Looking for "Ethical Job"

Looking for "Ethical Job"

nzovwe

Senior Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
118
Reaction score
31
A man with 27 years of age, graduated in 2012 (BSc. Agricultural Economics and Agribusiness) is looking for a job, currently, the man located at Dodoma region, anybody with any need at anywhere with this man just send me a "PM". Guys nice to hear more from you! (A man is single with permanent home place settled in MBEYA region). Actually the man has no any experience lather than data collections in two different research institutions settled in TZ +255(0) 688 459 988)
 
With that grammar, any serious & needy employer will refrain from contacting you. I'm getting suspicious of your bachelor.
 
Haya sasa msomi kashavunja "yai" to the best of his knowledge, waajiri mpoooooooooo?
 
Is English your tenth language ?

Sio kazi zote zinahitaji lugha za kigeni, hata cha kuombea maji kinatosha.., sasa sababu "Clothes makes a Pirate" andika tu kwa kiswahili utaeleweka kuliko kuandika lugha ambayo umeikosea hii inaweza ikasababisha muajiri akaogopa kukuajiri akidhani na mengine utakosea wakati kumbe kwenye field yako upo vizuri..

Alafu unamaanisha nini unaposema Ethical Job
 
Wala isikupeshida Mheshimiwa!, hata kiswahili chenyewe sio kirahisi km unavyohisi. Lugha zetu za ujanani zimetuharibu. Nilikuwa namaanisha hivi:Mtu mzima mwenye umri wa miaka 27 akiwa na akili timamu anatafuta kazi, kazi ambayo ina maadili mema ya kitanzania (kwa hapa Tanzania kuna kazi zingine zina masharti magumu sana yasiyo na utu).

Kama umeweza kunielewa, Ubarikiwe sana!. Mm nmechezea sana lugha kama hizi "Ch[SUB]3[/SUB]Ch[SUB]2[/SUB]Ch[SUB]2[/SUB]cl"
 
hahahaa!!! kumbe kiingereza sio mchezo

Please wait.................................................................................................................,

Kiingereza ni lugha ya kigeni, hapa Tanzania tunakalili tu, pia katika kukalili wengine wana vichwa vibovu ingekuwa calculations sawa. So! usishangae sana maana kila mmoja na upungufu wake. "Kwani ww kiingereza umezaliwa nacho au umefundishwa tu?"
 
Kwangu mimi sio tatizo ninajua kwamba kuna skills tofauti katika kazi tofauti na huenda wewe kazi unayofanya haiitaji lugha lakini mimi sio kila mtu.., wengine wanaangalia hata appearance; kumbuka pia kuna stereotypes kwahio usimpe mtu chance ya kuku-judge kabla hata haujaitwa kwenye interview (sio vizuri kuonyesha weaknesses zozote) kwahio huenda ungeandika hapo juu kama ulivyoandika hapa chini watu tusingekuwa tunaongelea hapa lugha, na watu wangekuelewa unataka nini na sio kuku-misinterpret; kwa ushauri kama bado unataka kazi achana na huu uzi (umeshachafuka) fungua mwingine ambao utaelezea vizuri ueleweke (hata kama kiswahili kinakupa shida muulize hapo jirani yako akusaidie)
 
a man with 27 years of age
#just send me a pm
kimekushinda nini kuandika kwaa kiswahili

Usemi wako Nimeupokea kama ushauri, kwahiyo asnante kwa ushauri wako siku nyingine nitatumia kiswahili. Kama hujaelewa hiyo kauli: nilitaka nimaanishe kwamba "mtu mwenye umri wa miaka 27", "anayenihitaji maana sio lazima, anitumie ujumbe kwenye kibox cha ujumbe wa siri (private message)"
 
With that grammar, any serious & needy employer will refrain from contacting you. I'm getting suspicious of your bachelor.

Sijasomea syntax n.k , sema tu ktk maandishi tupo tofauti. Cha msingi km kweli umeielewa hiyo sentensi na ungekuwa na uhitaji naamini ww ungekuwa mtu wa kwanza kunitafuta lakini nadhani huna uhitaji na mm ndio maana. Anyway, Asante kwa kuniweka attention!!
 
