Sassebossa
Member
- Jan 13, 2013
- 27
- 3
Wanajamvi,
Leo nataka niwajadili viongozi wawili shupavu,wenye muono wasio na masikhara katika utendaji kazi wao!!
Kwanza ni mh. Edward Lowasa,mbunge wa Monduli na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Mzee huyu pamoja na kuhusishwa na scandle ya Richmond,bado anaonekana ndani ya CCM huyu ndiye angalau anaweza kupambana na mikikimikiki ya Urais. Kimsingi mpaka leo huwa najiuliza ni kwa nini vyama vya upinzani vilishadidia sakata la Richmond kwa Lowasa badala ya Kikwete mwenyewe! Ni nani asiyejua uhusika wa JK ktk Richmond?
Watanzania tuwe makini! Lowasa anakumbukwa kwa ushupavu wake ktk uongozi wake. Tumuunge mkono mzee wetu!
ZITTO KABWE: Kijana huyu hodari wa kufukunyua uozo na muonesha njia ya mabadiliko ktk uongozi,amekuwa muhanga wa siasa za udini na ukabila tangu alipotaka kugombea uenyekiti ndani ya chama chake cha CHADEMA. Kimsingi,kijana anauwezo wa hali ya juu sana wa kuliongoza taifa hili. Tofauti na katibu mkuu wake(SLAA) mwenye exposure ya kidini kwa kiasi kikubwa,ZITTO ZUBERI KABWE ni hodari katika mambo mbalimbali huku akitumia ujana wake kwenda nje kujifunza namna viongozi wa nchi mbalimbali walivyopambana kukwamua nchi zao ktk umasikini.
Kijana huyu,kama katiba ikimuruhusu,CHADEMA msitunyime haki watanzania ya kupata Rais ambaye sasa ndo mkombozi wetu!
Nahitimisha kwa kusema,kama Chadema wataendekeza ukabila wakati katiba imemruhusu ZITTO,na wakati huo huo CCM wakakumbuka kumkabidhi Lowasa bendera ya kijani,kwa mara ya kwanza CCM itachukua kura yangu.