Njoo monduli jionee mwenyewe kazi nzuri iliyotukuka ya Mhe EL Raisi mtarajiwa, then compare to mtama
Mbushunoti ni vizuri tu ukaeleza machache tukafahamu.
Binafsi sipingi kama kuna kitu cha wazi alichopigania kwaajili ya wapiga kura wake wa Monduli. Kwa kifupi tu Lowasa tangu ajiuzulu uwaziri mkuu alibaki bubu bungeni kwa miaka takriban 8, sasa sijui ni wapi aliyasemea mahitaji ya watu wake, walau kwa ndani ya miaka hii 8, bila hata kurudi nyuma sana.
Ninachofahamu ni mali zake binafsi: mahoteli ya kifahari, majumba ya kifahari, na biashara mbalimbali kuanzia Mondoli juu hadi kwingineko.
Kama Mbunge wa Monduli, tukisimamia ukweli nina mashaka kama kuna kitu wapiga kura wake watajivunia nayo, ingawa kwa bahati mbaya kwa miaka yote hawakuona mwingine aliye afadhali.
Monduli naifahamu kwa kiasi kikubwa, japo sio kila kijiji. Naifahamu pia kuwa ni baadhi ya wilaya katika mkoa wa Arusha ambazo watu wake wanaishi kwa dhiki na umaskini wa kutupwa. Ikulu aende tu, sina shida naye. Ila ninachojua ni kuwa hakuna kipya atakacholeta Tanzania, kama ambavyo hakuna kipya alichofanya kwa watu wa Monduli.
Jambo lingine ni Lowasa wa zamani sio wa sasa. Lowasa wa zamani walau alikuwa na nguvu na afya. Ila Lowasa wa sasa amechoka kimwili, japo nia yake ya kwenda Ikulu ni ile ile. Namtakia kila la heri.