Londa awachonganisha wakazi wa Kawe na wanajeshi


W

Walivyo

Member
Joined
Dec 8, 2009
Messages
11
Likes
1
Points
0
W

Walivyo

Member
Joined Dec 8, 2009
11 1 0
Mwishoni mwa wiki iliyopita Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa alijichukulia hatua mikononi na kwenda kulisawazisha eneo la jeshi pale Kawe Posta ili kuwapa unafuu wakazi wanaokatisha eneo hilo kuja Kawe ama kwenda Mbezi.

Lakini kitendo hicho kilichotafsiriwa na wengi kama mchakato wake wa kutafuta tena kura kutoka kwa wananchi wa kata hiyo kilileta tafrani baada ya unafuu baada ya wanajeshi kulizingira tingatinga la manispaa hiyo kwa kuingia na katika eneo la jeshi kikosi cha Lugalo bila taarifa.

Kilichotokea ni kwamba tangu siku hiyo wanajeshi walilizuia eneo hilo la kilima cha Posta Kawe kutotumika tena na wananchi wakati wakizuia na baadhi ya vifaa vya manispaa ikiwemo tingatinga.

lakini tetesi zinasema kwamba baada ya baadhi ya wanajeshi kuywasiliana na Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Ukwamani kujua kwa nini ilichukua uamuzi wa kwenda kulichonga eneo lake bila taarifa, ofisi hiyo haikuwa na taarifa na ilielezwa kwamba Londa alichukua uamuzi bila kuwashirikisha.

Taarifa zilizopo ni kwama leo serikali ya mtaa inajiandaa kupelekea barua kuomba ruhusa ya kuachiwa kwa eneo hilo kutumika kama ilivyokuwa awali kwani sasa wananchi wanataabika kwa kushuka bondeni 'Shoko' na kupandisha hadi njia panda na baadae kuelekea Kawe.

Ikumbukwe kwamba awali eneo la kituo cha njia panda kilifungwa na jeshi baada ya kuwepo kwa tuhuma kwamba vitendo vya ukabaji na uporaji kwa wapita njia vilikuwa vikifanywa a baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 34 KJ cha kambi ya Lugalo.

Wakati utawala bora ukihamasisha, Londa anakiuka kwa uroho wa madaraka na kuchukua sheria mikononi mwake jambo linalowasababishia tabu wananchi badala ya ahueni.

Kama kuna mtu ana fahamu kilichoendelea zaidi kwa siku ya leo basi atujulishe zaidi.
 
M

Mike 1234

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Messages
1,634
Likes
4
Points
0
M

Mike 1234

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2009
1,634 4 0
inasikitisha sana, sijui lini watz tutaamka na kuchagua viongozi wa kweli bila kudanganywa na vitu ambavyo havina msingi kama hivi,na kweli kawe wakimpitisha tena huyu jamaa basi nitaamini kuna uganga, by the way watu wanapita pale kama kawaida inaonekana jeshi wameelewa somo na kuwaruhusu waendelee kutumia njia
 
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
5,173
Likes
652
Points
280
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
5,173 652 280
Poleni wakazi wa Mbezi juu... Na kwa jinsi ambavyo jiografia ya hapo Corner ya "Dito" ajali zaweza kuongezeka...
 
ABEDNEGO

ABEDNEGO

Senior Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
109
Likes
2
Points
0
ABEDNEGO

ABEDNEGO

Senior Member
Joined Aug 20, 2009
109 2 0
Londa huyu tena ??Mjumbe wa NEC!!!!
 
W

Walivyo

Member
Joined
Dec 8, 2009
Messages
11
Likes
1
Points
0
W

Walivyo

Member
Joined Dec 8, 2009
11 1 0
Hili la uganga hata silishangai, jamaa maarufu kwa visomo pale kwake. Hata Jumamosi usiku kulikuwa na kisomo na dua. Ingawa baadhi ya watu wa Kawe nasikia wamestuka na kususia kwenda, mheshimiwa amekuwa akiwachukua wahudhuriaji kutoka mafia kwa kia ili kusherehesha shughuli yake.
 
Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Messages
2,100
Likes
34
Points
0
Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2010
2,100 34 0
Mjini pagumu unadhani ataleaje watoto wa nyumba ndogo?
 

Forum statistics

Threads 1,250,033
Members 481,189
Posts 29,718,777