vikao vya Halmashauri na kuwafanya Wananchi kufuatilia kwa karibu sana namna Wawakilishi wao wanavyo wasilisha hoja za maeneo wanayotoka kwa ufanisi.

Mwisho, ninawaomba Wananchi wa Jiji la Arusha mzidi kutuunga mkono katika jitihada na harakati za kuleta maendeleo kwa Jamii.

Ahsante,

Imetolewa;

OFISI YA MSTAHIKI MEYA,
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
S.L.P 3013,
ARUSHA-TANZANIA
 
umbeya, na wivu, kama bunge wanajifungia, kwa nini chadema Arusha wasionyeshe mfano wa uwazi kwa wananchi wao?

Maccm mtakufa na roho mbaya zenu, kuwanyima wananchi kujua wa wakilishi wao wanafanya nini, na kujua bajeti mnawanyima, halafu wenzenu wakionyesha njia ya uwazi, mnalialia?

Bg up Arusha. Chadema waonyesheni njia ccm kwamba kuwatumika wananchi siyo siri.
 
Back
Top Bottom