Lori la mafuta lagonga treni na kulipuka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lori la mafuta lagonga treni na kulipuka.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nazjaz, Apr 11, 2011.

 1. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Lori la mafuta lililokuwa likitokea Dsm limegonga kichwa cha treni wilani Manyoni mkoani Singida na kisha kupinduka.
  Baada ya kupinduka wananchi wakafika eneo la tukio na kuanza kuchota mafuta.
  Mmoja kati ya wananchi hao akafungua betri na ndipo moto mkubwa ukalipuka.
  Zaidi ya watu 11 wamejeruhiwa vibaya sana na moto huo na wamelazwa katika hospitali ya wilaya.
  Source: Radio One Breaking News
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Dah! Sasa sijui hawa wanajua kuwa kuna mchakato wa Katiba Mpya unaendelea? Maana vifo vya "kuchota" mafuta vimetokea mara nyingi, lakini bado ni wembe ule ule!!
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Kuna wale walipukutika kijiji kizima kule Mbeya. Lile lilikuwa ni fundisho tosha.
   
 4. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani hizi ajali za mwaka huu mbona zinatisha sana kila siku ajali na watu wanafariki na wengine wanapata majeraha ya maisha. Kwanini tusichukue hatua madhubuni ya kuzuia jhizi ajali za kila siku. Mimi siamini ajali hazina kinga maana kwanini kila siku zitupate sisi tu na si nchi zilizoendelea inamaana wao wanalinda vipi...? Gari haipinduki yenyewe bila kuwa na sababu za uzembe wowote ikiwepo mwendo kasi uzembe wa dereva, tairi kupasuka uzembe wa tajiri kutokununua tairi kwa muda muafaka na kufanya service na uzembe mwingine mwingi ukiwepo ulevi, kuendesha kwa leseni faki rushwa kwa askari usalama nk. Tuamke tuchukue hatua la sivyo tutakwisha sisi na familia zetu
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Rushwa inapukutisha taifa letu. Wasimamia sheria ndio wavunjaji wakubwa wa sheria hizo.
   
 6. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa Radio One Breaking News watu 3 wamepoteza maisha hapo mhapo na 11 kulazwa hospitalini.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mafuta hayaibiwi pamoja na kiberiti au betri...kukosa elimu na gharama zake!! Poleni wafiwa wote
   
 8. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  Mamlaka ya Mapato TRA na Mamlaka ya Leseni wamekuja na mkakati wa kudhibiti utoaji wa leseni mpya. Kigezo kilikuwa madereva kupitia vyuo vinavyotambulika lakini kinachotokea ni aibu, maana mahesabu ya haraka zaidi ya 50% zimetoka kwa rushwa pamoja na vyeti bandia. By the way, tumedharau suala la elimu (ya udereva pamoja na formal) lakini ina uhusiano mkubwa sana na ajali zinazotokea na hata ukisikiliza maelezo ya ajali zote hizi utaona hilo. TUMEFIKA PABAYA!!!!
   
 9. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  WATU wanne wamekufa na wengine 41 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mafuta pamoja na treni katika tukio lililotokea leo asubuhi mkoani Singida.Kwa mujibu wa mashuhuda wetu ajali hiyo imetokea baada ya lori hilo kuigonga treni iliyokuwa ikielekea stesheni ya Manyoni Singida na kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi wengine 41 wakiwamo askari 11 waliokuwa wakitoa msaada.

  Imedaiwa kuwa baada ya lori hilo kuigonga treni ghafla ilianza kuwaka moto uliosababisha majeruhi hao ambao walikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

  Hata hivyo, baada ya lori hilo kuigonga treni hiyo lilimwagika mafuta ambapo wananchi walianza kuzoa kwa kutumia ndoo na madumu.

  Kutokana na tukio hilo, polisi walilazimika kuweka ulinzi wa kutosha lakini, hata hivyo, walizidiwa nguvu na kusababisha wengine kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya miili yao.

  Kamanda wa Polisi mkoani huo, Celina Kaluba, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa kamili zitatolewa baadaye leo.

  Maiti na majeruhi walipelekwa hospitali ya wilaya


  source: Dar leo/ Redio one
   
 10. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Imethibitishwa Polisi wawili wameuawa baada ya kuzidiwa na nguvu ya wananchi
   
Loading...