Lowasa anafanana na Wafuasi wake!

Lowasa anafanana na Wafuasi wake!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,837
Kweli ndio maana wazungu walisema ,,birds of a feather flock together " ukimuangalia fisadi Lowasa na wafuasi wake wanaojiita ukawa wote tabia zao zinarandana, wote ni watu waliopoteza uhalisia, kwa mfano fisadi Lowasa alinukuliwa akisema kwamba hakuna wakumkata CCM akakatwa, alisema hawezi hama CCM isipokuwa wao (sijui wao ni akina nani) ndiyo watahama, lkn matokeo yake alihama , akasema akienda ukawa ataondoka na Wabunge 150 ktk CCM ameondoka hakuna aliyemfwata isipokuwa makapi yaliyotemwa na CCM, haya sasa hivi anasema atashinda asubuhi na mapema wakati tafiti za kitaalamu zinaonyesha kwamba kama uchaguzi ukifanyika leo hii ataambulia kwenye kama asilimi 20% hivi hilo nalo kama vile wafuasi wake analikataa anasema wamemfiksi na kwamba tusubiri oktoba 25!

Sasa kwenye uchaguzi pia atapigwa mbaya na WatanZania tena itakuwa chini ya hiyo asilimia 20% na baada ya hapo atakuja na singo nyingine tena sasa sijui itakuwa ni ipi kwa maana SADC, AU, EU & Co. wote watasema uchaguzi ulikuwa wa salama na wa haki, sasa sijui nani hata atamsikiliza tena!
 
...

....Masasi Leo Hiii Lowasaaaaaaaa!!!

12006095_760412324102644_2875703010076251645_n.jpg
 
Alafu hiyo tafiti ya twaweza imesema kama uchaguzi utafanyika leo, ikumbukwe sasa hivi ndio Loasa yuko kwenye peak yake lwa kuwa na wafuasi 'wengi'.
 
Yule anaepiga push - up Kwenye majukwaa badala ya kumwaga sera atakuwa board guard wa Lowasa. Hata jamii inaona kazi inayomfaa ni uboardguard!
 
Sikatai,mimi nafanana na Lowassa kwa maamuzi magumu,busara na uvumilivu.
Kwanini nisimpende?Kura yangu na niliowashawishi ni zake.
 
Subirini matokeo mtajiharishia, mbona alipokua ccm mnyapara alisema lowasa ni safi? Kinana nae alisema lowasa safi? Amekua fisadi alipohama au sizitaki mbichi hizi?
 
Wasiwasi wangu lowassa atasema ameibiwa Kura.sijuwi itakuwaje atajuwa mwenyewe lakini akitaka asubiri mpaka 2025.
 
Katika siku ambazo magufuli kajichoresha basi ni leo katika ubaunsa wake wa kupiga push ups.Lakini anaweza kuwa bodyguard mzuri wa Edo.
 
Hahah huna hata aibu mmeanza push up...mtakoma mwaka huu
 
Wafuasi wa lowassa ni wanaume wa shoka na wasomi....twaweza
 
Sikatai,mimi nafanana na Lowassa kwa maamuzi magumu,busara na uvumilivu.
Kwanini nisimpende?Kura yangu na niliowashawishi ni zake.

Asante Nifah kwa mahaba yako kwa huyu kiumbe mstaarabu Mr Edo Ngoyai Lowassa.La Prezda
 
haaa haa lowasa alikuwa safi alivyokuwa ccm leo yuko upinzani ni mbaya.duh siasa za majitaka hizi ni hatarsana..
 
Back
Top Bottom