Logical fallacy: Appeal to the authority, ‘argumentum ad verecundiam’

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Hili ni kosa la ufikiri ‘logical fallacy’ ambayo huona usahihi kwenye jambo kwa kuwa mtu mmoja mwenye mamlaka au mtu mashuhuri amesema, bila kuangalia kama mtu husika ana utaalamu au amefanya tafiti juu ya jambo husika

Kosa hili baadhi ya ‘Logicians’ wanalivunja hadi kufika ngazi ya chini kabisa kwa mtu mmoja mmoja. Kwa mfano, watoto wanapocheza mpira halafu, wanabishana kuhusu goli, kisha mwenye mpira ndiyo anakuja kuamua kama ni goli au si goli, na wote watamsikiliza, sio kwa sababu yuko sahihi bali kwa sababu ndio mwenye mpira

Katika ufikiri ukishafahamu hili, unajua ya kuwa usahihi haupo kwa mtu maarufu au mwenye mamlaka. Bali usahihi upo kwenye ushahidi usio na shaka, uliochujwa kitaalamu na kujaribiwa. Maisha sio mazoezi kuna makosa hudumu

FAIDA ZA APPEAL TO AUTHORITY

Kosa hili ni muhimu kibiashara, yaani kuna biashara zinataka utaalamu kuelezewa lakini kwenye masoko mtu anaweza kumtumia mtu maarufu kutangaza biashara yake na watu wakanunu bila kujiuliza zaidi

Mfano: Mtu maarufu anaweza kuwa kwenye tangazo la dawa, kama Hedex, then anakuambia tumia hedex, utakubali kwa sababu ni maarufu sio kwa sababu anautaalamu juu ya masuala ya dawa

Baada ya watu kufahamu kuhusu kosa hili, wale vijana waliokuwa wanapata kipato kupitia 'umodel' wampeungua sana kwa kuwa umodel hauna impact sana kwenye masoko kama watu maarufu wanavyoweza kuleta matokeo chanya

Hii ndio sababu watu maarufu hupewa ubalozi wa makampuni na hutumika kwenye kampeni mbalimbali

Faida nyingine zitafute mwenyewe


HASARA

Hasara ya kumfuata mtu asiye na ufahamu kuhusu jambo husika ni sawa tu na kipofu kumfuata kipofu, kwa kuwa wao huenda kwa kubahatisha akikosea mmekosea wote na mkapotea wote.

Kwenye uwanja wa fikra, kinachotakiwa ni fikra, ushahidi na sio mamlaka au historia.

Ile hali ya kudhani kwa kuwa ulifanya tafiti fulani basi majibu ya tafiti husika yawe kuwa majibu hata ya tatizo jipya,

Hell No!


Signed

Oedipus
 
Mbona umeongea fact tupu!!
kuna wapuuzi wamejipatia mali au ushindi wa kesi mbalimbali kisa mamlaka au elimu ambayo haihusiani na shauri.

Hali hii inawaathiri watu masikini na wale wasio na mamlaka.Kwa kijijini ujinga huu ni mwingi kiasi kwamba wengine huamua kuacha kudai/kujitetea kisa mtesi wake ni flani.

Wanasheria/wanaharakati mliohitimu tumieni fursa kwa kununua kesi kama hizi kisha mpewe comission!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom