Danny greeny
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 3,856
- 1,647
Na Saed Kubenea, Mwanahalisi toleo la 277.
Je, Lowassa anaamini anachokisema? Anastahili kueneza anachokihubiri? Kama haamini anachokisema na anahubiri asichostahili kuhubiri, nini kimemsukuma kueleza haya sasa?
Kwanza, Lowassa haamini kwenye kujitolea “nguvu kazi.” Ndiyo maana kila anakopita, hakuna ambako aliweka nguvu kazi yake. Hakuna alikotoa jasho lake. Bali kote alikopita, kuanzia mkoani Singida, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Kigoma, Lowassa amemwaga fedha, badala ya kujitolea nguvu kazi.
Pili,Lowassa anajua sababu za wananchi kupoteza uzalendo na kutaka kulipwa ujira kwa kazi wanayoifanya. Ni kwa sababu, wamechoshwa na vitendo vya viongozi wao waliowapa dhamana.
Kwa mfano, baraza la mawaziri liliagiza mkataba kati ya serikali na makampuni ya Richmond/Dowans uwe wa mwaka mmoja. Lakini baadhi ya viongozi, Lowassa akiwa miongoni mwao, walibadilisha maelekezo ya baraza la mawaziri na kuliamuru Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO), kujifunga kwenye mkataba wa miaka miwili.
Aidha, kwa kisingizio cha nchi kutaka kuingia gizani, Lowassa aliamuru kubadilishwa kwa vigezo vya utoaji wa zabuni kutoka 24 vilivyowekwa awali hadi vinne ili kuweza kuibeba Richmond.
Pale alipoona Richmond imeshindwa kukidhi hata kigezo kimoja kutoka miongoni mwa vigezo vinne vipya vilivyowekwa, kikiwamo kile kinachoweka sharti la kampuni kuwa na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika miradi ya umme, aliamuru kazi ya kutafuta mzabuni ifanywe na kamati ya serikali, badala ya Bodi ya Tenda ya TANESCO.
Mbali na hayo, Lowassa anafahamu thamani halisi ya mitambo ya Richmond/Dowans; si zaidi ya dola za Marekani 40 milioni. Lakini kwa makusudi alikubali serikali kujifunga kwenye mkataba unaowalazimisha kuilipa kampuni hiyo, kwa kila siku, kama malipo ya kuweka mitambo – Capacity Charge – dola za Marekani 100,000; karibu Sh. 152 milioni.
Chanzo: http://mwanahalisi.co.tz/lowassa_anajua_uzalendo_au_ni_%E2%80%98machozi_ya_mamba%E2%80%99