makondekoujiji
JF-Expert Member
- Aug 31, 2015
- 384
- 500
Dah humu kuna watu wakongwe ila tukiangalia I'd zao tunaweza dhani ni vijana wenzetu lol!Shikamoo Mzee.Unanikumbusha mbali sana mkuu.
Hiyo picha ya kwanza ni miaka ya 1960. Enzi hizo fasheni yetu ilikuwa suruali za kubana sana kama za vijana wa leo - hiyo aliovaa huhu bwana. Elvis Presley alikuwa ndio habari ya mjini na twist ndio dansi lenyewe. George Mukabi, Edward Masengo, Mwenda Jean Bosco, Frank na dadazake, Salim Abdallah ndio walikuwa wakali wa muziki wa dansi Afrika Mashariki.
Sasa kuhusu hizi suruali za kubana hawa vijana wa siku hizi wana bahati sana. Siku hizo waziri mkuu alikuwa mzee Kawawa. Alitoa amri kuwa tusivae tena hizi suruali za kubana na yeyote ataekutwa amevaa kipimo kilikuwa kupitisha chupa ya soda. Kama chupa haikuweza kuporomoka kutoka kiunoni mpaka chini miguuni hiyo suruali ilitiwa mkasi. Lakini sasa mabebi ndio walikuwa wanatufukuzilia sisi wenye suruali hizo - Ee bwana we, patashika gani hiyo mitaani.
Sasa ikaja miaka ya 70. Hapo tukiwa vyuoni tulitilia hizi bell-bottom (picha ya pili). Staili hiyo nayo ilivuma kipindi kirefu huku tukivaa viatu vya gorofa. Watu wengi waliteguka miguu kwa viatu hivi vikiitwa raizoni (raised-on shoes).
Ushauri: Fasheni ikipitwa na muda usiitupe. Iweke na mjukuu wako anaweza kuja kuitumia kama fasheni mpya kwao.
Asante kwa kunipa fursa ya time-travel back to the past.
cha baba? Havikua vya kike kweli hivyo?
View attachment 307860
vyote ni vya kiume mkuu sema ni matoleo tofauti tu
View attachment 307861
inasemekana kua wanaume ndio walikua wakwanza kabisa kuvaa high hills shoes kabla ya wanawake japo leo hii wanawake ndio wanaotumia zaidi aina hii ya viatu ( raised on shoes)
duh! Mkuu una miaka mingapi kwasasa? Maana umechimbua vitu ambavyo hata sivijui. Kumbe humu kuna baba zetu eeh
Dah humu kuna watu wakongwe ila tukiangalia I'd zao tunaweza dhani ni vijana wenzetu lol!Shikamoo Mzee.
Alikuwa anatumia hayo Zaman kipindi hicho mshua ni Mkuu wa district
View attachment 307860
vyote ni vya kiume mkuu sema ni matoleo tofauti tu
View attachment 307861
inasemekana kua wanaume ndio walikua wakwanza kabisa kuvaa high hills shoes kabla ya wanawake japo leo hii wanawake ndio wanaotumia zaidi aina hii ya viatu ( raised on shoes)
inabidi tuheshimiane humu kwa umri
Eee, tuseme tu nilikuwepo tangu enzi ya mkoloni.
Enzi hizo kichwani 'Afro' la nguvu
likichanuwa watoto watashoboka mtaa mzima.
Mbali ya shati la ndege
la kubana, kulikua na mashati ya mchelemchele pia kulikukwa na yale
mashati ya vitambaa vya mpira a.k.a.
no smoking, yaliyokuwa yakishonwa
'slim fit' mengine yakiachiwa
kuchanuwa huku mikononi.
Enzi hizo
mabuga/mapekos yalikuwa na stlye
fulani ya kusukwa sehemu za kwenye
mifuko hususan miwili ya mbele.
Hapo mtu bukheri kwenda kucheza
'Kamanyola bila jasho' na "masantula
ngoma ya mpwita'.....
miaka ya 81 maeneo ya magomeni tumeshapendeza yaani hakuna mtoto anayekukataa ukiwa umepiga raizoni yako na kichwani una bonge la afro
ha ha ha ha kwa kweli 'Old is
Gold'
duh! Mkuu una miaka mingapi kwasasa? Maana umechimbua vitu ambavyo hata sivijui. Kumbe humu kuna baba zetu eeh
Mkuu ulikipata wapi kiatu changu? :smiling: Nilikuwa na kama hicho chajuu, exactly.
cha baba? Havikua vya kike kweli hivyo?
Nakumbuka hiki kiatu cha baba
yaan uwepo wako hapa na jinsi ulivyoelezea hayo mambo umenikumbusha mbali sana. Nyinyi wazee mliokulia kipind cha ukolon mnakuwa na ubabe wa kikolon kweli.
Watu mmekula chumvi humu jf. Shikamoo babuUnanikumbusha mbali sana mkuu.