''''''Love vs Racism'''''

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Wakati nikifikiria namna ya kumaliza tatizo langu na mama wa rafiki yangu kipenzi nimekutana na kisanga kingine cha kusikitisha lakini kujifunza pia

Lakini hii sio yangu ila ni ya jamaa ambae ni fundi mzuri sana wa ngua a.k.a fundi cherehani

Huyu jamaa bana kiukweli ni fundi mzuri sana wa nguo za kawaida lakini pia ni fundi mzuri sana wa nguo za watu wenye asili ya Asia almaarufu kama Wahindi au "Wadosi"

Huyu jamaa yangu alikuwa nasifika sana kwa hao watu kwa ujuzi wake wa kuzishona hizo nguo hadi wakawa wanamuambia kuwa atakuwa ni mhindi mweusi

Alikuwa anapata "oda" nyingi sana ya kushona nguo hizo na alikuwa anajipatia kipato cha kutosha.Kama mjuavyo kwenye muingiliano wa kikazi na maisha hutokeza mambo mengi sana na moja ya mambo hayo ni mapenzi na hili limeleta faida kwa wengi na hasara kwa wengi,kwa huyu jamaa yangu sijui niseme ni hasara au faida,sijui

Jamaa yangu huyu ambae suruali yangu ilikuwa ikichanika yeye ndie aliyekuwa ananishonea[maana maisha magumu suruwali siku hizi ina bei ya mbuzi...lol] alijikuta akijiingiza kwenye mahusiano na binti wa Kihindi ambae walidumu kwa muda wa miezi 6 kabla ya zahma kutokea

Mahusiano yao yalianza pale ambapo binti alimueleza wazi kuwa amevutiwa na jamaa na jamaa aliona hiyo kama ni bahati ya pekee na walianza mahusiano yao mara moja

Ilikuwa ni juzi[kwa mujibu wa maelezo ya jamaa yangu] usiku majira kama ya saa 1:30 jamaa yangu alipopeleka nguo ya mama wa mpenziwe baada ya kuimaliza kuishona na mama huyo alihitaji kuivaa kwenye tukio la harusi ja jamaa wa familia hiyo,fundi alipoifikisha nguo na "mama mkwe" wake kuijaribu na kumuenea fundi alilipwa hela na kuanza kuondoka na kabla hajavuka "geti" lanyumba hiyo maeneo ya mwanga hafifu alikuja mpenziwe na kumuaga kwadeep kiss huku akiamini haonekani,kumbe mama mdogo wake na binti alikuwa amesimama jirani kabisa na eneo walilokuwepo wahusika kwani alikuwa ndio amekuja tu kwaajili ya kuzungumzia maandalizi ya mwisho mwisho ya harusi ambayo fundi alikuwa amepeleka ngu husika

Mama mdogo aliwaona na kila walichokifanya kilionekana na mama mdogo

Binti alimaliza kumuaga mpenziwe na kurudi nyumbani,mama mdogo nae alirudi ndani na kisha kuwaita wazazi wa binti na kuanza kueleza kila alichokiona,binti alipigwa na butwaa,alipoulizwa alikana lakini baada ya kutishiwa kupewa kibano alisema ukweli na usiku huo huo walimwambia binti awaambie mahali mhusika anaishi

Binti kwa kubanwa na baba yake na kaka yake aliwapeleka hadi jamaa alipokuwa anaishi na walipofika walimkuta jamaa ndio nae anafika,bila kuuliza kaka wa binti yule alifika na kuanza kumshambulia fundi lakini fundi alijitetea na kufanikiwa kujiondoa mikononi mwa "shemejie" huyo na kusogea pembeni

Wote mama.baba,mama mdogo na kaka wa binti walianza kumtusi kwa maneno ya mkibaguzi yule fundi na huku binti akiwa analia tu bila kuongea chochote na baada ya kutoa matusi walimgeukia binti na kumwambia amefanya kosa sana kuitia nuksi familia kwa kufanya ngono na 'uchafu" yaani mtu mweusi na adhabu yake ni kwenda kusafishwa,sijui huko kusafishwa ni kufanywa nini maana binti alikuwa anaambiwa kwa kihindi[binti ndie aliyetafsiri maneno hayo kwa fundi]

