Mwishoni mwa wiki iliyopita Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa alijichukulia hatua mikononi na kwenda kulisawazisha eneo la jeshi pale Kawe Posta ili kuwapa unafuu wakazi wanaokatisha eneo hilo kuja Kawe ama kwenda Mbezi.
Lakini kitendo hicho kilichotafsiriwa na wengi kama mchakato wake wa kutafuta tena kura kutoka kwa wananchi wa kata hiyo kilileta tafrani baada ya unafuu baada ya wanajeshi kulizingira tingatinga la manispaa hiyo kwa kuingia na katika eneo la jeshi kikosi cha Lugalo bila taarifa.
Kilichotokea ni kwamba tangu siku hiyo wanajeshi walilizuia eneo hilo la kilima cha Posta Kawe kutotumika tena na wananchi wakati wakizuia na baadhi ya vifaa vya manispaa ikiwemo tingatinga.
lakini tetesi zinasema kwamba baada ya baadhi ya wanajeshi kuywasiliana na Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Ukwamani kujua kwa nini ilichukua uamuzi wa kwenda kulichonga eneo lake bila taarifa, ofisi hiyo haikuwa na taarifa na ilielezwa kwamba Londa alichukua uamuzi bila kuwashirikisha.
Taarifa zilizopo ni kwama leo serikali ya mtaa inajiandaa kupelekea barua kuomba ruhusa ya kuachiwa kwa eneo hilo kutumika kama ilivyokuwa awali kwani sasa wananchi wanataabika kwa kushuka bondeni 'Shoko' na kupandisha hadi njia panda na baadae kuelekea Kawe.
Ikumbukwe kwamba awali eneo la kituo cha njia panda kilifungwa na jeshi baada ya kuwepo kwa tuhuma kwamba vitendo vya ukabaji na uporaji kwa wapita njia vilikuwa vikifanywa a baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 34 KJ cha kambi ya Lugalo.
Wakati utawala bora ukihamasisha, Londa anakiuka kwa uroho wa madaraka na kuchukua sheria mikononi mwake jambo linalowasababishia tabu wananchi badala ya ahueni.
Kama kuna mtu ana fahamu kilichoendelea zaidi kwa siku ya leo basi atujulishe zaidi.