Logic Mindset vs Biblical Mindset: Mfia dini njoo 🫴🏻.

Logic Mindset vs Biblical Mindset: Mfia dini njoo 🫴🏻.

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
2,287
Reaction score
4,507
Jamani, hadithi ya Kaini na Habili inakwamisha kidogo ikiwa tukaangalia kwa logic. Kaini anaua Habili, kisha anapelekwa katika nchi ya Nodi, eneo lililokuwa mbali na Edeni. Swali ni, Nodi ilitoka wapi wakati Adam na Hawa walikuwa wanadamu pekee?

Kisha, Kaini ana mke, na kwa kuwa wote walitoka Adam na Hawa, mkewe lazima awe ndugu yake. Hii kimsingi inafanya kazi kihesabu, lakini kimaadili na kwa mtazamo wa leo inakinzana. Biblia pia inasema Kaini akajenga mji wa Henoko, lakini mji ukiwa na watu wachache sana, je, ni nani aliyeishi hapo? Kwa kweli, baadhi ya mambo hayaeleweki literal labda ni symbolic, ikituonyesha fundisho kuhusu wivu, adhabu, na uzao wa binadamu.

Personally the bible isn't 100% true if misses something, ukitumia logic kuuliza hivi vitu havina majibu. Pengine wafia dini tusaidizane
 
Mm sio mfia Dini.
Ila ngoja nijaribu kujibu ninavyoelewa.

Bila shaka Adam alizaa wana weng zaid na sio Kaini na Habil pekeyake.

Mwanzo 5 :4-5
"Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake."

Hapa unamuona mtoto mwingine wa Adam.Sethi. kwahiyo ukiacha hawa watatu unaona alizaa wengne wake kwa waume.

Ingawa Biblia haisemi waziwazi kwamba mke wa Kaini alikuwa binti ya Hawa.

Mke wa Kaini anatajwa baada ya Kaini kufukuzwa, na muda mredu ulipita.
Kwahiyo yawezekana kuwa huyo Mke alikuwa mmoja wa wajukuu wa Adamu na Hawa..

Kwahiyo alioa mtoto wa ndugu yake.
 
Still doesn't make sense bro, according to the bible Yani unavyosikia nchi unaelewa maana yake nini, pia ukisoma bibilia imeandikwa kuwa akamtafuta mkewe kwenye hiyo nchi how comes??

Kwakuwa dada ni dada yake angishi kwenye nchi moja na Adamu.
 
Nchi ni sehem. Usichukulie kwa muktadha wa ukubwa kama ilivyo leo.
"Mungu alimtoa Adam kwenye nchi ya Eden."

Pia hapa anasema
Mwanzo 4:15
[15]BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga."

Hapa ni baada ya Kaini kumuua Abel.
Ina maana kama wangekuwa watu wanne tu (Adam, Hawa, Kain na abel) na baadae Habil kuuliwa wangebaki watatu.
Kwahiyo kusingekuwa na haja ya kuwekwa alama Kaini ili asiuliwe na watu.

Hii inaonyesha kuwa Walikuwepo watu wengne Kipind hiki cha Kaini.
Watu wengine waliozaliwa na Hawa na Adam.

Alaf hapa
Mwanzo 4:16
[16]Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.

(Usichukulie nchi kwa ukubwa huu wa sasa na pia unaona alikaa karibu eden . Ina maana karibu na Ndugu zake).

Ndio maana nikasema huenda Alimuoa mmoja wa watoto wa hao ndugu zake.

Kumbuka ni kipind kirefu kilipita. Sio jambo la miaka 10 au 20.

Kaini na ndugu yake Abeli walikuwa wa kwanza kati ya watoto kadhaa waliozaliwa na Hawa.
Na hawa watoto walioana wenyewe kwa wenyewe.
 
Utaambiwa biblia inasomwa ki roho
Ni ukweli hata hivyo.

Biblical Mindset, msingi wake ni Imani, na Imani haiitaji uthibitisho wa nje wala logic, inahitaji kujua na kupokea.