Baadae walimuahidi jamaa kumuadhibu vikali kwa kuichafua familia yao kisha waliondoka

Walipofika nyumbani binti aliadhibiwa sana na aliambiwa ni lazima apelekwe India na kukaa huko hadi atakapopata mchumba maana hiyo ni laana kwao,aliambiwa kuwa mipango ya safari hiyo itafanywa kesho yake yaani jana na leo ilikuwa asafiri

Asubuhi sana jana binti alitoroka na kwenda kwa fundi na kumueleza kuwa anahisi kuwa walichopanga kumfanyia sio kizuri na yeye anampenda jamaa na hayuko tayari kumuacha na hatorudi tena nyumbani kwao kwakuwa akirudi watamtenganisha na fundi na yeye hayuko tayari hilo litokee

Binti alikuwa ametoroka na kiasi cha fedha ambacho jamaa bado hajajua ni shilingi ngapi na binti alimuahidi waondoke waende wakaanzishe maisha mengine,fundi bado ana wasiwsasi sana kuishi na huyo binti na hivi sasa wapo mafichoni huku fundi akijiuliza kama afuate ushauri wa mpenzie ama laa

Fundi anaogopa kwa kuwa binti amemuambia kuwa kama atafanikiwa kuolewa nae nyumbani kwao binti watamfuta kwenye familia na watamuhesabu kama amekufa kwa kuwa hawatakuwa tayari kurudi kuishi nae tena kwa kuwa atakuwa amechafuliwa vya kutosha

Jamaa amekosa kabisa kujiamini kwa sababu kwanza anatafutwa na hao wazazi wa binti lakini pia yupo na binti ambae hajaridhia kabisa kuishi nae na zaidi sana wanaishi maisha ya kujificha jificha na pia hawezi kumfukuza huyo binti kwakuwa anaona yeye ndie aliyemsababishia yaliyompata

Jamaa anajuta sana kujiingiza kwenye mahusiano na huyo binti kwani anaona kama maisha yake yamevurugika na jamaa zake wamemwambia kuwa anatafutwa sana ni bora akajiondokea na kupotea kabisa mjini

Kwa muda huu jamaa ambae amenipa kisa hiki anasema kuwa jamaa hapatikani tena kwenye simu na hajui kama tayari amekamatwa au ndo hivyo katokomea

Maisha haya yanaweza kukuingiza kwenye mitihani ambayo inatakiwa ujasiri mkubwa ili kuivuka,kama jamaa huyu ananisikia ni bora awe jasiri na akubali kuishi na huyo dada na kama anaweza asikimbie apambane nao kwani sidhani kama wanaweza kufanya chochote kile kwani hawa watu sio watu wa "shughuli",au kama anaogopa aondoke na binti akaanzishe maisha mahali pengine,kwani nini bana?

Lakini kumkimbia huyo binti atakuwa amekosea sana

UKIPENDA VITAMU UKUBALI NA WAKATI VITAKAPOBADILIKA KUWA VICHUNGU NA UVUMILIE HADI VITAKAPOKUWA VITAMU TENA

Mapenzi yanaposhindana na ubaguzi wa rangi,kaazi kweli kweli!!!!!!!!!

W/end njema!!
 
Wahindi gani hao walokua hawajastaarabika?

Dada anaonekana kapenda maana wahindi wana true love...sijui kapewa nini lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Wahindi gani hao walokua hawajastaarabika?

Dada anaonekana kapenda maana wahindi wana true love...sijui kapewa nini lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Wahindi wanatuita watu weusi "kaliya" sina hakika kama inaandikwa hivyo kwa kihindi lakini inamaana kuwa ni kama jitu au likitu flan hivi jeusi lisilokuwa na akili

Unalijua hilo?

Unajua kuwa ubaguzi hauwezi kuisha hadi kiama?
 