Haya sasa msomi kashavunja "yai" to the best of his knowledge, waajiri mpoooooooooo?

Mwajiri ni mtu yeyote tu, unaweza ukawa ni wewe, mimi, yule. Lakini hiyo siyo best knowledge yangu. Km unadhani unaweza ukafanya "perfect" kila mahali endelea kukashfu mali ya umma. Mtu yupo serious anatafuta kazi haya makosa yapo hata iweje, hata ww hujakamilika ndg yangu
 
Kwangu mimi sio tatizo ninajua kwamba kuna skills tofauti katika kazi tofauti na huenda wewe kazi unayofanya haiitaji lugha lakini mimi sio kila mtu.., wengine wanaangalia hata appearance; kumbuka pia kuna stereotypes kwahio usimpe mtu chance ya kuku-judge kabla hata haujaitwa kwenye interview (sio vizuri kuonyesha weaknesses zozote) kwahio huenda ungeandika hapo juu kama ulivyoandika hapa chini watu tusingekuwa tunaongelea hapa lugha, na watu wangekuelewa unataka nini na sio kuku-misinterpret; kwa ushauri kama bado unataka kazi achana na huu uzi (umeshachafuka) fungua mwingine ambao utaelezea vizuri ueleweke (hata kama kiswahili kinakupa shida muulize hapo jirani yako akusaidie)

weakness huwa zipo, mm naamini km mtu kweli yupo serious na ana uelewa km huo wa kwako ataweza kunitafuta tu, kazi inatafutwa maelezo yanaweza kukupa picha ya mtu anaetafuta kazi haina haja ya kurudia kuandika. Naamini imeeleweka japo kwa shida,
 
Kuna jambo moja kubwa sana ambalo naona haujaligundua..., wewe kama mtafuta kazi ni bidhaa (product) na muajiri ni mnunuzi (customer) kwahio wewe kama product you need to sell yourself..., ni sawa sawa wewe unauza nyanya alafu kwenye meza unapanga nyanya mbovu mbovu wakati kwenye tenga unaacha nzuri, ukijifariji kwamba kuna waelewa ambao watajua kwenye tenga kuna nzima..., mwisho wa siku unakosa fursa za wateja unajikuta hata zile nzima za kwenye tenga nazo zinaoza
 
Usitumie kusoma Sayansi kama kisingizio cha kuandika lugha mbovu, kwani hyo bachelor yako programs zake zilikuwa zinaendeshwa kwa kichina? Na unadai unazo research reports 2, uliandika Kilatini? Sayansi sio tiketi ya kutojua kiingereza, mbona tunawaona kina Prof. Sarungi na Magembe wanafanya presentation za kimataifa kwa kiingereza fasaha kabisa? Angekuja mwanasheria hapa akaandika lugha tusiyoielewa tungeweza kumuelewa coz wale wanatumia kiingereza tofauti kidogo na taaluma zingine na nyakati zingine misemo mingi ya kilatini..
 
Please wait.................................................................................................................,

Kiingereza ni lugha ya kigeni, hapa Tanzania tunakalili tu, pia katika kukalili wengine wana vichwa vibovu ingekuwa calculations sawa. So! usishangae sana maana kila mmoja na upungufu wake. "Kwani ww kiingereza umezaliwa nacho au umefundishwa tu?"

mimi huwa nakoseaga kiswahili tuu ambacho nimezaliwa nacho
 
haaaaaah! mimi simcheki mtoa mada ila wale wanaomkashifu na kumhukumu kwa yeye kutokujua kuandika kiingereza lakini tutambue kuwa tunamdhihaki mwenzetu aliyejiamini na kuandika kile kitu kwa jinsi anavyokijua yeye sasa ndugu zangu wanaojua kiingereza cha kuandika hapo jamaa kawafikisha mtakosoa mpaka January wakati cha kuongea huwezi kusimama hata dakika tano haaaaaa.
 
Back
Top Bottom