Kwenye mada, Inawezekana kabisa Kaini alioa ndugu yake, ingawa watoto wakike hawakuwa wanatajwa/kuandikwa kwa utaratibu wao kipindi hicho only in exceptions.
Ukiangalia hata kipindi cha kina Ibrahim ingawa watu walikuwa wengi tayar duniani, ila bado walioana ndugu, kama Ibrahim na Sarah.
Hata Isaka alioa binamu, sawa na Yakobo n.k

Kinachoweza kuchanganya ni mpangilio wa simulizi tu, na hii inaathiriwa na muda kilipoandikwa kitabu hicho cha Mwanzo pamoja na mazingira ya wakati huo kinaandikwa.
 
Jamani, hadithi ya Kaini na Habili inakwamisha kidogo ikiwa tukaangalia kwa logic. Kaini anaua Habili, kisha anapelekwa katika nchi ya Nodi, eneo lililokuwa mbali na Edeni. Swali ni, Nodi ilitoka wapi wakati Adam na Hawa walikuwa wanadamu pekee?

Kisha, Kaini ana mke, na kwa kuwa wote walitoka Adam na Hawa, mkewe lazima awe ndugu yake. Hii kimsingi inafanya kazi kihesabu, lakini kimaadili na kwa mtazamo wa leo inakinzana. Biblia pia inasema Kaini akajenga mji wa Henoko, lakini mji ukiwa na watu wachache sana, je, ni nani aliyeishi hapo? Kwa kweli, baadhi ya mambo hayaeleweki literal labda ni symbolic, ikituonyesha fundisho kuhusu wivu, adhabu, na uzao wa binadamu.

Personally the bible isn't 100% true if misses something, ukitumia logic kuuliza hivi vitu havina majibu. Pengine wafia dini tusaidizane

Ndugu yangu, maswali unayouliza ni ya msingi sana kwa mtu anayesoma Biblia kwa mtazamo wa mantiki ya kawaida. Lakini kumbuka, Biblia haikuandikwa kama kitabu cha historia ya kisayansi bali kama mwongozo wa kiroho unaobeba ujumbe wa imani. Ndiyo maana kuna mambo ambayo kwa logic ya sasa yanaonekana kama hayana majibu ya moja kwa moja, lakini kimsingi yana maana ya kiroho inayotufundisha.

Kuhusu nchi ya Nodi, Biblia haisemi kwamba kulikuwa tayari na watu huko. Inaweza kuwa ni jina lililotolewa kwa eneo ambalo Kaini alienda kuishi baada ya kuondolewa karibu na Edeni. Hivyo hoja kwamba “kulikuwa na nani” haina msingi mkubwa, bali maana yake ni kwamba Kaini alitengwa na familia yake na kupelekwa mbali zaidi.

Swali la mke wa Kaini pia linachukuliwa vibaya tukipima kwa kigezo cha maadili ya leo. Mwanzo, wanadamu wote walitokana na Adam na Hawa, na ili kizazi kiendelee kuenea, kulikuwa na ndoa za kifamilia. Baadaye Mungu alipoendelea kuweka sheria na miongozo, ndoa hizo zikakatazwa. Hii inaonyesha mpito wa mwanzo wa binadamu kuelekea kwenye jamii yenye kanuni thabiti.

Hata pale Biblia inaposema Kaini alijenga mji, haimaanishi mji mkubwa kama tunavyoujua leo. Wakati ule watu waliishi miaka mingi sana, na kizazi cha Adam kiliongezeka kwa haraka. Mji huo unaweza kuwa ulikuwa ni makazi ya familia na uzao wa Kaini, ambao baada ya miaka mingi walijikusanya na kuunda jamii.

Kwahiyo, hadithi ya Kaini na Habili sio tu simulizi ya kihistoria, bali ni funzo la kiroho. Inatufundisha kwamba wivu na hasira vinaweza kuzaa dhambi kubwa, Mungu huchukia damu ya asiye na hatia, na hata mwenye dhambi bado anaachwa kuishi kwa ajili ya mpango wa Mungu kutimia. Tukisoma kwa mtazamo wa logic tutabaki na maswali mengi yasiyokuwa na majibu, lakini tukisoma kwa mtazamo wa Biblia, tunaona hekima, fundisho na mwongozo wa maisha ya kiroho.
 
Back
Top Bottom