Wahindi wabaguzi sana....Mbona wakati wanashona nguo kwa huyo fundi hawakuona kama anawachafua..?Hapo jamaa akatoe taarifa polisi..
 
hawa maponjoro dada zetu wanawafukua vilivyo wala hatuongei, sisi tukigusa wao eti tunawachafua. Huyu jamaa achague kuish na huyo mwanamke ama la! Hawez amkimbie, anaweza basi akomae
 
Wahindi wanatuita watu weusi "kaliya" sina hakika kama inaandikwa hivyo kwa kihindi lakini inamaana kuwa ni kama jitu au likitu flan hivi jeusi lisilokuwa na akili

Unalijua hilo?

Unajua kuwa ubaguzi hauwezi kuisha hadi kiama?

Me najua watu weusi wanawaita golo....
 
Hakuna watu wabaguzi wa ngozi nyeusi katika dunia hii kama watu wa bara la Asia...

Wahindi pia wana kasumba ya kuishi kimatabaka, familia maskini haiwezi kujumuika na familia ya kitajiri...

Kwa watu waliokuwa wanafuatilia tamthiliya ya " India A Love Story" almaaruf kama Tikhe wanaweza kukumbuka visa vya mapenzi vs ubaguzi mule ndani...
 
Tena uwe dini tofauti ndo uchafu unaongezeka.Jamaa kama anampenda binti amuoe tu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Jamaa akomae na toto la kikuch kuch hilo kwani walipokuwa wanapeleka nguo kushona si alikuwa anawapima kwa kuwashika makalio na matit hapo hawakuona huo uchafu binti ameongeza kidogo tu kwamba yeye ameshikwa akiwa hana nguo,ampe mimba fasta maana maisha ya wazaz yameisha saiz ni zamu ya binti ilitakiwa wabaki kuwa washauri tu huku wakishuhudia binti yao anavyolicheza sebene la maisha
 
Mimi siwezi muoa wala kutembea na muhindi. Mimi ni bora kwa rangi yangu kuliko wao.
 
Racism ni state of mind....kukataliwa kutoka na binti yao ni haki kama ilivyo kwa wachaga kukataa wahaya etc.....ubaguzi upo kila sehemu kila kona....huyo binti amepata tu mihemko kwakuwa bado hajapata mchumbwa wa kihindi...sidhani kama ni sahihi kumshauri jamaa amuoe hasa katika hali hiyo....ataweza kumuimbia kuch kuch hotae, yelarkihee...divaniii..divanaa...kila siku:music:

kula rotii na pariki....lol...binti afuate matakwa ya familia tu....jamaa atoe ripoti polisi kutishiwa maisha...wadosi wanaogopa polisi sana...watamwabie yaishe....
 
binafsi nina mpenzi mzungu lakin mambo kama hayo huwa yapo.sema inatakiwa unakuwa mguu ndan mguu nje.ubaguz upo.nashaur jamaa aachane nae
 
Jamaa yako yuko katikati ya mtihani akimuacha atakua kafanya vibaya sana na pengine bidada akajiua si unajua hawa watu huwa wepesi kujiua . Akiendelea kuishi nae huyo binti wazazi na ukoo wake wote watam-disown. Sasa kazi kwake mwenzake ame-sacrifice mpaka ukoo na huo ndio upendo wa kweli ameacha yote kwa ajili yake.
 
Mie nakubaliana nawe. Jamaa aonyeshe msimamo na kuendelea mapenzi na huyu binti haitakuwa rahisi lakini inawezekana. Binti kamzimia kwa mapenzi ya kweli na si kwa kuwa na bank account iliyoshiba hadi kumwagika kule bank. Siku hizi ni nadra sana kuona mapenzi ya namna hii.

 
^^
Eiyer
Hakuna ubaguzi mbaya kama unaohusisha mapenzi. Na hili unaloeleza halikuanza leo, upo ubaguzi wa mapenzi katika rangi, kabila, kiwango cha uchumi na mengine.
Kipimo cha penzi la kweli ni uwezo wa kustahimili magumu. Hao ni wakati wao wa kujisimamia.
^^
 
Last edited by a moderator:

Ubaguzi ni dhambi mbaya sana!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…